Lindi yetu na Sri Lanka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lindi yetu na Sri Lanka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zitto, Sep 20, 2012.

 1. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Lindi yaweza kuwa Sri Lanka ya Tanzania|Zitto Kabwe, Mb

  Watanzania wengi tukisikiajina Sri Lanka jambo kubwa linalotujia kwa haraka ni ama Chai au Vita ya TamilTigers. Nakumbuka tulipokuwa darasa la sita Shule ya Msingi tulisoma ‘Chai SriLanka' na kusoma miji kama Kolombo, Batikaloa na Trinkomalee (Colombo,Batticaloa, Trincomalee). Lakini tulipashwa sana habari kuhusu vita vya wenyewekwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka takribani thelathini. Juzi nilikuwa SriLanka. Vita imekwisha mwaka majuzi 2009. Chai ipo nyingi sana. Mwaka 2010 SriLanka iliuza nje jumla ya tani 314,000za chai yenye thamani ya dola za kimarekani 1.37 bilioni na hivyo kuongozaduniani kimapato ingawa Kenya ilisafirisha chai nyingi zaidi, tani 441,000.Hata hivyo kutokana na ubora wa zao hilo kuwa chini kidogo Kenya ilipata dolaza kimarekani 800 milioni tu. Mwaka huo Tanzania, yenye eneo kubwa zaidi lakulima nchi zote hizo iliuza nje tani 34,000 tu na kupata dola za kimarekani 61milioni hivi. Licha ya kwamba Tanzania ni nchi ya nne kwa kuzalisha Chai Afrikabaada ya Malawi, Uganda na Kenya, bado inaweza kuwa katika nafasi ya juuduniani iwapo tukiamua kuwa makini katika mambo tufanyayo na kupenda kufanyamambo makubwa.

  Siku hizi napenda sanakujua historia za nchi katika kupambana na umasikini wa watu wao. Lengo nikuelewa juhudi za nchi mbalimbali katika kuleta maendeleo ya watu na kujifunzapale ambapo nchi zimefanikiwa. Ukitembea mitaa ya Jiji la Colombo unaona mjimzuri msafi uliopangwa vema na kila mtu anaonekana kushughulika. Njia nzuri yakujua ukweli wa maisha ya watu ni kuongea na watu wenyewe. Mara nyingi hutumiamadereva wa taxi au Bajaji kwa jiji kama la Colombo. Katika mazungumzo nabaadhi ya madereva wa Bajaji nilizokuwa natumia pale Colombo niliona mwelekeommoja wa. Kwamba katika kipindi cha miaka 10 iliyopita maisha yao yamebadilikasana. Wakisifia kuisha kwa vita dhidi ya Tamil Tigers na kuongezeka kwa mapatoyao kwa watu kutumia zaidi usafiri. Dereva wa Bajaji wa Jiji la Colomboanaingiza wastani wa rupia 4000 (shilingi45,000) kwa siku. Nikataka kujua nini kimepelekea mabadiliko haya ya kipatoambacho mpaka wenye Bajaji wanafaidika nayo. Takwimu zao zinaeleza mengi sana.Serikali iliamua kupambana na umasikini na hasa umasikini wa vijijini.

  Mwaka 2002 asilimia 22.7ya wananchi wote wa Sri Lanka walikuwa wanaishi chini ya mstari wa umasikini.Ilipofika mwaka 2011 kiwango cha umasikini kilikuwa asilimia 6 tu. Umasikiniulishuka kwa kiwango kikubwa katika maeneo ya vijijini. Katika kipindi chamiaka mitatu kati ya mwaka 2007 mpaka 2010 umasikini wa wananchi wa Sri Lankawalio kwenye sekta ya Chai (Estate sector) ulishuka kutoka asilimia 32 yawaliokuwa wanaishi chini ya mstari wa umasikini mpaka asilimia 11.4 na wale wa vijijini nje ya sekta ya Chai umasikiniulishuka kutoka asilimia 24.7 mpaka asilimia 9.4 katika kipindi hicho. Nilipoulizazaidi kwa wanasiasa na viongozi wa Serikali nikaambiwa kuwa mabadiliko makubwayaliyotokea miaka ya karibuni yalitokana na Serikali kufanya maamuzi mahususiya kuelekeza fedha nyingi zilizokuwa zinakwenda vitani kwenye uwekezajivijijini. Wanasema walitumia fedha nyingi kwenye ruzuku ya mbolea kwa wakulima,kusambaza umeme vijijini na kujenga barabara za vijijini. Siku niliyofikaniliona kwenye moja ya magazeti yao lakila siku Rais wao akizindua Mtambo wa kuzalisha umeme katika mji waTrincomalee uliopo Mashariki ya nchi hiyo.

