Linux (Ubuntu, kubuntu, Debian, fedora, linux mint, kali linux, android etc) special thread

Mkali hii project wamemaliza asee, kwa hii software ni kama office imekalika bila kuhitaji windows tena, taasisi sasa zianze tu kupunguza gharama maana office suite ndio huwa shida kubwa ya maofisi kutumia linux.

Nimeipenda sana hii....
Hata libreoffice ipo poa na openoffice
 
Libre office na OpenOffice hazifikii kiwango cha MS Office ase, ila hii wps office hii...kila kitu, mtu wa windows na mtumiaji wa MS Office hapati shida na hii asee...
ni kweli hata mi nimeliona hilo, nimeielwa sana hii wps.
 
Kurekebisha external yako fuata yafuatayo, kwanza kompyuta yako imeshaathirika nakushauri fuata haya maelekezo kwa kutumia kompyuta ya mtu mwingine, halafu hiyo kompyuta weka smadav 2017.

1. Download software moja inaitwa USBFIX, google utaipata ni bure kabisa.
2. Kuna options zitatokea za kurekebisha(kumuondoa virus) sikumbuki vizuri, utachagua ya kwanza
3. huyo virus atakuwa ametolewa.

Hatua ya mwisho, tafuta mtu mwenye ubuntu, chomeka flash utaona kuna folder limeandikwa drive ndimo humo kuna mafile yako yote, yatoe na hivyo vifolder vingine visivyo na maana vi-delete, basi hapo utakuwa umemaliza mchezo.
 
Njia nzuri ambayo itawork bila ku install chochote kwa PC yako ni command tu fungua CMD halafu Andika drive letter mfano
D: kisha bonyeza enter halafu itatokea kama hivi D:/> utaendelea kuandika command nyingine ambayo ni attrib -r -a -s -h /d /s (kisha bonyeza enter Hapo mchezo umekwisha kuthibitisha Andika dir kisha enter Hapo utaona list ya files na folders zote zilizokuwemo
Command hii lengo lake ni kufichua hidden files n folders
 
hii ni kwa kuondoa shortcut pekee sio virus.
 
WAle ambao kompyutea zao zina webcam(web camera) unaweza weka software moja ambayo inaitwa cheese.
kuinstall andika code zifuatazao.
Code:
sudo apt-get install cheese

wale wazee wa kuedit video na mambo ya mambo ya videos kwa ujumla, huku kuna software inaitwa LIVES, jinsi ya kuinstall LIVE andika code zifuatazo kwenye terminal
Code:
sudo add-apt-repository -y ppa:n-muench/vlc
kisha
Code:
sudo apt-get update
halafu andika code hii kuiweka kabisa
Code:
sudo apt-get install lives
 
Inawezekana ku install idm pamoja na crack yake kwenye Ubuntu? Natumia Ubuntu 16.04 LTS
 
Inawezekana ku install idm pamoja na crack yake kwenye Ubuntu? Natumia Ubuntu 16.04 LTS
Kuinstall inawezekana lakini unaweza isifanye kazi, humu wameweka alternatives to idm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…