Lipumba 'aisigina' CHADEMA bungeni

Lipumba 'aisigina' CHADEMA bungeni

Tangu lini? Sultan akawa mshaur wa makamanda.
 
Profesa gani ? Kwa maneno anayoongea hapo sidhani kama profesa au ndio kuchumia tumbo? K ama hana kazi mwambie aje nimpe kazi ya kufagia workshop yangu ,i will pay him better i promise

Unadhihirisha umbumbu wako kama haumjui waulize wamarekani na waingereza, uganda, kenya ni nani pr Lipumba.
 
Cuf kimebaki kufanya press conference dsm na mtwara.kwishney chezea ndoa ya mkeka.
 
Namheshimu sana Prof. Lakini naona kajichanganya mno katika hoja hii. Anaposema wapinzani wanashindwa kujenga hoja halafu wakati huo huo anasema mawaziri wanatoa majibu mepesi, hapo anamaanisha nini?Majibu mepesi kwa maswali gani? Waliyojiuliza mawaziri wenyewe au kutoka upinzani. Kama ni kutoka upinzani amewezaje kujua kwamba jibu ni jepesi iwapo swali halikuwa na hoja ya msingi kwa wa-Tz kama alivyodai yeye mwenyewe?Binafsi nimeona Mh. Lipumba ameshindwa kujieleza.
Prof. anahitaji ku recharge!. Labda akachimbue kitabu tena. Hivi hakuna refresher programs za watu kama hawa? Maana sasa taalumu kapoteza, siasa kapoteza na chama kaua! Prof tafadhali!
 
Uyu mzee badala ya kukaa mezani kutushauri jinsi ya kupamba ili tujimarishe kiuchumi yeye anapoteza mda majuKwaani tena kwa ngonjera na maneno ya khanga...ni aibu kwa mchumi kama huyu...ayo Mambo yana mtu kana nape....au wale wa ganga njaa wa Lumumba
 
Unadhihirisha umbumbu wako kama haumjui waulize wamarekani na waingereza, uganda, kenya ni nani pr Lipumba.
Ya kale baba, enzi hizo!!!!!!!!! Historia,.tukaweke makumbusho.. Usisahau kwamba duniani hakuna permanency wala constancy!. Kila kitu na watu hubaddilika. Ukifahamu hii, hutadharau unachokiona leo kwa kuwa unaamini ulichosikia miaka 20 iliyopita. Ingekuwa hivyo, bado angekuwa nao. Hakuna mtu anayependa kupoteza kizuri.
 
Kweli huyu ni "le profeseri" mwali huyo, ndoa tamu jamani, Kumbe huyu yupo? Mnyamwezi asiyekubalika kwao, Aliingia kichwa kichwa uchaguzi wa Igunga akapigwa za uso, CCM ilipata kura 26000, CDM kura 23000 na CUF 4000. LE PROFESERI.
 
Unadhihirisha umbumbu wako kama haumjui waulize wamarekani na waingereza, uganda, kenya ni nani pr Lipumba.

Kwahiyo huo uprofesa wake unafanya kazi marekani ,uingereza ,uganda sijui kenya, ila akiwa nyumbani anakuwa kichwa BOGA .listen my broda kwa upumbavu alioongea hapo juu he is not deserving to be even my garden boy
 
Huwa anazungumzia bunge lipi? Maana kwa hili nilijualo mimi nimeshuhudia Mnyika akiongelea hoja za wananchi kuhusu maji, nimemsikia Wenje akizungumzia suala la matatizo ya ardhi Mwanza na nimemsikia Zitto Kabwe akizungumzia masuala ya uchumi na kupinga ufisadi au hayo ni masuala ya chama?
 
Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema vurugu zinazoendelea bungeni zinasababishwa na Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kushindwa kujenga hoja na mbinu za kuwabana wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema wabunge wa Chadema wana tabia ya kufuata mfumo wa kwenda bungeni na hoja zinazobeba chama chao na si za Watanzania wote kama jinsi CCM wanavyofanya.

"Kambi rasmi ya upinzani imepoteza uwezo wa kujenga hoja za mashiko na mbinu madhubuti za kuwabana wabunge wa CCM bungeni na badala yake Chadema, wamekuwa na tabia mbaya ya kubeba chama chao," alisema Profesa Lipumba.

Alisema kambi rasmi ya upinzani pia imeshindwa kulinda utaratibu mzuri wa kutetea masilahi ya umma bila jazba na hoja zenye mashiko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ilipokuwa ikiongozwa na CUF, Kiongozi huyo alisema kambi ya upinzani inapaswa ijipange upya kwa utaratibu na mikakati mizuri ya kuteta hoja za wananchi bila kuyumbishwa na wabunge wa CCM.

"Bunge usiwe uwanja wa kuonyesha mbwembwe za chama bali uwe uwanja wa kutetea haki za wananchi, wabunge wanapaswa wabadilishe mitazamo ya kuona bungeni ni sehemu ya kujionyesha kisiasa na chama chako kinafanya nini nje ya Bunge," alisema Lipumba.