  Nikajiuliza mbona na sisitunatekeleza MKUKUTA na tunasema kwamba tunawekeza fedha nyingi sana vijijini?Mbona na sisi tunatoa ruzuku ya Mbolea yenye thamani ya zaidi ya shilingibilioni 60 kwa mwaka? Inakuwaje wenzetu wafanikiwe sisi tusifanikiwe? Tanzaniaimeanza kutoa mbolea ya ruzuku katika msimu wa mwaka 2006/2007 kama ilivyo kwaSri Lanka. Wenzetu katika miaka 3 kiwango cha umasikini kimepungua kwa asilimia15 kwa wananchi walio katika sekta hiyo ya Kilimo na wanaoishi vijijini. Sisikatika kipindi cha muongo mmoja, 2001 mpaka 2011, umasikini umepungua kwaasilimia mbili tu. Moja ya sababu ya sisi kushindwa ni kwamba mfumo wa mboleaya ruzuku umegubikwa na ufisadi wa hali ya juu sana. Mfumo huu umedhihirishanamna ambavyo kazi ya kupambana na Ufisadi ni ya kimfumo zaidi maana kwa namnaviongozi wa vijiji wanavyoiba mbolea ya ruzuku unaweza kiurahisi kabisa kusemarushwa ni sehemu ya utamaduni wa Mtanzania. Siamini hivyo. Ninaamini kwambamfumo wetu unazalisha wala rushwa, walafi na watawala wenye tamaa nawasiotosheka kama nilivyoeleza katika makala zangu zilizotangulia. Je tukiondoaufisadi wa mbolea ya ruzuku tunaweza kupata mafanikio ambayo wenzetu wameyapata?Sina jibu wala jawabu la swali hili. Hata hivyo ninaamini kwamba kutofanikiwakwetu ni zaidi ya ufisadi. Ni kutofanya kazi kwa bidii? Ni kukosa umakini? Nikutofurahia mafanikio? Ni kukosa uongozi thabiti unaoweza kusimamia mchakato wamaendeleo kuanzia ngazi ya kijiji mpaka Taifa?

  Hebu tutazame pamojatakwimu hizi. Sri Lanka ina ukubwa wa kilometa za mraba 65,000. Mkoa wa Lindiuna ukubwa wa kilometa za mraba 66,000. Sri Lanka ina Pato la Taifa la dola zakimarekani 60 bilioni mwaka 2011, Tanzania Pato lake la Taifa ni dola zakimarekani 24 bilioni. Sri Lanka ina jumla ya watu milioni 20, Tanzania inajumla ya watu milioni 45, Mkoa wa Lindi una jumla ya watu 750,000 hivi. SriLanka na Tanzania zote zina Bajeti ya dola za kimarekani bilioni Tisa hivi.Uchumi wa Sri Lanka unategemea sana zao la Chai na Utalii kwa fedha za kigeni.Mkoa wa Lindi una eneo kubwa zaidi la Kilimo kuliko Sri Lanka nzima hasaukizingatia katika hekta 5.2m zinazofaa kwa Kilimo ni hekta 500,000 tu ndiozinalimwa. Zao la Korosho laweza kuwa Chai ya Lindi. Kilometa za mraba 18,000za mkoa wa Lindi ni Selous Game Reserve, Kilwa ni kivutio tosha cha utalii wakila namna na Mkoa wa Lindi una fukwe ambazo hazijawahi kuguswa toka duniaiundwe na mola.

