Lipumba afafanua maana ya kuwaita CCM ''Intarahamwe"

Lipumba afafanua maana ya kuwaita CCM ''Intarahamwe"

Akiongea na Wazanzibari walio wengi katika viwanja vya Pemba jana May day Lipumba alisema"

"Sisi tumewaita CCM intarahamwe kutokana na lugha zao za kibaguzi dhidi ya makundi mbali mbali ambyo ndio iliyokuwa inatumiwa na jamaa hawa wa Intarahamwe ambayo baadae ikasababisha mauwaji makubwa.

"Ndugu zanguni maana ya Intarahamwe ni wanyaruwanda au warundi ambao wakifanya kazi pamoja ndio tafsiri yake. Sasa pana pana kundi la CCM limeamua kufanya kazi pamoja ili kuzuwia mawazo na maoni ya wananchi na kuanza kuleta lugha za kibaguzi kwa wananchi na katika jamii za kitanzania"

Akaendelea kusema "CCM walipokuwa wanachangia bungeni walikuwa wanatoa lugha za matusi na kibaguzi na wengine walikuwa wanafurahi kupiga makofi na kugonga meza bungeni kushadidia ubaguzi huo na matusi hayo. Ambapo alisema lazima atokee mtu awaeleze lugha za matusi na kibaguzi hazikubaliki.

"Hatutaki yaje yatokee mauaji na vurugu zilizosababishwa na Intarahamwe wa Rwanda. Hatuhitaji na Intarahamwe ya CCM kuja kusababisha vurugu na mauwaji hapa Tanzania."

Kwenu wadau,;

Huyu Lipumbaf amepoteza sifa na hadhi ya kuitwa Profesa.
 
'Interahamwe'....ili ni kundi kubwa la wahutu wa kinyarwanda lililoongoza mauaji ya kimbali nchini Rwanda mwaka 1994. Ni kundi lililo nia mamoja (kubaka, kufanya mauaji ya kinyama) dhidi ya watutsi. Kwa mauaji hayo yalivyokuwa, nidhairi wahusika hawakuwa na chembe yoyote ya ubinadamu. Walijawa chuki iliyokithiri mipaka.

Kwa hali ilivyoonekana katika mijadara ya bunge la katiba mpya, ni dhairi, wachangiaji wengi kutoka kundi la 'waliowengi' dhidi ya 'wachache' lilionesha chuki iliyokithiri na uchochezi ambao haujawai tokea Tanzania. Walistahili kuitwa 'Interahamwe'. Hata hivyo chembe chembe za unterahamwe ktk kundi ilo la 'waliowengi' zilionekana mapema. Ukichimbua michango yangu hapa JF neno hilo nimelitumia sana kuonesha nchi ilikokuwa inaelekea.

Kwa maana nyingine Interahamwe ni kundi kubwa ambalo linaweza endeshwa na watu wachache wenye madaraka na fedha kufanya maagamizi ya kimbali pasipo hata wao ku-reason kwa nini wafanye ivyo. Hatutegemei Tanzania yetu ifikie huko, japo dalili zinaonesha.
Mkuu ni kweli kuwa INTERAHAMWE wakati mwingine wanajulikana kama ABAKORAKAMO.
 
Lipumba mgombea urais wa kudumu CUF hii ni demokrasia??
 
Nachukia sana watu wasiopenda Amani. Hawa UKAWA wamejipanga kuvuruga Amani ya Nchi ila hawatafanikiwa kwa sababu watanzania ni wajanja, hawako tayari kuona wajinga wachache wakivuruga yale mazuri tuliyoachiwa na waasisi wetu.
 
Mkuu ni kweli kuwa INTERAHAMWE wakati mwingine wanajulikana kama ABAKORAKAMO.

Haaaaa..ni mecheka sana. Kuna jamaa mwenye ID kama hiyo hapa jf. Fuatilia uone hoja zake..zaki-interahamwe vile.
 
Hivi huyu mchumi bado anaishi Tz? Naona alipotea kabisa
 
Du kuna Intrahamwe wengi humu jf. Angalia wanavyotoa pofu kwenye post zao. Mmojawapo ni huyo aliyeingia na ID mpya akijiita Weston Songoro. Huyu atakuwa ni Intrahamwe Ritz bila shaka.

Tiba
 
kwa ufupi haya ndiyo maintarahamwe aliyoyakusudia Pro. Lipumba
Real Killers!

Interhamwe.jpg
 
Hata shetani alikuwa Malaika mwema wa Mungu, sembuse ccm kwa Tanzania!
kisha we ndie hasa interahamwe, hilo rungu katika avatar yako ndo hasa yalokuwa yakitumiwa na ndugu zako interahamwe kule Rwanda.
 
Nachukia sana watu wasiopenda Amani. Hawa UKAWA wamejipanga kuvuruga Amani ya Nchi ila hawatafanikiwa kwa sababu watanzania ni wajanja, hawako tayari kuona wajinga wachache wakivuruga yale mazuri tuliyoachiwa na waasisi wetu.


Hebu tuangalie kauli hizi za viongozi wa CCM:
- Muundo wa serikali tatu ukipita Wapemba wasipite Zanzibar,
- Muundo wa serikali tatu ukipita Wapemba wahame Zanzibar.
- Wapemba hawana undugu na wabara ,'
- Serikali tatu zikipita mtatuambia lini Pemba iliungana na Unguja.
- Zanzibar ni kisiwa cha watu weusi.
- Maoni ya serikali tatu yametolewa na watu wengi wa kigoma na Pemba.
- Serikali 3 zikipota Zanzibar itaongozwa kiislam hivyo wakristo msikubali ( wakati huo huo serikali mbili itatatua kero za Zanzibar kwa kuipa Zanzibar madaraka kamili na kujiunga na jumuia ya nchi za kiislam,OIC)
- Muundo wa Serikali tatu ukipita nitaingia msituni( Makofi ,pwaa,pwaa,pwaa,pwaa toka kwa wajumbe wa CCM) huku msemaji akiwa ni mwanajeshi aliyebadilisha majukumu ya kazi.
- Muundo wa Serikali tatu ukipita serikali itapindua nchi kwa kwa kukosa mishahara
- Serikali tatu zikipita wapemba watanyang'anywa mali zao zote na kufukuzwa.
- Serikali tatu zikipita wakristo hawataweza kwenda kanisani kusali kwani kikundi cha uamsho ni cha kigaidi hivyo kitaleta fujo.
Hizi kauli zilitolewa na wajumbe ambao ni viongozi wa Chama na serikali ya CCM. Na kwa sababu hazikukemewa basi kila mwana CCM anaona kwamba ni sifa kuhubir chuki na vitisho kwa watanzania wasio kubaliana na rasimu ya CCM
Amani ya nchi hii itaondolewa na CCM kwa sababu wote wanalinda maslahi yao kwa namna yoyote hata kwa kutoa roho za watu. Hii sio CCM sio ile ya Nyerere aliyoiacha.Hii ni CCM maslahi.
 


Kitendeo alichokifanya Prof Lipuma akilingani na heshima anayopewa na jamii achilia mbali kuwa wasomi wanamtegemea sana katika fani ya Uchumi na masuala mengine kwani ni mingoni mwa watu makini ambao maandiko na matamshi yake vyaweza tumiwa na wasomi kwenye tafiti za kitaaluma. Kama ni kweli ni yeye ametoa ufafanuzi kwa kile alichomaanisha kuwaita wajumbe wenzake ma Intarahamwe na kukimbia vikao vya Bunge bado hajakidhi vigezo vinavyoweza kumrudishia hadhi yake. Haiingii akilini Profesa tunayemuamini kulikimbia Bunge linaloweza kujadili mambo na kufikia maamuzi yanayokubalika kikatiba badala yake anajiunga na kundi lililosheheni ushabiki kwenda mitaani na kufanya mikutano inayohamasisha hisia nje ya Bunge la Katiba ambavo kwa vyovyote matokeo yake hayatumiki kwenye Bunge.

Ni ushauri tu kwamba Prof aombe tu samahani kwamba ilikuwa slip of tongue na awashauri wenzake warudi Bungeni tuendelee kupata michango na hoja makini kutoka kwa watu makini.

Kwani wewe ni nini usichokiona kuwa hakiko sahihi ktk kuwaita hao jamaa "interrahamwe?" Au ndio walewale mmeshatoka mjengoni na sasa mnaendesha u-intarrahamwe huku nje!!??

Tunamuheshimu sana Lipumba na wala hahitaji kununua hiyo heshima kutoka kwa hawa CCM a.k.a interrahamwe!!
 
Back
Top Bottom