Lipia kitanda cha chuma kwa awamu

Nashukuru kwa mrejesho. Bei ni negotible, inaweza shuka. Lakini mkumbuke unalipa kwa installments, kuna storage cost, ulinzi pia unaweza kufanyiwa home delivery. Karibuni.
Angalau useme hivyo ndugu yangu
 
350,000 bado ghali Nenda LAMU utapewa bure.

Hii tabia ya watu kujifanya 'critics' kwenye biashara za watu mnakera Argrr!
Issue siyo kujifanya critic, issue ni biashara, mimi nimeshakaa kwenye biashara, mfanyabiashara huwa ana tabia ya kujua counter part wake bei za bidhaa zipoje ili waende sawa, kitu kingine unachosahau wateja wengi wana ile kitu ya consumer behaviour, atataka ajue ni wapi kuna fair price, labda kama huna experience ya biashara, kitu kingine ni quality ya product unayotoa, ndiyo maana kuna vitanda mpaka vya milioni kadhaa.

zaidi ya hapo, mimi sijamlazimisha auze 350000, ni ushauri tu ingawa wabongo wengi ukiwashauri wanafikiri negative, embu muangalie huyu nimemtoa Zoom Tanzania nenda kaangalie huko uone
 
Kitanda cha laki 280000 au 250000 unauza laki 5. Kweli wabongo tumezoea wizi. Kawauzie wezi wenzako.
 
teh teh nimemkumbuka bibi yangu akinibadilisha nepi
Hahaha aisee wewe ni noma mpaka unakumbuka bibi alivyokuwa akikubadilisha nepi ulikuwa na miaka mingapi kipindi hicho bado ulikuwa ukilala na dad na mummy hahaaa [emoji85] [emoji87]
 
Harufu ya Utaperi zaidi...

Hii lugha wengine tunaichukulia vibaya... Yaani utoe laki mbili na nusu hupewi kitu hadi umalizie laki mbili na nusu zingine ndio unapewa kitanda... Huku Tangazo likisema lipia kwa awamu kwa lugha hiyo ni kana kwamba unapewa mzigo and then unakuwa unaulipia kidogo kidogo hadi deni liishe... waulize watu wa boda boda wanaoingia mkataba.. wanapewa chombo na wao wanapeleka hesabu hadi siku ikifikia kiasi cha gharama ya pikipiki na kifaida kidogo inakuwa mali ni yake kabisa..

Sasa wewe huna sababu n atangazo lako yaelekea huna mtaji hivyo unatumia njia ya kuhadaa watu...
 
Mwananyamala ehemu gani ?naomba iunielekeze in-box kama hautojari nahitaji
 
Laki tano na Godoro mkuu maaana kwa hiyo bei labda kutangaze mitaa ya post kwenye vigogo wa selikali
 
Kitanda cha chuma 5ft x 6ft kizuri, bei yake ina range kati ya Tshs: 250,000/= na 300,000/=. Tunatengeneza kwenye workshop yetu.
Pia waweza kuja na design yako tunatengeneza.
 
>>> Atakae Nunua hiki Atakuwa anamapungufu sio BURE ...............>>>
 
Naona ktk vitanda bora unavyotengeneza naona hili ndio umekiona bomba utuvitie eeeeenh!!
 
Halafu mkuu urembo wa mtindo huo mbona unaogopesha sio rafiki kwa watoto,mtoto anaweza bembea nao akifika chini hayo mavyuma yamemtoa utumbo
 
Makumbusho, Mwananyamala, Mkwajuni, Kigamboni kwa Urasa, na Kigamboni pale NSSF kote vitanda vya chuma vya saizi hiyo vinaanzia 250k na havizidi 350k. Na vizuri kuliko hiki cha kwenye picha.

Kwa hii bei mkuu naona kuna watu wako umewalenga.
 
Sijaona ubunifu wowote kwenye kitanda chako. Bei yenyewe inaonyesha ni kwa jinsi gani pesa ya Tanzania ilivokosa thamani. Kitanda Kinauzwa nusu milioni???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…