Lipi kati ya haya bado unafanya?

Lipi kati ya haya bado unafanya?

kuruka sarakasi kwenye maranda au kwenda xul na maua ya saa nne.
 
SIJUI KAMA SIKU HIZI IPO HII!
1. Kupakwa GV kwenye kidonda
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa j2 tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa
'rangi mbili'
5. Kupamba kadi sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe
kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa na mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au
pindo la kanga
9. Kwenda kuangalia sinema za
Ukimwi na Lishe sokoni
10. Ku rewind kanda kwa peni
11. Ndala kuchemshwa ili
zisiishe
12.Kucheza umeshikilia kaptula
sababu mpira umekatika
13.Kuchonga penseli na meno
14. Kukata ndala, ati ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni
kisa nywele ndefu
16. Wewe unakumbuka nini...?

hakuna hata moja arifee
 
kwa wale mainjinia wawa umeme, umeshawahi kulamba chaji ya betri mitaani? Umeshawahi kutumbukiza fungu la betri chooni kwa imani kwamba hazitaisha nguvu?
umenikumbusha mbali aise....japo ni injinia mtarajiwa ila sio wa umeme! wengine tulikua tunasema ukilamba betri yenye chaji ulimi utakatika lol..
 
Kutumwa dukani kununua mawe ya tochi na mdingi akimaanisha betri za tochi
 
kupiga picha ukiwa umeshikilia kiuno mapozi
 
kwa wale mainjinia wawa umeme, umeshawahi kulamba chaji ya betri mitaani? Umeshawahi kutumbukiza fungu la betri chooni kwa imani kwamba hazitaisha nguvu?

Hahahahaha ili uweze kupiga mziki siku nzima wakati una kanda moja ya Awilo na radio 1 ndo inashika.hahahaha.
 
Back
Top Bottom