Prof. Lipumba aunguruma Zanzibar. Amtaka Maalim Seif kujirudi

Jul 29, 2018
9
4
PROF LIPUMBA AMTAKA MAALIM SEIF KUJIRUDI

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahimu Lipumba amesema chama chicho kipo tayari kushiriki katika uchaguzi mdogo wa uwakilishi katika jimbo la Jang'ombe.

Akizungumza na Wanachama pamoja na viongozi wa CUF wanaomuunga mkono kwa upande wa Zanzibar Prof Lipumba amesema hawawezi kuendelea na siasa za kususia chaguzi mbalimbali zinazoendelea nchini hivyo wanachama wajipange kuweza kushiriki katika uchaguzi mdogo wa marejeo katika jimbo la Jang'ombe.

“Kamwe hatuwezi kila siku kuacha kushiriki katika uchaguzi wowote jambo ambalo linapelekea kushusha imani na hadhi ya chama chetu” alisema Prof. Lipumba.

Aidha prof Lipumba amesema kuwa chama cha CUF kinauwezo kubwa wa kushinda uchanguzi ujao wa mwaka 2020 endapo viongozi na wafuasi wa chama hicho watashirikiana katika kukijenga chama na kuondoa matabaka yanayochangia kukiyumbisha chama hicho wakati huu.

Amesema 2020 CUF watashiriki uchaguzi kwa kusimamisha viongozi kwa ngazi zote Urais, Ubunge, Udiwani na Uwakilishi ili kuweza kuwapa haki yao ya kikatiba na kuweza kusimamia na kulinda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Hata hivyo Amesema chama cha wananchi Cuf kitaendelea kuunga mkono Upatikanaji wa serikali ya Umoja Wa kitaifa na muungano wa serikali ya TATU.

Prof. Lipumba amemtaka maalim seif sharif hamadi kujirudi na kuacha kuendelea na siasa zisizokuwa na tija kwa taifa badala yake ajirudi na kuendeleza chama kwa misingi iliyowekwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya mjini amesema imefika wakati cuf ikatae siasa za ubaguzi ambazo hazina faida yoyote kwa taifa.

"Tumechoka kubaguliwa huyu mbara , huyu mzanzibar, huyu mpemba na huyu muunguja" alisema mwenyekiti huyo wa cuf wilaya ya mjini unguja.

Mkutano huo wa viongozi na wanachama umefanyika katika ukumbi wa beit-lyamini bwawani mjini unguja.
 

Attachments

  • FB_IMG_1534486737792.jpg
    FB_IMG_1534486737792.jpg
    63 KB · Views: 28
  • FB_IMG_1534486728385.jpg
    FB_IMG_1534486728385.jpg
    66.5 KB · Views: 29
2020 anaelekea jikoni maana ruzuku iliyotafutwa na akina Maalim ndo itakuwa mwisho. Mtatiro nae ameelekea huko ili asaidie kushawishi wakubwa pesa iwe inatoka kwa wakati maana Prof ana kazi nayo maalum.
 
Eti lipumba aunguruma Zanzibar, sema lipumba aongea Zanzibar, mwenye kuunguruma Zanzibar ni maalim seif peke yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom