Lipi kati ya haya bado unafanya?

Lipi kati ya haya bado unafanya?

abunerimgaya

Member
Joined
Nov 13, 2012
Posts
78
Reaction score
15
SIJUI KAMA SIKU HIZI IPO HII!
1. Kupakwa GV kwenye kidonda
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa j2 tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa
'rangi mbili'
5. Kupamba kadi sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe
kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa na mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au
pindo la kanga
9. Kwenda kuangalia sinema za
Ukimwi na Lishe sokoni
10. Ku rewind kanda kwa peni
11. Ndala kuchemshwa ili
zisiishe
12.Kucheza umeshikilia kaptula
sababu mpira umekatika
13.Kuchonga penseli na meno
14. Kukata ndala, ati ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni
kisa nywele ndefu
16. Wewe unakumbuka nini...?
 
Sa tutafanyaje wakati tushakuwa watu wazima.

Ngono tu ndo haipitwi na wakati.
 
Kunyolewa kwa mkasi...hii ndo kali kwa % kubwa hii inakwemda kuisha. Kama c saloon basi hata kwa wembe na kitama. Nimecheka!
 
Kuvaa kiatu/nguo oversize
Kuoga nje
Kuchoma mswaki Moto palipo katika
Kunywa maji kwa kukinga maji mikononi
 
Kuiba sh. 10, 5 nyumbani. Umepewa hela ya sadaka na hutoi hiyo sadaka
 
kwa wale mainjinia wawa umeme, umeshawahi kulamba chaji ya betri mitaani? Umeshawahi kutumbukiza fungu la betri chooni kwa imani kwamba hazitaisha nguvu?
 
Kwangu jambo niclo weza acha ni kupiga chabo mhh ilo siwezi acha kabisaaaa
 
Nakumbuka kutafuta Ustaadhi kuchinja Kuku,Mbuzi kwenye sherehe mbalimbali za Home kaajili ya wenzetu Waislam kitu ambacho sasa Mhm hakipo!
 
Back
Top Bottom