Wabunge CUF wajisalimisha kwa Lipumba

Wabunge CUF wajisalimisha kwa Lipumba

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
1553198809608.png

MBUNGE wa Kilwa Kusini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Suleiman Bungara maarufu Bwege amekuwa mbunge wa pili kutangaza rasmi kuingia kambi ya Profesa Ibrahim Lipumba ambayo sasa ndio inaongoza CUF. Bwege alikuwa mmoja wa wabunge waliokuwa wakiunga mkono iliyokuwa kambi ya CUF - Maalim iliyokuwa ikiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye amehamia ACT- Wazalendo.

Maalim Seif na mwasisi mwenzake wa CUF, Profesa Lipumba waliingia kwenye mgongano wa kimaslahi uliokia hatua ya kuwagawa wabunge wa chama hicho. Mgawanyo uliozalisha CUF ya Maalim Seif na ile ya Lipumba. Huku mvutano huo ukiendelea Osi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ilimtambua Profesa Lipumba kuwa ndio kiongozi wa chama hicho hali iliyosababisha Maalim kufungua kesi Mahakama Kuu kutaka kutengua utambuzi wa Osi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa CUF ya Lipumba, kesi ambayo Maalim alishindwa.

Huku Maalim Seif akishindwa kesi hiyo, Profesa Lipumba ameidhinishwa na Mkutano Mkuu wa CUF uliotishwa na Baraza Kuu la CUF kuwa Mwenyekiti wa chama hicho ambapo ameingia madarakani na uongozi wake na kwa sasa hatma ya wabunge hao waliokuwa upande wa Maalim Seif inadondokea mikononi mwake.

Mbunge Bwege ameamua kuweka wazi utayari wake wa kufanya kazi na Lipumba, akiliambia gazeti hili kuwa hana sababu ya kusita kufanya hivyo kwani yeye ni mtumishi wa wananchi wa Kilwa waliomchagua kupitia CUF na kwa kuwa CUF iliyobakia ya Lipumba, analo jukumu na kuendeleza mapambano ya kupigania haki chini yake.

“Ninachoweza kusema ni kuwa uamuzi wa Maalim kuhamia ACT ni wa kwake yeye mwenyewe kwa kuwa ana maamuzi yake na mie ninayo yangu,” alisema Bwege ambaye ni mmoja wa wabunge machachari na wachangiaji bungeni. Mbunge mwingine aliyejitokeza ni Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali ambaye juzi alika osi kuu za CUF Tanzania Bara, Buguruni jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa anataka kuendeleza mapambano ya kupigania haki yanayoendeshwa na CUF na kuwa anaendelea na Lipumba kufanya kazi hiyo.

Bobali alisema amerudi nyumbani na kwamba wapo wengi watakaorudi kuungana na Profesa Lipumba na kuwa sasa ni wakati wa kukijenga chama na waliondoka kwenda sehemu nyingine ni utashi wao. “Nimerudi nyumbani baada ya msuguano uliodumu kwa miaka mitatu ndani ya CUF na uliokidhoosha chama, nawaomba mnisamehe kwa yaliyotokea,” alisema.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya alibainisha kuwa chama hicho kinawakaribisha wanachama na wabunge waliokuwa upande wa Maalim Seif na kuwataka kujitangaza kuwa wanaungana na CUF Lipumba. Alibainisha kuwa wabunge wote wa CUF kwa sasa wapo chini ya Lipumba na wanatakiwa kwenda kwenye osi za chama na kuelezea nia yao ya kufanya kazi na mwenyekiti huyo huku akitahadharisha kuwa watakaokiuka na kuanza kuzungumzia chama vibaya pembeni watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

“Kwanza sisi kama uongozi tulikuwa tunataka kuwaita wote kuka makao makuu ya chama mara moja kuwahoji nia yao ya kuendelea kufanya kazi nasi au hapana, lakini kwa kile tunachoona kimeanza kujitokeza ni kizuri kwa kuwa wapo ambao wameanza kutupigia simu kuomba kurejea,” alisema Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kaliua mkoani Tabora kupitia CUF. Katibu Mkuu wa CUF, Khalifa Suleiman Khalifa alithibitisha uwezekano wa wabunge waliotangaza kumuunga mkono Maalim Seif kuitwa kwenye makao makuu ya Buguruni kusikilizwa msimamo wao.