  Sri Lanka hawana GesiAsilia. Lindi na hasa Wilaya ya Kilwa ndio mzalishaji mkubwa wa Gesi asiliahapa nchini. Pia sehemu kubwa ya Gesi iliyogunduliwa hapa nchini ipo katikamkoa wa Lindi inagwa wengi wetu hudhani kwamba ipo mkoa wa Mtwara. Lakini Lindina Mtwara sawa tu. Mtwara ina kilometa za mraba 16,000 (chini ya eneo la Lindilililopo Selous). Tufanye Lindi na Mtwara kwa pamoja ndio Sri Lanka yaTanzania. Tunaweza kujenga uchumi wa dola za kimarekani bilioni 60 kwa Lindi naMtwara? Tunaweza kufanya mikoa hii iwe na kiwango cha umasikini chini yaasilimia 3 ya wananchi wake? Tunaweza kuingiza watalii 800,000 kwa mwaka kwamikoa hii tu? Tunaweza kuuza nje Korosho yenye thamani ya dola za kimarekaniangalau 600 milioni? Tunaweza kutumia sehemu ya Mapato yatokanayo na Gesi asilikujenga miundombinu ya barabara, umeme, reli na maji kwenye wilaya zote za hiiSri Lanka yetu? Tunaweza kuwekeza kwenye Elimu kuhakikisha kila motto anapataelimu bora? Tunaweza kuhakikisha kuwa asilimia 97 ya wakazi hii Sri Lanka yetuwanapata huduma za Afya?

  Majibu ya maswali yotehaya ni NDIO. Utashi. Utayari. Uthubutu. Hebu tuthubutu kuiweka Sri LankaTanzania. Lindi na Mtwara ni zaidi ya Sri Lanka. Nikipata fursa ya kuandikatena nitaandika kuhusu uwekezaji kwenye Elimu nchini Sri Lanka na kwamba Hakiya kupata Elimu mpaka Chuo Kikuu ni haki ya kikatiba yenye kuweza kudaiwamahakamani.
   
 2. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,062
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Chini ya uongozi wa? Tatizo la Watanzania hawajui kuwa huwezi kutarajia kuvuna maembe kutoka kwenye mvule! Mvule hauna matunda jamani. Na kama kwa miaka 50+ tumeambulia hapa tulipo, basi hiyo hamsini mingine haitakuwa tofauti. Dalili ya mauti ni Ukimwi!
   
 3. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Ni kwamba viongozi wakishaingia panono fikra hutoweka na kuanza fanya kinyume na ahadi na viapo walivyokuwa wakijiapiza enzi wakiwa katika vumbi jingi.

  Ulisha spend sometimes kujiangalia kama umebadilika toka kipindi fulani?Na mabadiliko hayo bado hayajagusa malengo yako miaka kadhaa nyuma?Pengine unaweza tafakari na kupata majibu unayoyauliza hapa.Umewahi kiuliza mawee ya kigoma na dagaa zingeweza kuwa tofauti kwa kiasi gani?
   
 4. ma2mbo

  ma2mbo JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Naona sasa ivi kila mtu akili yake ipo Lindi,ngoja na mimi nianze kujipanga tufaidi na sisi vya kwetu...maana tukizubaa baadae tutaishia kupiga kelele wenzetu wala.
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Watalii laki nane Lindi?
  infrastructure ya watalii laki nane sio kitu rahisi hivyo
  ni bora tu tupange maendeleo kwa ujumla tu....
  kuliko hizi za watalii laki nane Lindi
   
 6. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  watalii idadi hiyo ndio inakuja nchini na bado accomodation ni issue.pengine watatumia ndege kwenda selous na kurudi lala kwingine huku wengine wakilala ktk mahema na hotels/lodge chache za selous.Kwanza hospitality industry ni duni sana Lindi,songea,morogoro,mtwara,iringa,mbeya, mpaka rukwa.Yaani ni kama tanzania kufikiri andaa kombe la dunia.

