Lipumba aondoka nchini baada ya kujiuzulu

wana jukwaa.
naomba kwa unyenyekevu tujadili hili swala la prof. kujiuzuru na kukimbia nchi..
nisingependa kuhoji kuhusu tuhuma alizozotoa kwa viongozi wenza wa ukawa..yah me nakubaliana nae tena zaidi ya 80%.

lipumpa amekuwa mwenyekiti wa cuf zaidi ya miaka 16 akiwa kiongozi mkuu tena wa chama cha upinzani.. kiundani anajua mateso na wakati mgumu unaowakumba viongozi wa upinzani hasa kwa nchi za kiafrika nadhani nae watakuwa mhanga.. lakini kwa mtu anayetaka mabadiliko huwa anazipokea changamito zote na kuziishi akitegemea ipo siku atayaona mabadiliko.
juzi tu mda mchache baada ya kujiuzuru alikwea pipa na kwenda majuuu... swali langu ni je hayo mabadiliko anaenda kuyapigania akiwa nje ya nchi.. je. kama kuna uozo aliuona ndani ya upinzani yeye kama mtu msafi ajitoa na kusema siasa basi wakati amekuwa mpiganaji miaka mingi??? je amemwacha nani anayemwamini atapampana na chama tawala??
Mkuu,
1.Ungemsikiliza vizuri Lipumba wakati anajiuzulu baadhi ya maswali usingeuliza ,Alishasema anafanya nini baada ya kujiuzulu
2.Sikuzote kama hukubaliani ni itikadi,ilani,sera na mwendendo wa chama njia pekee huwa ni kujiuzuru ili usiwe mmoja kati ya wanaosimamia na kupitisha yale usiyoyaamini
 
https://youtu.be/0_ZoVp0oPDI

Jee escrow imemnunua lipumba?
Fedha za ufisadi za escrow zimemnunua Lipumba. Hakuweza kujizuia na ushawishi wa mabillion ya bure.....video hio akimkaribisha Lowassa leo...anakuja na cinema nyengine
Mkuu Lipumba ni binadamu sio malaika,YES alimkaribisha Lowassa lakini si ameshasema kwa nini msimamo wake umebadilika,hebu fikiria mkuu
 
Kwa taarifa yako lipumba alikua mhimili mkubwa ukawa. Cuf wameanza kuhamia ACT. Ukawa inakufa. Yetu macho
Inakufa UKAWA au CUF? kwani katika UKAWA, CUF inauhitaji sana UKAWA kuliko UKAWA inavyoihitaji CUF
 
Mkuu,
1.Ungemsikiliza vizuri Lipumba wakati anajiuzulu baadhi ya maswali usingeuliza ,Alishasema anafanya nini baada ya kujiuzulu
2.Sikuzote kama hukubaliani ni itikadi,ilani,sera na mwendendo wa chama njia pekee huwa ni kujiuzuru ili usiwe mmoja kati ya wanaosimamia na kupitisha yale usiyoyaamini

Mkuu Lipumba ni binadamu sio malaika,YES alimkaribisha Lowassa lakini si ameshasema kwa nini msimamo wake umebadilika,hebu fikiria mkuu

Hebu punguza kukata viuno, jipe muda angalia video hii hapa.

Watch "Prof. Lipumba akiwa Msikitini na Siasa za Tanzania" on YouTube - https://youtu.be/ujwfFUUAD70
 
Mkuu Lipumba ni binadamu sio malaika,YES alimkaribisha Lowassa lakini si ameshasema kwa nini msimamo wake umebadilika,hebu fikiria mkuu

Ni kweli ni binaadam na weakness zetu ni tamaa tu.
Alikua mbele kila kitu kuanzia mwanzo hadi mwisho mpaka siku lowasa anatangaza nia lipumba alikuwepo na kuongea sifa tupu kwa lowasa.
Ni wazi Li proffessa ameuza mechi dakika za majeruhi its shame for him
 
Pg-1-300x220.jpg

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

SAA chache baada ya Profesa Ibrahim Lipumba kutangaza kujiuzulu wadhifa wa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), ametoweka nchini.

Hata hivyo, haikufahamika mara moja amekwenda nchi gani na atakaa kwa muda gani.

Profesa Lipumba aliondoka nchini baada ya kumaliza mkutano wake na waandishi wa habari katika Hoteli ya Peacok jijini Dar es Salaam, ambako alitangaza kujiondoa katika chama chake na katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Taarifa zilizopatikana, baada ya kumaliza mkutano na waandishi, alielekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), na aliondoka nchini kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda (Rwanda Air).

Awali kiongozi huyo ambaye alivaa suti ya ‘dark blue’ na shati jeupe alikuwa apande ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) 485, lakini alibadili mwelekeo baada ya kufika uwanjani na kuamua kupanda Rwanda Air kuelekea Kigali saa 9 alasiri.