Wabunge hao 22 wanatokea visiwani Zanzibar huku Bara walikuwa wanne ambao hadi sasa wapo walikwisha weka wazi utayari wao wa kufanya kazi na Profesa Lipumba huku wengine ndio wanangojewa. “Idadi yao ndio hiyo na wanangojewa msimamo wao kwa kuwa tumeshasema kuwa sie uongozi wa CUF wa sasa tupo tayari kupigania maendeleo na wao kwa kuwa ni wabunge chini yetu basi kwa sasa warejee tujenge chama na kukabiliana na tofauti zetu,” alisema Khalifa.

John Gagarini kutoka Kibaha, anaripoti kuwa Chama cha ACT - Wazalendo Mkoa wa Pwani kimefurahishwa na kujiunga kwa Maalim Seif, na kusema kwao huo ni mtaji mkubwa hasa katika kipindi cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa Vijiji na Vitongoji kwa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa mwakani. Akizungumza na waandishi wa habari osini kwake mjini Kibaha, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa, Mrisho Swagala amesema Maalim Seif kujiunga na chama chao kwao ni kama kupata dhahabu ambayo ilikuwa inachezewa na wengine na amejiunga wakati mwafaka kuelekea uchaguzi.

Swagala amesema Seif ni kiongozi mwenye ushawishi mkubwa nchini hivyo anaamini wao wamepata dhahabu na ndiyo mwanzo wao kuwa chama kikubwa cha upinzani nchini tofauti na kilivyokuwa zamani na kuamini kuwa watafanya vizuri kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwakani. “Tunaamini tumepata mtu ambaye anakwenda kukinyanyua chama chetu kwani tumeona kule Zanzibar alivyoweza kuwa na wabunge wengi na kukaribia kushinda nafasi ya Urais licha kushindwa kwa kura chache kila alipokuwa akiwania nafasi hiyo hivyo kupitia ACT atafanya vizuri zaidi,” amesema Swagala.

Amesema hata kwa Bara, Maalim Seif anakubalika kwani hata baadhi ya wafuasi wa CUF mkoani Pwani wameonekana nao kujiunga na ACT ili kumuunga mkono kiongozi huyo wa upinzani baada ya kujiengua kwenye chama hicho baada ya kutoelewana na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba
 
Sasa ulitegemea nini hapo?akiondoka CUF saa hizi anazidi kutuletea umaskini wa billion 4 za uchaguzi wa marudio.Ila ataenda ACT mwakani
That's so considerate of him and remaining CUF MPS's
 
Wajiandae tu kujiunga na ACT wazalendo mwakani mwezi wa Sita.
Atakayebaki CUF hataweza kupata hata udiwani.

ACT wazalendo kitakua chama kikuu cha upinzani kitakachopata wabunge wasiopungua 35 wa kuchaguliwa.
Cuf ikijitahidi sana itapata Mbunge mmoja tuu.

Na pia kuna uwezekano wa kukosa kabisa labda waachiane majimbo na CCM vinginevyo moto wa UKAWA mwakani utakua ni hatari kubwa sana.

Ni wakati sasa wa Zito kuanza ziara kwenye ngome zote za CUF na kupokea wanachama.
Anzia Mtwara ,Lindi, Temeke, Pwani, Tanga,Tabaora na Morogoro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo nilikuwa nampinga kesho nami nitatangaza kuungana nae ili nimalizie muda wangu...Nitimkie ACT.......
 
