Hili ni tatizo sugu hata jamaa yangu analo kwenye Huawei ascend y 330. Lilishajadiliwa sana hapa lakini inaonekana ufumbuz wake ni pasua kichwa!!
Mtu aliyepigana vya kutosha na tatizo hili ni
Mu7 ebu fuatilia maelezo yake kama yakusaidia:
Nifuatilie kwa makini:
Usisumbuke kutafuta suluhisho la hiyo Gps
kwenye simu yako. Mimi natumia Tecno M7.
Mwaka jana nilipata tatizo kama hilo
nikahangaika sana kulirekebisha kwa setting
kwenye simu yangu, ikashindikana. Nilibadili
hata Launcher haikusaidia. Nikamshirikisha
fundi mmoja mtaalamu sana wa simu naye
akashindwa. Fundi wa pili ndio akanipa ukweli
kuwa ni issue ya mtandao wa Airtel. Na kweli
ukiweka line ya mtandao mwingine Gps
haijiwashi kabisa ila ukiweka Airtel tu inawaka
na kila ukiiweka off inajiwasha yenyewe baada
ya muda mfupi tu.
Niliwapigia Airtel Huduma kwa Wateja nikaeleza
shida yangu na mtoa huduma akaniahidi
kulishughulikia. Jioni ya siku hiyo akanipigia
simu akinieleza kuwa ameshalishughulikia,
nizime simu na nisiiwashe tena mpaka kesho
yake asubuhi. Kesho yake nilipowasha, kweli
halikuwepo tena.
Mwaka huu limejitokeza tena mwezi Juni
nikawapigia tena Airtel Huduma kwa Wateja
lakini niliambulia kupewa ahadi za tatizo
kushughulikiwa mpaka nikakata tamaa.
Niliamua kuhama mtandao jumla kwa maana ya
ununuzi wa vifurushi maana shida hiyo
inatokea kwenye Slot 1 ambayo ina access ya
3G na hutokea uwapo katika eneo lenye
network ya 3G tu. Slot1 nimeweka Vodacom na
Slot 2 Airtel na Gps haijiwashi kabisa. That's
the only solution. Atakaekuelekeza tofauti na
hapo mwongo!