  Zoezi la Miss Tanzania tuu limeonyesha jinsi gani kulikuwa na tofauti za vigezo vya tasnia ya urembo.Thanx God,ukuaji wa media umesambaza ufahamu.
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  Hii habar ya Sri lanka ,mara Singapore,mara Malaysia
  ni rahisi mno kuizungumza mdomoni
  kilimo for export while mafuta tu ya kula tuna import?
   
 8. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,530
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  na hiyo ni nchi iliyokua kwenye vita vya ndani

  sisi hatuna vita wala majanga.... sifa yetu kubwa ni majungu, kukata viuno na majungu
   
 9. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Well said,nilikuwa na hilo wazo ila nikasema nisubiri wengine kama wanaona hilo.Mh. amekuwa na roll model wengi sana wengine wamepiti anjia tofauti sana kufikia hapo walipo, kuna waliotumia matendo yasiyo na haki za binadamu na kuna wengine wameharibu mazingira sana, etc kwa hiyo si wote wanaweza kuwa mifano kwa pamoja katk nchi moja.Wengine walifika hapo kutoka na hali ilivyokuwa ikibadilika.

  Seems mheshimiwa anapiki kila kitu king`aacho, bila kujua ndani ili kupata namna ya kuyageuza yote hayo ina our own ways.Na kuja na plan inayofanya kazi.

  Vipaumbele vingi kama JK?sasa Lindi na utalii si tunaanza mambo ya Zenj,kuzua wabara wasiende.Watajaa watu wa Arusha na Kilimanjaro katika kila sector ya utalii hadi waanze lia kutaka ulinzi.Zenj wenyewe hawana huduma nzuri kabisa, ni kwa vile wawekezaji wengi ni wageni na wamewekeza usimamizi mzuri kwa wafanyazi kiasi cha kuwafanya wasionyeshe kushindwa kufanya kazi under minimum supervision.
   
 10. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  hivi haya mambo uliyoya note JK Hayaoni anapokuwa ziara nje ya nchi?
  Nilichogundua kwa haraka ni kuwa TANZANIA tukipata uongozi mzuri na usimamizi thabiti wa vipaumbele tunaweza kabisa kuwa na pato la taifa MARA 30 ZAIDI ya sri- lanka.
   
 11. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  tunayo vita kubwa sana katik fikra sahihi.Hatuna misingi katik kila kitu kuanzia tamaduni, misingi ya haki, malengo ya muda mrefu na mfupi, na hivyo tumeishia kukosa consistency ktk kila nyanja kitaifa.Sasa hivi watanzania ni wepesi sana k buy cheap ideas .Utaona tupo wepesi kushika kila kitu ndio maana tunakosa kila kitu.
   
 12. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,530
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  na kuamini serikali ndio suluhu ya kila kitu, hata namna ya kupunguza vitambi na majungu
   
 13. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,530
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  i think as part of the plan... lazima kuangalia nini kinahitajika kuserve the purpose kwahiyo vitu kama hivyo should be considered in th eplan,

  whenever planning for any kind of business, huwezi kusahau social services and security kwenye planning equation
   
 14. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  kuamini serikali ni dhambi ya ujamaa kuifanya dola kuwa ndio Mungu.Kwa kila nchi ya kijamaa hata mtu aliyeajribu jituma katk ubunifu kidogo tuu lazima alilie serikali?Mifumo mingine ya nchi huichukia serkali sana kwa vile huchukua kodi yao na kuichezea vibaya au kupanga policies mbaya zinazowazuia kukimbizana na maisha.Wajamaa wanaita "selfishness" wakti wanajua binadamu ni selfish ndio maana hana policy ya kusahre mke wa ndoa n anafanya wa ufanisi sana kazi inayoitwa yake.

  MAtajiri waliotengeneza hela kihalali wanazichukia serikali sana,kwani wao hutumia tuu,hulipana mishahara tuu kwa hela za wengine na ndio maana agenda ni kuwahonga wajinga wanasiasa na kuzichukua hela zao kwa mgongo wa nyuma.Sisi tunapenda serikali na wezi wake.
   