Ila bora wabaki Kwa Lipumba maana awajui kesho yao waweza wasirudi Tena bungeni ukakosa huku na huko
 
Wajiandae tu kujiunga na ACT wazalendo mwakani mwezi wa Sita.
Atakayebaki CUF hataweza kupata hata udiwani.

ACT wazalendo kitakua chama kikuu cha upinzani kitakachopata wabunge wasiopungua 35 wa kuchaguliwa.
Cuf ikijitahidi sana itapata Mbunge mmoja tuu.

Na pia kuna uwezekano wa kukosa kabisa labda waachiane majimbo na CCM vinginevyo moto wa UKAWA mwakani utakua ni hatari kubwa sana.

Ni wakati sasa wa Zito kuanza ziara kwenye ngome zote za CUF na kupokea wanachama.
Anzia Mtwara ,Lindi, Temeke, Pwani, Tanga,Tabaora na Morogoro

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo mbunge mmoja atatokea wapi?
 
Bwege hana cha kukosa. Yeye tayari ameshaonesha nia ya kutogombania ubunge mwaka 2020. kwahiyo sio ajabu kwake kuelemea upande wa Lupumba. ila 2020 atakuwa mwanachama wa ACT
 
View attachment 1050788

MBUNGE wa Kilwa Kusini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Suleiman Bungara maarufu Bwege amekuwa mbunge wa pili kutangaza rasmi kuingia kambi ya Profesa Ibrahim Lipumba ambayo sasa ndio inaongoza CUF. Bwege alikuwa mmoja wa wabunge waliokuwa wakiunga mkono iliyokuwa kambi ya CUF - Maalim iliyokuwa ikiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye amehamia ACT- Wazalendo.

Maalim Seif na mwasisi mwenzake wa CUF, Profesa Lipumba waliingia kwenye mgongano wa kimaslahi uliokia hatua ya kuwagawa wabunge wa chama hicho. Mgawanyo uliozalisha CUF ya Maalim Seif na ile ya Lipumba. Huku mvutano huo ukiendelea Osi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ilimtambua Profesa Lipumba kuwa ndio kiongozi wa chama hicho hali iliyosababisha Maalim kufungua kesi Mahakama Kuu kutaka kutengua utambuzi wa Osi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa CUF ya Lipumba, kesi ambayo Maalim alishindwa.

Huku Maalim Seif akishindwa kesi hiyo, Profesa Lipumba ameidhinishwa na Mkutano Mkuu wa CUF uliotishwa na Baraza Kuu la CUF kuwa Mwenyekiti wa chama hicho ambapo ameingia madarakani na uongozi wake na kwa sasa hatma ya wabunge hao waliokuwa upande wa Maalim Seif inadondokea mikononi mwake.

Mbunge Bwege ameamua kuweka wazi utayari wake wa kufanya kazi na Lipumba, akiliambia gazeti hili kuwa hana sababu ya kusita kufanya hivyo kwani yeye ni mtumishi wa wananchi wa Kilwa waliomchagua kupitia CUF na kwa kuwa CUF iliyobakia ya Lipumba, analo jukumu na kuendeleza mapambano ya kupigania haki chini yake.

“Ninachoweza kusema ni kuwa uamuzi wa Maalim kuhamia ACT ni wa kwake yeye mwenyewe kwa kuwa ana maamuzi yake na mie ninayo yangu,” alisema Bwege ambaye ni mmoja wa wabunge machachari na wachangiaji bungeni. Mbunge mwingine aliyejitokeza ni Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali ambaye juzi alika osi kuu za CUF Tanzania Bara, Buguruni jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa anataka kuendeleza mapambano ya kupigania haki yanayoendeshwa na CUF na kuwa anaendelea na Lipumba kufanya kazi hiyo.

