Mh. Lipumba unaheshimika hebu chambuzi zako jitahidi zisiwe na dosari au mwandishi kaongeza ya kwake? Maana utakuja ulizwa hivi Nawewe ni Professor?
Kwenye bold hapo, moja ya hoja za Mbowe katika hotuba ya kuchangia bajeti ya ofisi ya waziri mkuu ilihusu suala la Lwakatare. Is this not a party issue?
Hii haikuwa issue ya kitaifa bali ilijikita zaidi kwenye maslahi ya chama.
Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema vurugu zinazoendelea bungeni zinasababishwa na Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kushindwa kujenga hoja na mbinu za kuwabana wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema wabunge wa Chadema wana tabia ya kufuata mfumo wa kwenda bungeni na hoja zinazobeba chama chao na si za Watanzania wote kama jinsi CCM wanavyofanya.
Kambi rasmi ya upinzani imepoteza uwezo wa kujenga hoja za mashiko na mbinu madhubuti za kuwabana wabunge wa CCM bungeni na badala yake Chadema, wamekuwa na tabia mbaya ya kubeba chama chao, alisema Profesa Lipumba.
Alisema kambi rasmi ya upinzani pia imeshindwa kulinda utaratibu mzuri wa kutetea masilahi ya umma bila jazba na hoja zenye mashiko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ilipokuwa ikiongozwa na CUF, Kiongozi huyo alisema kambi ya upinzani inapaswa ijipange upya kwa utaratibu na mikakati mizuri ya kuteta hoja za wananchi bila kuyumbishwa na wabunge wa CCM.
Bunge usiwe uwanja wa kuonyesha mbwembwe za chama bali uwe uwanja wa kutetea haki za wananchi, wabunge wanapaswa wabadilishe mitazamo ya kuona bungeni ni sehemu ya kujionyesha kisiasa na chama chako kinafanya nini nje ya Bunge, alisema Lipumba.
Alisema viongozi wa Serikali wanapaswa kubadilika kuhusu namna ya kutoa majibu bungeni.
Profesa Lipumba alisema mawaziri wengi wanakuwa wakitoa majibu mepesi katika maswali ya msingi yanayoulizwa na wabunge wa upinzani.
Alisema Bunge linatumia muda na pesa za walipakodi vibaya kwa baadhi ya wabunge kuwa na ubishi usiokuwa na tija, kutoleana matusi na wengine kuingilia hoja za wenzao bila sababu za msingi.
Profesa Lipumba pia alisema Spika wa Bunge, Anne Makinda amepoteza uwezo wa kuliongoza Bunge.
Source: Gazeti la mwananchi
Tangia CUF ijiunge na CCM, Lipumba amekuwa akianza kutoa pumba naye.
Hoja ya Mnyika ya maji darisalamu ilikuwa inataka kuleta maji kwa wanachama wa CHADEMA tu???
Hoja ya Nassari ya Elimu je, ilikuwa elimu kwa wana CHADEMA tu???
Profesa Lipumba ana haki ya kusema lile analoamini hata kama litapata watu wawili kwa kila watu kumi kwa lile alilolisema. Profesa Lipumba 1995 aligombea urais akashindwa; 2000 akagombea tena akashindwa; 2005 akagombea tena akashindwa; 2010 akagombea tena akashindwa. Ninaomba yeyote mwenye kujua siri ya kushindwa kwake kwa mara zote anapogombea urais.......
Sababu za kushindwa na CCM waulize Slaa na Mbowe maana wote wamepigwa chini na CCM kwa nyakati tofauti, tofauti yao Slaa alikuwa makini sana mpaka akafanikiwa kuliona kontena la kura feki kule mbeya pamoja na kupewa taarifa za siri na watu wake walokuwa kwenye system juu ya mpango wa kuiba kura zake lakini hawakumpa mbinu ya kuzuia wizi huo!
Kwa nini kila mara vulugu zinapotokea Mkuu wa kambi ya upinzani, Mh. Mbowe huwa hayupo bungeni? Kuna kuwa kama njama fulani zinakuwa zimepangwa ili labda ionekane Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzania hahusiki kwa nia mbadala ku-protect image fulani ya chama. Kama angekuwepo wakati vulugu zinafanyika lazima watu wangetaka kuona anafanya nini kuhusiana na wabunge wake wanaopiga kelele za hovyo bungeni. There's something fishy in CHADEMA!! Is this happen by coincidence?.
Wapi nimekwambia INANIUMA. Kwani wewe kinakuwasha nini kwa maandiko yangu kama yana maana hiyo au hayana.wewe inakuuma nini?kama yupo kama hayupo wewe inakunyima kula?bogus!
Hawa maprofesa njaa hawa Cuf wapiganie ndoa yao waachane na ChademaChama Cha Wananchi (CUF), kimesema vurugu zinazoendelea bungeni zinasababishwa na Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kushindwa kujenga hoja na mbinu za kuwabana wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema wabunge wa Chadema wana tabia ya kufuata mfumo wa kwenda bungeni na hoja zinazobeba chama chao na si za Watanzania wote kama jinsi CCM wanavyofanya.
Kambi rasmi ya upinzani imepoteza uwezo wa kujenga hoja za mashiko na mbinu madhubuti za kuwabana wabunge wa CCM bungeni na badala yake Chadema, wamekuwa na tabia mbaya ya kubeba chama chao, alisema Profesa Lipumba.
Alisema kambi rasmi ya upinzani pia imeshindwa kulinda utaratibu mzuri wa kutetea masilahi ya umma bila jazba na hoja zenye mashiko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ilipokuwa ikiongozwa na CUF, Kiongozi huyo alisema kambi ya upinzani inapaswa ijipange upya kwa utaratibu na mikakati mizuri ya kuteta hoja za wananchi bila kuyumbishwa na wabunge wa CCM.
Bunge usiwe uwanja wa kuonyesha mbwembwe za chama bali uwe uwanja wa kutetea haki za wananchi, wabunge wanapaswa wabadilishe mitazamo ya kuona bungeni ni sehemu ya kujionyesha kisiasa na chama chako kinafanya nini nje ya Bunge, alisema Lipumba.
Alisema viongozi wa Serikali wanapaswa kubadilika kuhusu namna ya kutoa majibu bungeni.
Profesa Lipumba alisema mawaziri wengi wanakuwa wakitoa majibu mepesi katika maswali ya msingi yanayoulizwa na wabunge wa upinzani.
Alisema Bunge linatumia muda na pesa za walipakodi vibaya kwa baadhi ya wabunge kuwa na ubishi usiokuwa na tija, kutoleana matusi na wengine kuingilia hoja za wenzao bila sababu za msingi.
Profesa Lipumba pia alisema Spika wa Bunge, Anne Makinda amepoteza uwezo wa kuliongoza Bunge.
Source: Gazeti la mwananchi
sitoshangaa kama unaweza kumuuliza mama aliyekuzaa hv na wewe ni mama? sa utashindwa kumuliza lipumba kama naye ni prof...nyie tena wasomi nguli wa nchi hii mnawezekana, sentensi zenu tatu za kingereza ushajiona newton