Alisema viongozi wa Serikali wanapaswa kubadilika kuhusu namna ya kutoa majibu bungeni.

Profesa Lipumba alisema mawaziri wengi wanakuwa wakitoa majibu mepesi katika maswali ya msingi yanayoulizwa na wabunge wa upinzani.

Alisema Bunge linatumia muda na pesa za walipakodi vibaya kwa baadhi ya wabunge kuwa na ubishi usiokuwa na tija, kutoleana matusi na wengine kuingilia hoja za wenzao bila sababu za msingi.

Profesa Lipumba pia alisema Spika wa Bunge, Anne Makinda amepoteza uwezo wa kuliongoza Bunge.


Source: Gazeti la mwananchi

Hebu ninukuu na mimi basi jamani.... Msiwe wachoyo wa nukuu. Profesa Lipumba kaona Chadema wametingwa bungeni, kama kukabwa roba fulani hivi, CCM wanakaribia kupoteza focus ya agenda ya ufisadi kabisa bungeni,
Lipumba anaona enheee....hapo hapo! Chadema wamepoteza nini vile?

Chadema wamepoteza focus ya issue muhimu bungeni: Issue ya Utawala Bora imekufa. Na hilo alijafika hapo kama ajali. Ni mpango mkakati ku ondoa hiyo focus bungeni. Kambi Rasmi ya Upinzani ya CUF ilikuwa ya Samuel Sita. He was sober. Leo CCM wameweka Mganga wa Mifugo kuendesha bunge makusudi. Wewe mganga wa mifugo na bunge wapi na wapi!

Hata angekuwa CUF mule bungeni leo, bado huyo mganga wa mifugo angekuchanganyeni tu! Cheza na CCM wewe....
 
Tunashauri Profess ang'atuke siasa kama sasa anaonyesha mapenzi yake kwa mume bila aibu kwa nini asilinganishe chadema na cuf hizo ndio zao Mnyaa naye alipewa lisaa pale TBC kuzodoa Chadema
 
Hoja zinaletwa kihuni,kila mbunge anamatatizo yake jimboni kwake.nafikiri ugeni wa bungeni,na wote waliofukuzwa ni mara yao ya kwanza kuingia bungeni.

Hapo kwenye RED unamaanisha nini? hili ni Bunge la ngapi tangu wachaguliwe kuwa wabunge? na pia sijui unamaanisha nini unaposema Hoja zinaletwa kihuni, ndugu kabla ya kuandika fanya Editing kwanza kichani ndo uiname kwenye Keyboard na kuandika.
 
Ni mnafiki huyu hana jipya. Angejiuliza inakuwaje CDM wasiotetea maslahi ya Watanzania bungeni badala yake kuonyesha mbwembwe ndani ya Bunge wanakuwa na umaarufu mkubwa katika sehemmu nyingi nchini ukilinganisha na chama chake ambacho hakionyeshi mbwembwe!? Maprofesa wengine!!! Sijui hata huo uprofessa waliupata vipi kwa jinsi wanavyoonyesha unafiki wa hali ya juu kwa mambo yaliyo wazi kabisa.

QUOTE=Mpola Mpola;6221617]Lipumba katika observations zao hajaona kabisa ya Mwigulu na Lusinde?[/QUOTE]
 
Lipumba anazeeka vibaya wakuu na ukiongeza na swala la ndoa basi akili yote inakuwa ipo kimlugo mlugo tu.
 
Asante profesor kwa kuliona hilo, hapa juzi kati niliweka uzi unaonyesha jinsi "wabunge wachadema wanavyokera sana" bungeni hawa mambumbu na waendeshwa na hisia wakaleta vioja kama walivyowabunge wao na kukosa hoja za kuwatetea wabunge wao matokeo yake wanaanza mbona mbona n wewe usubiri waje utakiona cha mtema miwa.

Lipumba ameolewa na CCM mwambie atulie kwenye ndoa mbona anatufatafata kama vile huwa tunampiga chabo wakati wanakunjwa na CCM
 
Hoja zinaletwa kihuni,kila mbunge anamatatizo yake jimboni kwake.nafikiri ugeni wa bungeni,na wote waliofukuzwa ni mara yao ya kwanza kuingia bungeni.

unaleta ujinga wa business as usual, hii generation sio ya kuburuza na bunge haliendeshwi kwa mazoea
 
Vimulimuli alivyopewa Seif Sharif na ahadi alizopewa Lipumba nanwatawala vimeathiri uwezo Wa kufikiri Wa professor
 
Mzee Lipumba amechoka akili sasa anamwaga Pumba.

Lakini ndo mambo ya ndoa hayo.
Ukiolewa na jambazi ni lazima ujifunze kutunza siri za mueo jambazi.

Tangu CUF wawekwe unumba na CCM, wanamipasho hao!! Utadhani machangu fulani.
 
Back
Top Bottom