Bobali alisema amerudi nyumbani na kwamba wapo wengi watakaorudi kuungana na Profesa Lipumba na kuwa sasa ni wakati wa kukijenga chama na waliondoka kwenda sehemu nyingine ni utashi wao. “Nimerudi nyumbani baada ya msuguano uliodumu kwa miaka mitatu ndani ya CUF na uliokidhoosha chama, nawaomba mnisamehe kwa yaliyotokea,” alisema.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya alibainisha kuwa chama hicho kinawakaribisha wanachama na wabunge waliokuwa upande wa Maalim Seif na kuwataka kujitangaza kuwa wanaungana na CUF Lipumba. Alibainisha kuwa wabunge wote wa CUF kwa sasa wapo chini ya Lipumba na wanatakiwa kwenda kwenye osi za chama na kuelezea nia yao ya kufanya kazi na mwenyekiti huyo huku akitahadharisha kuwa watakaokiuka na kuanza kuzungumzia chama vibaya pembeni watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

“Kwanza sisi kama uongozi tulikuwa tunataka kuwaita wote kuka makao makuu ya chama mara moja kuwahoji nia yao ya kuendelea kufanya kazi nasi au hapana, lakini kwa kile tunachoona kimeanza kujitokeza ni kizuri kwa kuwa wapo ambao wameanza kutupigia simu kuomba kurejea,” alisema Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kaliua mkoani Tabora kupitia CUF. Katibu Mkuu wa CUF, Khalifa Suleiman Khalifa alithibitisha uwezekano wa wabunge waliotangaza kumuunga mkono Maalim Seif kuitwa kwenye makao makuu ya Buguruni kusikilizwa msimamo wao.

Wabunge hao 22 wanatokea visiwani Zanzibar huku Bara walikuwa wanne ambao hadi sasa wapo walikwisha weka wazi utayari wao wa kufanya kazi na Profesa Lipumba huku wengine ndio wanangojewa. “Idadi yao ndio hiyo na wanangojewa msimamo wao kwa kuwa tumeshasema kuwa sie uongozi wa CUF wa sasa tupo tayari kupigania maendeleo na wao kwa kuwa ni wabunge chini yetu basi kwa sasa warejee tujenge chama na kukabiliana na tofauti zetu,” alisema Khalifa.

John Gagarini kutoka Kibaha, anaripoti kuwa Chama cha ACT - Wazalendo Mkoa wa Pwani kimefurahishwa na kujiunga kwa Maalim Seif, na kusema kwao huo ni mtaji mkubwa hasa katika kipindi cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa Vijiji na Vitongoji kwa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa mwakani. Akizungumza na waandishi wa habari osini kwake mjini Kibaha, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa, Mrisho Swagala amesema Maalim Seif kujiunga na chama chao kwao ni kama kupata dhahabu ambayo ilikuwa inachezewa na wengine na amejiunga wakati mwafaka kuelekea uchaguzi.

Swagala amesema Seif ni kiongozi mwenye ushawishi mkubwa nchini hivyo anaamini wao wamepata dhahabu na ndiyo mwanzo wao kuwa chama kikubwa cha upinzani nchini tofauti na kilivyokuwa zamani na kuamini kuwa watafanya vizuri kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwakani. “Tunaamini tumepata mtu ambaye anakwenda kukinyanyua chama chetu kwani tumeona kule Zanzibar alivyoweza kuwa na wabunge wengi na kukaribia kushinda nafasi ya Urais licha kushindwa kwa kura chache kila alipokuwa akiwania nafasi hiyo hivyo kupitia ACT atafanya vizuri zaidi,” amesema Swagala.