Chanzo cha uhakika kutoka uwanjani hapo, kililieleza MTANZANIA kuwa Profesa Lipumba, alifika saa 7:00 mchana akiwa na vijana wawili wa kiume ambao walionekana kama walinzi wake.

Katika muda huo ambao Profesa Lipumba alikuwa katika taratibu za kuondoka, palikuwapo na ndege nne tu za kwenda nje ya nchi.

Vijana hao ambao hawakujulikana majina yao, walikuwa wakifuatilia kila hatua ya kile alichokuwa akikifanya Profesa Lipumba, huku yeye akionekana mwenye wasiwasi na msongo mkubwa wa mawazo.

“Profesa Lipumba anaonekana hayuko katika hali ya kawaida, anaonekana ni mtu mwenye msongo wa mawazo, na pia ana wasiwasi kama vile kuna jambo linamsumbua.

“Macho yake yalionekana ni mekundu mithili ya mtu aliyekuwa akilia kwa muda mrefu, huku uso wake ukionekana hauna furaha,” kilisema chanzo chetu.

Wakati hayo yakiendelea, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amelazimika kukatisha shughuli za kiserikali alizokuwa nazo Zanzibar na kwenda jijini Dar es Salaam kunusuru hali ya sintofahamu ndani ya chama hicho.

“Ndiyo hivyo imeshatokea, lakini tayari katibu mkuu amekuja bara kuhakikisha mambo yanakaa sawa na chama hakiyumbi,” alisema kiongozi wa CUF ambaye hakupenda kutajwa gazetini.
 
yaonekana huyu bwana aliwekwa kati akapelekwa kijeshi jeshi atangaze vile, tusi muhukum ipo siku atasema ukweli,
 
Niliwahi kusema Lipumba ni Mkimbizi wa Kinyarwanda, baba yake alikuja kijana mdogo na akawa anakaa kambi ya Mishamo badae akahamia kambi ya ulyankulu na badae ali settle urambo ambako ndo chimbuko la Lipumba hivyo sishangai kukimbilia nchini Rwanda.
 
Lipumba ni mchumia tumbo na hii inadhihilisha kuwa wana cuf walikuwa wanatwanga maji kwenye kinu
 
View attachment 274342

Anaenda kujificha aibu za watanzania wenye kuhitaji mabadiliko maana alidhani atausambaratisha ukawa kumbe ndio anazidi kuuimarisha
 
Lipumba ni mnafiki sana,tena mtu msomi ?
 
Lipumba ni mchumia tumbo na hii inadhihilisha kuwa wana cuf walikuwa wanatwanga maji kwenye kinu

Lumumba ni pandikizi la CCM kwa upinzani.Aliwekwa pale kuharibu upinzani na kulinda maslahi ya chama tawala.Lowassa ameingia upinzani bila mzaha kwa 100%.Lumumba akajua mbinu zake zimeshajulikana solution ni kujitoa upinzani.
 
Niliwahi kusema Lipumba ni Mkimbizi wa Kinyarwanda, baba yake alikuja kijana mdogo na akawa anakaa kambi ya Mishamo badae akahamia kambi ya ulyankulu na badae ali settle urambo ambako ndo chimbuko la Lipumba hivyo sishangai kukimbilia nchini Rwanda.

Inawezekana hiyo pia
 
Lumumba ni pandikizi la CCM kwa upinzani.Aliwekwa pale kuharibu upinzani na kulinda maslahi ya chama tawala.Lowassa ameingia upinzani bila mzaha kwa 100%.Lumumba akajua mbinu zake zimeshajulikana solution ni kujitoa upinzani.

Nikweli kabisa kakimbia aibu,ila atarudi tu
 
Kuna mambo ya msingi nahitaji kuyafahamu kwenu wachambuzi wa masuala ya siasa... 1. Je, ni vibaya kutofautiana mtizamo na mawazo ndani ya chama chako? Km. ilivyotokea kwa Dr. Nchimbi, Dr. Slaa na sasa Prof. Lipumba 2. Je, ni dhambi kwa mwanachama wa vyama vinavyounda UKAWA kuhama chama?
 
Kuhusu lipumba kuhongwa hela na CCM na Mbowe kununuliwa na Lowassa... imekaaje hii?
 
Jaman wana Jamvi.
Baada ya kujiuzulu uwenyekiti wa CUF prof. inasemekana aliondoka kwenda nje ya nchi. Je prof. kaelekea wapi? au amerudi Washington alikokua mwaka majuzi akifanya kazi UN?
Mwenye nyepesi wadau atujuze shime.
 
Back
Top Bottom