Lipumba: Aomba haki itendeke, amtaka Seif apokee simu zake!

Freyzem

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
10,381
Reaction score
25,272
Hatimae Prof Lipumba amekubali kunyoosha mikono juu na kutaka kufanya mazungumzo na Katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif, amemtaka Maalim Seif kupokea simu zake anazompigia ili ampe kazi na waweze kukijenga chama kwa pamoja!
Aidha Lipumba amekiri wazi kuwa chama hicho chenye makazi yake Buguruni kimekumbwa na ukata wa hali ya juu!
1480353785323.jpg

Huu ni mwendelezo wa sinema za Lipumba, anachohitaji ni ruzuku, baada ya janja yake ya kutaka kufungua akaunti kutibuliwa, akili zinaanza kumrudi baada ya kuisoma namba!!
 
mimemsikiliza huyu ndugu kwenye taarifa ya habari, nikagundua huyu bwana anajua anachokifanya.

Hana hata haibu kwamba alijuvua mwenyewe uenyekiti na sasa anaupigania kwa nguvu zote!

Alafu kuna watu wanamshangilia kama mazuzu, wakati mtu mnae mshangilia aliwaacha mkiwa vitani?
 
Haswa, huyu mtu ni hatari sana na mwenye uchu wa pesa na madaraka!
Alivyosusia uchaguzi na kukimbia, alitegemea kwamba akirudi atapata support?
Nahisi huyu mtu huwa anapiga Kitwanga ndio anakwenda kwenye media...
 
mkuu tangu 1995 cuf haikuwai kupata wabunge zaidi ya m1 tanzania bara.

Ila kwa kujitoa kwake na watu wakapambana kwa nguvu zao chini ya mwenyekiti wa mpito ndugu twaha taslima cuf ikatoka na zaisi ya wabunge 8 tanzania bara leo bila mshipa wa aibu anakuja na kushupaa heti anataka kukujenga chama?

Alikuwa wapi tangu mwaka 1995 mpaka leo ndiyo anataka kukijenga chama kwa kutumia mgongo wa wenzake waliokipigania chama hiki alichokitelekeza kwenye uchaguzi akitarajia kitakufa?

Halafu watu wanamshangilia msaliti? Tanzania kuna maajabu sana tena ni zaidi ya maajabu 7 ya dunia.
 
hata chadema viongozi wake karibu wote awana haya
List of shame
Lowasa wamemtukana sana bila haya ccm wenyewe wamekaa kimya,leo hao hao chadema wanampaka rangi lowasa kila kona ya mtaa kama si laana ni nini,na wafuhasi wamekuwa kama mazezeta hakuna anae hoji huo usafi wa lowassa,ukiwa kijana ndani ya chama cha chadema utakuwa umelishwa limbwata na viongozi wa juu...
 
Kwa sasa huyu mtu hana mvuto kabisa, siasa ilishamkataa!
Hataweza kukijenga chama tena kwa kuwa wanachama wengi hawamtaki,analazimisha kukubalika..
 
Mnao mlaumu lipumba muoneeni huruma jamani.
Hivi haya maisha magumu mnadhani yapo kwenu tu? atakula wapi? amepata sehemu ya kujistiri.
Hivi hamuoni wazee wenzake kina Wahasira wameamua kujenga viota mahakamani?
Hali ngumu Wakuu.
 
Hatimae Prof Lipumba amekubali kunyoosha mikono juu na kutaka kufanya mazungumzo na Katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif, amemtaka Maalim Seif kupokea simu zake anazompigia ili ampe kazi na waweze kukijenga chama kwa pamoja!
Aidha Lipumba amekiri wazi kuwa chama hicho chenye makazi yake Buguruni kimekumbwa na ukata wa hali ya juu!
View attachment 440780
Huu ni mwendelezo wa sinema za Lipumba, anachohitaji ni ruzuku, baada ya janja yake ya kutaka kufungua akaunti kutibuliwa, akili zinaanza kumrudi baada ya kuisoma namba!!

