Lipumba 'aisigina' CHADEMA bungeni

Lipumba 'aisigina' CHADEMA bungeni

Bunge linaendeshwa kwa sheria, haliendeshwi kwa uwingi wa mvi au uwingi wa siku za kumbonji bungeni.
Wananchi tumezoea kusikiliza bunge la kufunika mambo bila kuchambua undani.
Kwa kukosa dira na uadirifu wa kisheria Kiti cha Spika kinayumba kama mlevi wa gongo na mnazi.


Hoja zinaletwa kihuni,kila mbunge anamatatizo yake jimboni kwake.nafikiri ugeni wa bungeni,na wote waliofukuzwa ni mara yao ya kwanza kuingia bungeni.
 
Lipumba anazeeka vibaya wakuu na ukiongeza na swala la ndoa basi akili yote inakuwa ipo kimlugo mlugo tu.

Kijana una matani na viongozi wako wa juu wa Chadema ambao wamegoma kuoa?
 
Lipumba amepumbazwa na limbwata la CCM mpaka amepagawa na sasa anamwaga pumba. Hivi naye bado ni professa huyu?
 
Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema vurugu zinazoendelea bungeni zinasababishwa na Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kushindwa kujenga hoja na mbinu za kuwabana wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema wabunge wa Chadema wana tabia ya kufuata mfumo wa kwenda bungeni na hoja zinazobeba chama chao na si za Watanzania wote kama jinsi CCM wanavyofanya.

“Kambi rasmi ya upinzani imepoteza uwezo wa kujenga hoja za mashiko na mbinu madhubuti za kuwabana wabunge wa CCM bungeni na badala yake Chadema, wamekuwa na tabia mbaya ya kubeba chama chao,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema kambi rasmi ya upinzani pia imeshindwa kulinda utaratibu mzuri wa kutetea masilahi ya umma bila jazba na hoja zenye mashiko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ilipokuwa ikiongozwa na CUF, Kiongozi huyo alisema kambi ya upinzani inapaswa ijipange upya kwa utaratibu na mikakati mizuri ya kuteta hoja za wananchi bila kuyumbishwa na wabunge wa CCM.

“Bunge usiwe uwanja wa kuonyesha mbwembwe za chama bali uwe uwanja wa kutetea haki za wananchi, wabunge wanapaswa wabadilishe mitazamo ya kuona bungeni ni sehemu ya kujionyesha kisiasa na chama chako kinafanya nini nje ya Bunge,” alisema Lipumba.

Alisema viongozi wa Serikali wanapaswa kubadilika kuhusu namna ya kutoa majibu bungeni.

Profesa Lipumba alisema mawaziri wengi wanakuwa wakitoa majibu mepesi katika maswali ya msingi yanayoulizwa na wabunge wa upinzani.

Alisema Bunge linatumia muda na pesa za walipakodi vibaya kwa baadhi ya wabunge kuwa na ubishi usiokuwa na tija, kutoleana matusi na wengine kuingilia hoja za wenzao bila sababu za msingi.

Profesa Lipumba pia alisema Spika wa Bunge, Anne Makinda amepoteza uwezo wa kuliongoza Bunge.



Source: Gazeti la mwananchi

kweli namna hii halafu wazungu wakituita waafrika manyani tutakasirika? kama kweli mtu aliyesoma kwa kiwango cha uprof anatema pumba kwa kiwango hiki, tena publicly, tutegemee nini kwa mwafrika asiyesoma au hata graduate wa first degree tu? kweli waafrika wengi tumelaaaniwa! prof li.pumba ulaaniwe kwa unafki na uzandiki huu. unatumia elimu yako kuiangamiza jamii badala ya kuiponya. Mungu atakulipa kwa kadri ya uzindaki wako.
halafu wazu
 
Asante profesor kwa kuliona hilo, hapa juzi kati niliweka uzi unaonyesha jinsi "wabunge wachadema wanavyokera sana" bungeni hawa mambumbu na waendeshwa na hisia wakaleta vioja kama walivyowabunge wao na kukosa hoja za kuwatetea wabunge wao matokeo yake wanaanza mbona mbona n wewe usubiri waje utakiona cha mtema miwa.