Amesema hata kwa Bara, Maalim Seif anakubalika kwani hata baadhi ya wafuasi wa CUF mkoani Pwani wameonekana nao kujiunga na ACT ili kumuunga mkono kiongozi huyo wa upinzani baada ya kujiengua kwenye chama hicho baada ya kutoelewana na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba
Mafao muhimu sana na bado Mwaka mmoja tu
 
Ni sahihi hata ingekuwa Mimi, bunge likivunjwa wanenda AcT , tunza hii comment yangu mpaka mwakani

Sent using Jamii Forums mobile app
Wabunge kutoka Zenji, wanaweza kuuachia Ubunge kwa kujiunga na ACT sasa. Wa Bara, hawana jeuri hiyo. Watasubiri mpaka Bunge livunjwe, ili wavune mamilioni ya kiinua mgongo chao.
Lakini ile sheria (ikipita) ya mwanachama mpya hagombei mpaka muda fulani upite, itawabana. Hivyo hawatakuwa na sifa ya kugomhea. Wamalizie malizie tu huu uhondo uliobaki!
Ukweli wa mtu upo moyoni kwake ngoja wakistaafu ubunge ndo utaona rangi zote 120+

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama wataaminiwa sana na Lipumba
 
ACT from ZERO to HERO
ZITTO hapo kwanza kavuta fungu heavy pili chama kimepata jina
Kweli kwa mungu sio kwa mzungu[emoji1321]‍♂️
Bwege na wenzio malizieni muda kisha mvute mafao yenu(mamilioni kadhaa)siku bunge linavunjwa na baada ya hapo tunawasubiria ACT
Popote Alipo Sisi Tupo[emoji1321]‍♂️
 
View attachment 1050788

MBUNGE wa Kilwa Kusini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Suleiman Bungara maarufu Bwege amekuwa mbunge wa pili kutangaza rasmi kuingia kambi ya Profesa Ibrahim Lipumba ambayo sasa ndio inaongoza CUF. Bwege alikuwa mmoja wa wabunge waliokuwa wakiunga mkono iliyokuwa kambi ya CUF - Maalim iliyokuwa ikiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye amehamia ACT- Wazalendo.

Maalim Seif na mwasisi mwenzake wa CUF, Profesa Lipumba waliingia kwenye mgongano wa kimaslahi uliokia hatua ya kuwagawa wabunge wa chama hicho. Mgawanyo uliozalisha CUF ya Maalim Seif na ile ya Lipumba. Huku mvutano huo ukiendelea Osi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ilimtambua Profesa Lipumba kuwa ndio kiongozi wa chama hicho hali iliyosababisha Maalim kufungua kesi Mahakama Kuu kutaka kutengua utambuzi wa Osi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa CUF ya Lipumba, kesi ambayo Maalim alishindwa.

Huku Maalim Seif akishindwa kesi hiyo, Profesa Lipumba ameidhinishwa na Mkutano Mkuu wa CUF uliotishwa na Baraza Kuu la CUF kuwa Mwenyekiti wa chama hicho ambapo ameingia madarakani na uongozi wake na kwa sasa hatma ya wabunge hao waliokuwa upande wa Maalim Seif inadondokea mikononi mwake.

Mbunge Bwege ameamua kuweka wazi utayari wake wa kufanya kazi na Lipumba, akiliambia gazeti hili kuwa hana sababu ya kusita kufanya hivyo kwani yeye ni mtumishi wa wananchi wa Kilwa waliomchagua kupitia CUF na kwa kuwa CUF iliyobakia ya Lipumba, analo jukumu na kuendeleza mapambano ya kupigania haki chini yake.

“Ninachoweza kusema ni kuwa uamuzi wa Maalim kuhamia ACT ni wa kwake yeye mwenyewe kwa kuwa ana maamuzi yake na mie ninayo yangu,” alisema Bwege ambaye ni mmoja wa wabunge machachari na wachangiaji bungeni. Mbunge mwingine aliyejitokeza ni Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali ambaye juzi alika osi kuu za CUF Tanzania Bara, Buguruni jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa anataka kuendeleza mapambano ya kupigania haki yanayoendeshwa na CUF na kuwa anaendelea na Lipumba kufanya kazi hiyo.