Tangu awali kabisa Prof Amekuwa akitaka Maalim Seif wakutane lakin Maalim amekuwa akikaza ndio sababu Leo kaniambia kuwa Maalim asijidanganye wala asikubali kudanganywa na Mtu ajue kabisa Prof ni Mwenykt mpaka 2019 ikiwa atakuwa Hai
 
Mnao mlaumu lipumba muoneeni huruma jamani.
Hivi haya maisha magumu mnadhani yapo kwenu tu? atakula wapi? amepata sehemu ya kujistiri.
Hivi hamuoni wazee wenzake kina Wahasira wameamua kujenga viota mahakamani?
Hali ngumu Wakuu.
mkuu hivi ni kweli ndugu kaamia ofcn buguruni? Anapiga mbonji kabisa pale? Tehe tehe kusoma siyo kuwin maisha haaaaaaaaaaa.
 
hata chadema viongozi wake karibu wote awana haya
List of shame
Lowasa wamemtukana sana bila haya ccm wenyewe wamekaa kimya,leo hao hao chadema wanampaka rangi lowasa kila kona ya mtaa kama si laana ni nini,na wafuhasi wamekuwa kama mazezeta hakuna anae hoji huo usafi wa lowassa,ukiwa kijana ndani ya chama cha chadema utakuwa umelishwa limbwata na viongozi wa juu...
Hiyo ilishachuja,unapuuzwa tu
 
Tangu awali kabisa Prof Amekuwa akitaka Maalim Seif wakutane lakin Maalim amekuwa akikaza ndio sababu Leo kaniambia kuwa Maalim asijidanganye wala asikubali kudanganywa na Mtu ajue kabisa Prof ni Mwenykt mpaka 2019 ikiwa atakuwa Hai
Na Maalim kakaza kwa sababu ya jinsi yeye Lipumba alivyofanya wakati ule wa uchaguzi, kama asingesusia wakati ule leo yangekuwa yakizungumzwa mengine!
Btw kwani huo uenyekiti uchwara utamsaidia nini zaidi ya chama kuendelea kugawanyika? Huo ukata unamfanya aombe huruma kwa Seif ili wapate ruzuku, ambayo ndio huwa anaitegemea!
Seif hana ukata...
 
Kama huzijui siasa za Tanzania unaweza kumlaumu leo Lipumba akamsamehe Sefu.

Hawa ndugu wanacheza na akili zetu ninaimani kila mmoja anahamu ya kuwasiliana na mwenzie.

Sasa je wataanza vipi? hapo ndio panahitajika kuwajenga watu kisaikolojia kwanza Kabala ya kukutana kwao rasmi.

Ndio maana jana Sefu kasema yupo tayari kuyajadili na Lipumba, leo Lipumba anasema Sefu hapokie simu zake ili ampangie kazi.....lakini mwisho wa siku wote kwa pamoja wanalilia ruzuku iliyokatwa na msajili.

Hawa jamaa ninaimani kuna mawasiliano ya chini chini yanaendelea, ila wapo kutuandaa kisaikolojia kwanza kabla ya kumaliza bifu lao na hatimaye msajili aruhusu mrija wa ruzuku ndani ya chama.

Muda sio mrefu Lipumba na Sefu watakumbatiana, na vijana kama kawaida mtawashangilia.

"Usimwani mwanasiasa awe upinzani au chama tawala".......by Zitto.
 
hata chadema viongozi wake karibu wote awana haya
List of shame
Lowasa wamemtukana sana bila haya ccm wenyewe wamekaa kimya,leo hao hao chadema wanampaka rangi lowasa kila kona ya mtaa kama si laana ni nini,na wafuhasi wamekuwa kama mazezeta hakuna anae hoji huo usafi wa lowassa,ukiwa kijana ndani ya chama cha chadema utakuwa umelishwa limbwata na viongozi wa juu...
Ccm imelaghai Watanzania kwa miaka mingi sana,na bado inazidi kuvurunda!
 
Back
Top Bottom