Samahani kama nitasema kwamba wewe na Prof. Lipumba mna akili sawa! Kama umesoma hiyo habari vizuri utaona Lipumba anaji-contradict katika statement zake! Anasema Mbowe ndiye chanzo cha vurugu, wabunge wa Chadema wanapeleka hoja zenye maslahi ya Chadema na hapohapo anajisahau kama kuku na kupeleka lawama kwa mawaziri eti wanatoa majibu mepesi. Kwa uchambuzi utaona chanzo cha vurugu ni wabunge wa CCM na mawaziri wanaotoa majibu mepesi. Chadema wao wanaibana Serikali isitoe majibu mepesi au kupuuza hoja za msingi zenye maslahi kwa Taifa!
Halafu kwa hesabu ndogo ya 1+1 ni kwamba hakuna mgomvi bila kuwepo mgomvi wa kugombana nae. Kama Chadema ni wagomvi wanagombana na nani, maana haiingii akilini mtu kugombana bila kuwepo mtu wa kugombana naye ambaye na yeye naye ame-react back! Let us be honest...tusiwe bias! kama ni onyo basi litolewe kwa wabunge wote bila kujali chama!
 
Tangia CUF ijiunge na CCM, Lipumba amekuwa akianza kutoa pumba naye.
Hoja ya Mnyika ya maji darisalamu ilikuwa inataka kuleta maji kwa wanachama wa CHADEMA tu???
Hoja ya Nassari ya Elimu je, ilikuwa elimu kwa wana CHADEMA tu???

Kwakweli chadema mnakera.Mmetanguliza sana uchama naudini."AN idear of Economist or politian is more powerfull than commonly understood"By Keynasian.Prof uwezowako uko juu waerevu wamekuelewa wapumbavu utakeshanao.
 
swala la uprofesa sio hoja kwan kuna maprofesa wengine wameshindwa uchaguzi kwa takriban awamu 3-livingstone lusinde.
 
prof rudi kafundishe huku kumekushinda utajiaibisha kama hela unazo chunga heshma yako mzee wangu
 
Tangia CUF ijiunge na CCM, Lipumba amekuwa akianza kutoa pumba naye.
Hoja ya Mnyika ya maji darisalamu ilikuwa inataka kuleta maji kwa wanachama wa CHADEMA tu???
Hoja ya Nassari ya Elimu je, ilikuwa elimu kwa wana CHADEMA tu???


CHADEMA mnakera sana,mmezidisha uchama naudini hasa baada ya waraka wamakanisa wa mwaka 2010."An idear of Economists and politicians,whether they are right or wrong,are more powerful than commonly undestood"Prof kiwangochako kipo juu sana,waerevu tumekuelewa,wapumbavu utakeshanao.
 
Hoja zinaletwa kihuni,kila mbunge anamatatizo yake jimboni kwake.nafikiri ugeni wa bungeni,na wote waliofukuzwa ni mara yao ya kwanza kuingia bungeni.

Waliokaa bungeni muda mrefu kama kina Cpt Komba wamefanya nini?
 
Mbwembwe za chama.....ni zipi hizo....Suala la Katiba Mpya....Mbona hili ni la kitaifa. OK kumbe CUF WALIVYO JIFUNGIA CHUMBANI KULE ZANZIBAR kutengeneza makubaliano na CCM ...waliwakilisha maslahi ya vyama vyote vya upinzani na wananchi hasa waliouawa ule mwezi January . Hapo Profesa ameteleza kidogo.Nina wasiwasi wamemnukuu vibaya.

Katika Chama kilichojitahidi kusimama na kuzungumza hoja za wananchi ni CHADEMA na ndiyo maana kila mwananchi yuko tayari kusafiri umbali wowote kwa gharama zake kwenda kusikiliza tu kile wanachoongea...kwani kinagusa maslahi yake na maisha yake ya Kila siku...Nakumpa tumaini jipya la kufanya uchaguzi sahihi 2015
 
swala la uprofesa sio hoja kwan kuna maprofesa wengine wameshindwa uchaguzi kwa takriban awamu 3-livingstone lusinde..cuf kama akili ndo hizi?kwa nin msipate wabunge wawili tanzania bara..
 
jukuwaa la siasa limetekwa na chademalism idealogy. mtake msitake ukweli ndio huo.
 
Back
Top Bottom