Linganisha Zitto Kabwe na Wabunge wa CHADEMA

Linganisha Zitto Kabwe na Wabunge wa CHADEMA

Mmawia,

Mmawia unapomjibu mtu namna hiiinawezekana moyoni mwako ukaona umempatia lakini kwa wenye kuelewa huu si utetezi mzuri kwa chama chako, unakuharibia zaidi kuliko kujenga. Tambua Tanzania bado kuna kundi kuwa la watu amba hawajafanya maamuzi kuhusu chama cha siasa. Ushawishi wa kimantiki unatakikana.

Inawezekana huyo uliyemjibu unafahamu mlengo na lengo lake la posti sasa badala ya kumkamilishia mlengo yake ungetumia nafasi hii kumfanya kama daraja la kuvukia kwa kutumia maneno yake mwenyewe. Ukitulia na kutafakari vizuri utatambua kuliko ulivyojidhalilisha, kukidhalilisha chama na kuwadhalilisha mama na dada zetu.
 
Kumbuka! Sukari 3000 Kutoka 2000 na huu ni mwezi wa sita tu tangu tuishike ikulu.
Bavicha...dah kama KUB tu,yaani wao ni bei ya sukari na bia ndio hoja yao...kama KUB na wenzake kasusa bungeni kisa mafungu ya chai,bia na fulana kuelekezwa kwenye elimu.
 
Anachopigania Mbowe na wengine ni kuona mapambano yao dhidi ya udhalimu wa serikali na wananchi wanafahamu kila hatua. Huwezi kufanya mapambano ya kisiasa gizani halafu utegemee upande mmoja wa kujibu mapigo ndio ujitangaze.
Upinzani sehemu pekee ya kuweza kufahamika katika jamii nini mwelekeo wao ni bungeni na kidogo sana nikutano ya hadhara sasa kwa nini wakubali kufanyia shughuli zao gizani? Tena kwa mikutano hii ya hadhara ya bunge?
Tutarudia kusema hili mpaka lini nyie viziwi?
 
shikamooo zitto....!!!!! huwa napenda kukufananisha na messi katika siasa za bongo
 
Nimetazama na kusikiliza kwa makini hizo clip mbili tulizowekewa. Nifah hoja yako ni sawa, kwamba mazingira ya clip hizo ni tofauti kwa hiyo siyo sahihi kuzitumia hizo kuwalinganisha hao wawili. lakini pia, ukisema Zitto peke yake anawakilisha ACT-Wazalendo, ni sawa kwa sababu kwanza yeye ni "Kiongozi" wa chama hicho, cheo cha ngazi ya juu kabisa. pia yeye ndiye mbunge pekee wa chama hicho katika bunge hili. kwa hiyo Zitto anawakilisha kweli chama chake, peke yake. lakini Msigwa je? yeye ni mmoja kati ya wabunge wengi wa CHADEMA, na siyo kiongozi mkuu wa chama. kwa hiyo huwezi kumtumia yeye tu kama kiwakilishi, kwa kiwango kile kile unachoweza kumtumia Zitto kama kiwakilishi.

Lakini yote hayo tisa, nikasema OK, ngoja basi tuone nini kinaendelea pale kwa Msigwa. Pale, Msigwa anapambana na dola! anapambana na CCM! Nimepata nukuu ya kilichokuwa kinaendelea:

"Vurumai hizo zilizotokea baada ya Msigwa kukasirishwa na kitengo cha DC kutaka kumuengua ili asionekane anatoa msaada kwa watu wa jimbo lake bali DC ndio ionekane anajali wananchi. Shutuma zilienda mbali baada ya Msigwa kumueleza DC kuwa anajua anamhujumu na amekuwa anapanga mikakati ya siri ya kumfanyia hujuma ili aonekane hafanyi kazi jimboni kwake.

Juhudi hizo zimefanyika wiki iliyopita ambapo DC kwa kushirikiana na Humphrey Polepole waliandaa "mdahalo" na wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Iringa na kuanza kumsema vibaya Mbunge Msigwa, katika mdahalo huo Polepole amerekodiwa akisema Iringa walikosea sana kumchagua Msigwa sababu alikuwa anamuunga mkono "fisadi" Lowassa

Wakati DC Kasesera alimshutumu Mbunge Msigwa kutokwenda Tarafa ya Pawaga kusaidia wahanga wa mafuriko na Msigwa akamjibu kuwa aanze kumwambia Lukuvi kwa nini hajaenda maana Tarafa ya Pawaga ipo ndani ya Jimbo la Isimani, na hata yeye akienda sio lazima DC ajue, kama ambavyo yeye anaenda na kupiga picha na kurusha Facebook akimbeba mpiga picha ambaye haitaji msaada wa kubebwa.

Vurugu hizo ziliamuliwa na diwani na Meya wa Mji. Mwishoni Msigwa akamwambia DC awaite polisi wamuweke ndani maana katika vikao vya CCM DC Kasesera amekuwa akisema lazima amuweke ndani Msigwa kumtia adabu
"

Hayo ndiyo mazingira ambayo wapinzani wanafanya kazi ya siasa katika nchi hii. wanapambana na kila aina ya vikwazo. ukiona hivyo, ujue huyo ndio mpinzani wa kweli. Ndio maana kwa Wapalestina, kuna sifa za kiongozi wa kuaminiwa. mojawapo ni kwamba lazima awe amefungwa kataka jela za Israeli kwa kipindi kadhaa na mara kadhaa. Na ukiona mpinzani anasifiwa sana na hao anaowapinga, basi ujue iko namna. na ukiona mashabiki wa chama tawala wanamsifia mpinzani, basi ujue huyo siyo mpinzani tena. ni shosti wa watawala. wanagawana tonge. hao ndio washirika wa kufisidi watanzania. "partners in corruption".


