Lini ni ukomo wa Msimamizi wa mirathi

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
6,829
1,296
Wana JF naomba msaada; Nimshaurije Dada Esta

John na Joseph ni ndugu wa kuzaliwa tumbo mmoja mkubwawao akiwa John; Kwa kuwa john amefanikiwa kimaisha anamchukua Joseph hadi Dar es salaam anakoishi na kuishi naye na kumsomesha kama mdogo wake; kumbuka wakati huu John hajaoa! baada ya muda John anaoa na kumleta mkewe Jane nyumbani na maisha yanaeendelea; wanabahatika kuwapata watoto 4 (Sara, Peter, Eliza na Esta) na wanendelea kuishi na Joseph sasa ni uncle kwa watoto wao.

John anapata uhamisho wa kikazi kwenda Mwanza anamwacha Uncle Joseph mdogo wake pamoja na Jane shemeji na watoto wake wote katika nyumba yake kubwa iliyoko Magomeni. wakati huu tayari amejichumia mali nyingine ; ofisi ya stationery pale posta mpya; shamba kubwa la michungwa kule Chalinze na Msata; Nyumba nyingine kule Sinza na huko Mwanza alikohamia nabahatika kujenga nyumba nyingine na kwa kuwa John anadumisha mila basi huku Mwanza anaoa mke mwingine na kuishi naye.

Suala John kuoa akiwa mwanza linaleta msuko suko Dar na jane naye anaamua kuondoka nyumbani na kuwaacha wattoto (Sar, petr, Eliza na Esta )chini ya uangalizi wa uncle wao Joseph. huko mbele ya safari jane anaaza na bwana mwingine watoto Grace na Mage; wakati huko Mwanza John anazaa na bimdogo watoto Jerome na Lucy. baada ya Miaka mitano ya kukaa Mwanza John anaacha kazi na kuamua kurudi Dar kuendeleza miradi yake kwa kuwa Jane mkewe wa kwanza hayupo nyumbani ; huku akimwacha nyuma mkewe wa pili, na John anamajukumu kwani naye ameoa.

John na Joseph wanakubaliana kuwa maadam Joseph kaoa basi aende kuishi Buguruni pamoja na watoto wake John kwenye nyumba yake John. Baada ya mwaka moja wa kuishi Dar; John anatarikiana na bimdogo yule kule Mwanza na kuamua kumwachia nyumba ya kule Mwanza ikiwa kwa ajili pia ya watoto waliozaa pamoja.

Mwaka mmoja baadaye John anafariki na inakubalika (cjui ni kiukoo) Joseph awe ndio msimamizi wa Mirathi kwani katika watoto hakuna aliyefikisha miaka 18! Joseph anachukua biashara za Marehemu kaka yake na kuziendesha anafanikiwa kuendesha kilimo cha michungwa na ufugaji wa kuku kule mashambani hata anapanua biashara na kuanzisha chuo cha ufundi huku akiwasomesha watoyo wa marehemu. mapaka wote wanhitimu kidato cha nne. Sara binti wa kwanza wa John anajifunza ufundi na anaolewa na kuhamia kwa mumewe! Peter anajifunza ku operate computer na hatimaye yeye anakabidhiwa stationery ya kule mjini posta mpya; Eliza anaenda kusomea ualimu na baada ya masomo anapata mchumba anaolewa Esta kitinda mimba anamaliza form four na anafaulu vizuri lakini hapelekwi shule kwani ni mtundu sana na hatimaye anbeba uauzito hivyo huyu abaki nyumbani tuu; Miaka 2 inapita Esta yupo tuu nyumbani analea mwanawe; hakuna msaada wowote!

Sara hana shida; yuko kwa mumewe na hana mpango wa kumsaidia mdogo wake
Peter amekabidhiwa mradi hivyo kwake naye haimuhusu
Eliza bahati mbaya anafariki
Esta yupo tu kwa baba Mdogo Joseph na familia yake huku hajui hatima ya maisha yake na sasa mwanawe mdogo Frank!

mama yao huko aliko naye alifariki!

Samahani nimewachosha na kisa kirefu;

Lakini je Esta anayo nafasi gani kisheria ya ku contest custodian ya mali zilizokuwa za baba yake?
Ukizingatia ndugu waliotegemewa kumsaidia hawana msaada kakwe na huyu kakake ndio amependelewa na Baba yao mdogo Uncle Joseph?
Je sheria inamsaidieje kuzuia ukomo wa Msimamizi wa sasa Uncle Joseph?
 
Mmh nimesoma kisa hiki kirefu kweli, ngoja nipitie Probate and Administration of Estates Act kwanza nitarudi kwa mchango zaidi.
 
Mwendelezo ;

Nyumba ya magomeni imepangishwa kwa muda mrefu kwa Jamal; katika hali yakutatanisha Peter amemuuzia Jamal nyumba biala ya kuwashirikisha ndugu lakini siju katiaka makubaliano yepi Jamal hakupewa hati ya nyumba; Uncle Joseph kaamua kumfukuza Jamal aondoke lakini hakutaka mpaka akafikishwa mahakamani na mahakama iliyosikiliza imeamuru jamal atoke; Jamal kakata rufaa; kesi inaendelea; Ukiacha Peter; Ester na Sara hawajui mwenendo wa kesi; Uncle Joseph anadai ataishughulikia!

On another twist of events

Uncle joseph kaitisha watoto wa Johna na wale wa Mage; kadai atawakabidhi mali zao
Peter anakabidhiwa moja kwa moja ofisi iliopo mjini na nyumba iliyoko Sinza
Ester Anakabidhiwa shamba eka 2 na nyumba iliyopo Chalinze
sara anakabidhiwa shmba lilopo Msata
Inafahamika marehemu alikuwa na shamba Kisarawe; hili wanakabidhiwa watoto walizaliwa nje na Jane (Grace na Mage)!
Nyumba ya Magomeni wanaambiwa ina mgogoro mahakamani!

Je Esta akubali mgao huo?
Ni utaratibu gani unatumika kugawa mali?
 
Back
Top Bottom