Bobali alisema amerudi nyumbani na kwamba wapo wengi watakaorudi kuungana na Profesa Lipumba na kuwa sasa ni wakati wa kukijenga chama na waliondoka kwenda sehemu nyingine ni utashi wao. “Nimerudi nyumbani baada ya msuguano uliodumu kwa miaka mitatu ndani ya CUF na uliokidhoosha chama, nawaomba mnisamehe kwa yaliyotokea,” alisema.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya alibainisha kuwa chama hicho kinawakaribisha wanachama na wabunge waliokuwa upande wa Maalim Seif na kuwataka kujitangaza kuwa wanaungana na CUF Lipumba. Alibainisha kuwa wabunge wote wa CUF kwa sasa wapo chini ya Lipumba na wanatakiwa kwenda kwenye osi za chama na kuelezea nia yao ya kufanya kazi na mwenyekiti huyo huku akitahadharisha kuwa watakaokiuka na kuanza kuzungumzia chama vibaya pembeni watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

“Kwanza sisi kama uongozi tulikuwa tunataka kuwaita wote kuka makao makuu ya chama mara moja kuwahoji nia yao ya kuendelea kufanya kazi nasi au hapana, lakini kwa kile tunachoona kimeanza kujitokeza ni kizuri kwa kuwa wapo ambao wameanza kutupigia simu kuomba kurejea,” alisema Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kaliua mkoani Tabora kupitia CUF. Katibu Mkuu wa CUF, Khalifa Suleiman Khalifa alithibitisha uwezekano wa wabunge waliotangaza kumuunga mkono Maalim Seif kuitwa kwenye makao makuu ya Buguruni kusikilizwa msimamo wao.

Wabunge hao 22 wanatokea visiwani Zanzibar huku Bara walikuwa wanne ambao hadi sasa wapo walikwisha weka wazi utayari wao wa kufanya kazi na Profesa Lipumba huku wengine ndio wanangojewa. “Idadi yao ndio hiyo na wanangojewa msimamo wao kwa kuwa tumeshasema kuwa sie uongozi wa CUF wa sasa tupo tayari kupigania maendeleo na wao kwa kuwa ni wabunge chini yetu basi kwa sasa warejee tujenge chama na kukabiliana na tofauti zetu,” alisema Khalifa.

John Gagarini kutoka Kibaha, anaripoti kuwa Chama cha ACT - Wazalendo Mkoa wa Pwani kimefurahishwa na kujiunga kwa Maalim Seif, na kusema kwao huo ni mtaji mkubwa hasa katika kipindi cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa Vijiji na Vitongoji kwa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa mwakani. Akizungumza na waandishi wa habari osini kwake mjini Kibaha, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa, Mrisho Swagala amesema Maalim Seif kujiunga na chama chao kwao ni kama kupata dhahabu ambayo ilikuwa inachezewa na wengine na amejiunga wakati mwafaka kuelekea uchaguzi.

Swagala amesema Seif ni kiongozi mwenye ushawishi mkubwa nchini hivyo anaamini wao wamepata dhahabu na ndiyo mwanzo wao kuwa chama kikubwa cha upinzani nchini tofauti na kilivyokuwa zamani na kuamini kuwa watafanya vizuri kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwakani. “Tunaamini tumepata mtu ambaye anakwenda kukinyanyua chama chetu kwani tumeona kule Zanzibar alivyoweza kuwa na wabunge wengi na kukaribia kushinda nafasi ya Urais licha kushindwa kwa kura chache kila alipokuwa akiwania nafasi hiyo hivyo kupitia ACT atafanya vizuri zaidi,” amesema Swagala.

Amesema hata kwa Bara, Maalim Seif anakubalika kwani hata baadhi ya wafuasi wa CUF mkoani Pwani wameonekana nao kujiunga na ACT ili kumuunga mkono kiongozi huyo wa upinzani baada ya kujiengua kwenye chama hicho baada ya kutoelewana na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba

Wa bara wanafiki na njaa nyingi ngoja waone mziki wa huko pemba, hata hivyo bwege ni bwege tu 2020 atarudi ccm
 
Back
Top Bottom