 
Hizi takwimu umezipatia wapi?
Hivi wananchi walioko mijini ni wangapi na walioko vijijini ni wangapi?
Na umewahi kutembelea vijiji vingapi!
Maana vijijini nako kuna muamko mkubwa sana wa vyombo vya habari.
Sijui unaongelea wananchi wa nchi gani.

Eti Watanzania wanaomiliki luninga na visimbusi ni 15%?Like serious?
OMG....
Barbarossa nashindwa nikuweke katika kundi gani,maana wewe ni zaidi ya mpumbavu.
Hizo takwimu zake labda ni kwa wakaazi wa mkoa wa dodoma tu
 
Kwanza kwa kukusaidia tu, wala siyo TZ bali hata hapa Dar tu, watu wenye TV hiyo 15% hawafikiii, yaani namaanisha wenye TV majumbani mwao na siyo wanao angalia Bar!
Kama wewe huna sema, siyo unajitia kimbelembele kuwasemea wenzako,kwa hiyo posho ya buku 7 kutoka lumumba wewe kununua luninga itakuwa ni kitendawili
 
Msigwa, Mbowe na wenzao, hawawezi kujenga hoja za kimaendeleo kwa sasa. Walimtegemea zamani Zitto na Dr Slaa, sasa hivi wamebaki ni wanaharakati tu, wanangojea matukio tu, hawana mpango kazi wala dira ya 2025 kabisa.
 
Kwikwikwi CHADEMA kwisha habari tunasubiri mazishi tu. R.I.P CHADEMA.
 
Unalinganisha kamtu kamoja na taasisi yenye wabunge zaidi ya 40? Upumbavu wa kitanzania. Mapenzi binafsi kwa mtu mmoja
 
Kushangaa CCM kukubali hoja za Zito,ni sawa na kushangaa ngedere kula mahindi
 
Elimu ya mulugo inakupeleka kubaya
Mmawia its true that you cant win an argument with a stupid man. The more you argue the more stubborn they become. I agree to disagree ZZK is far intelligence than KUB and KUB and his merry men will continue with they're ridiculous stance in the house which don't benefit anybody.
 
Mmawia its true that you cant win an argument with a stupid man. The more you argue the more stubborn they become. I agree to disagree ZZK is far intelligence than KUB and KUB and his merry men will continue with they're ridiculous stance in the house which don't benefit anybody.
ZZK anasimama kama muwakilishi wa ACT kama mnaona anafanya vya maana kisifieni chama chake ACT na ikiwezekana chukueni kadi mjiunge ACT naona....hii ni pale chama cha kifisadi kinapojaribu kukipaisha chama kimoja kwaajili ya manufaa yake,
 
Hizi takwimu umezipatia wapi?
Hivi wananchi walioko mijini ni wangapi na walioko vijijini ni wangapi?
Na umewahi kutembelea vijiji vingapi!
Maana vijijini nako kuna muamko mkubwa sana wa vyombo vya habari.
Sijui unaongelea wananchi wa nchi gani.

Eti Watanzania wanaomiliki luninga na visimbusi ni 15%?Like serious?
OMG....
Barbarossa nashindwa nikuweke katika kundi gani,maana wewe ni zaidi ya mpumbavu.
Asante Malkia Nifah
 
Zitto Kabwe anasimama kama muwakilishi wa ACT kama mnaona anafanya vya maana kisifieni chama chake ACT na ikiwezekana chukueni kadi mjiunge ACT naona....hii ni pale chama cha kifisadi kinapojaribu kukipaisha chama kimoja kwaajili ya manufaa yake,
Chama kinachotetea ufisadi TZ hii Ni CHADEMA Tu au Na hao ndo hawampendi Zitto Kabwe
 
Chama kinachotetea ufisadi TZ hii Ni CHADEMA Tu au Na hao ndo hawampendi ZZK
Ngoja nikupe kidogo jinsi fikra za wana CHADEMA waliowengi zilivyo juu ya ZZK
Linapokuja suala la chama kama chama kimetofautiana na ZZK tutasimama na chama kwani tunaamini anaweka pabaya maslahi ya chama
Linapokuja suala la Upinzani dhidi ya kile chama cha mafisadi tutasimama na mpinzani yoyote hata akiwa ni ZZK
Hatutaamini kushirikiana na ZZK katika kipindi hiki mpaka pale tutakapojiridhisha hasimamii maslahi ya Chama Cha Mafisadi
Ndani ya CHADEMA kuna ambao tulikua tunamkubali ZZK kwa hoja na umakini wake hilo bado lipo lakini tutasimama nae kama mpinzani mwenzetu na pale tu atakapokua anasimama kama mpinzani mwenzetu.
ZZK ni mpinzani kwenye damu ni swala la muda tu mambo yake yatawekwa sawa na wapinzani wenzake na watakua meza moja.
ZZK ni mtu CHADEMA ni Chama.....Chama cha ukombozi wa mtanzania
Peopleeeeeees.......
 
Back
Top Bottom