 15. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,530
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  Binafsi naamini serikali nyingi hasa za africa ni far worse than malaya wanaopata ujira kwa kazi ngumu.... mifumo mingi ya serikali ni kutumia cha maskini na anayeishi kihalali, kukusanaya mapato, kukalia vikao, kulipana kufanya yasiyo ya lazima na kuzidi kutumia

  have you ever asked yourself, Tanzania tungefuta regional administrations, na kuweka district administration yenye only 50% ya walio sasa tunepunguza chochote kwenye tija??

  we are just focusing on feeding people and not generating income to feed more people
   
 16. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  kila siku wapo busy katik vikao vinavyokula hela, waki discuss jinsi ya kuongezewa posho..ila hawana hata element ya kujiuliza kwanini hawanajamaliza daily tasks.Huku wakiiba hadi stationeries.
   
 17. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  With this mentality hakuna kitu.watanzania tuna excitement kuliko mipango na determination ya kufuata hiyo mipango ili kufikia mafanikio tuyatakayo.
   
 18. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #18
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nimeona na kusoma nchi nyingi za Asia raia wake wanajali sana utaifa kuliko ubinafsi, ndo maana nchi nyingi sana za Asia ambazo zote zilikuwa maskini sana wakati wa ww2 zilipopata mwanya kidogo tu zimepiga hatua za ajabu.
  kuna kipindi nilisoma Post-War Japanese economy, wale wenzetu walifanikiwa kutoka kwa sababu ya uzalendo wa raia wao wakiongozwa na viongozi wao. walikuwa wanapelekwa nje ya nchi kusoma, walihakikisha wanasoma kwa manufaa ya taifa, wanarudi nyumbani na kuendeleza................ na strategies hizo hizo ndo zinatumiwa na mataifa mengine ya Asia.
  sasa sisi, raia wabinafsi, wengi wetu wa SSA tukipata mwanya wa kukimbia nchi zetu wala hatujiulizi mara 2. mtu anaenda kusoma nje, anasoma hadi PhD anaona bora abaki huko huko aendeshe taxi kuliko kurudi nyumbani kusaidia hata kufundisha sekondari. mtu anawaza tumbo lake na jamaa zake, siyo taifa. tukija kwa viongozi wetu ndo yaani najisikia kulia tu, kila likitoka bomu moja linaingia jingine. kwa mtindo huu tusahau kabisa kukutana na wenzetu, tutaishia kwenda kujifunza kila siku na hatu-graduate.
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,585
  Likes Received: 1,953
  Trophy Points: 280
  Mambo ambayo mleta mada(ambaye ni kiongozi) ameyaorodhesha kama ndiyo kikwazo,lakini kwa namna ambayo ni kama hana uhakika kwasababu ameyaorodhesha kama maswali.Nilitegemea hoja yake hii ingekuwa walau na mapendekezo mawili matatu given the fact that he's a leader.

  Kama alivyofanya kwenye kutolea mfano wa ufisadi wa mbolea,ameuliza maswali,tena kuna hilo ambalo rafiki yake JK kalisema kuwa "watu hawapendi kuona maendeleo",nadhani akimaanisha wapinzani.Hilo la Zitto sijui kama alizungumzia individually ama as a society(kwamba hatupendi kuona maendeleo).Kwa namna nyingine,ni kama haamini moja kwa moja kuwa ufisadi ndo tatizo kuu.

  Pamoja na kwamba ni kweli ufisadi unaweza kuwa pia ni tatizo la kimfumo,lakini hajatoa mapendekezo ama solutions.Makala hiyo ni nzuri tu lakini siyo yenye kuprovide solutions.Mleta hoja ametolea mifano ya mambo yanaoonyesha usawa ama mfanano kati ya mkoa/mikoa yetu wa/ya Lindi/mtwara vs Taifa la Sir Lanka,bila kuona kuwa mipango yetu kwa Lindi ni ya kimkoa na ile ya Sir Lanka ni ya kitaifa.Inawezekana kabisa kwamba Lindi ingekuwa Taifa basi lingekuwa mbali sana.

  Sisi tatizo letu kubwa ni uongozi hilo siyo siri hata kidogo.Ni hatuwa walizozichukuwa viongozi wa mataifa hayo ndizo zilizowafikisha hapo walipo.Viongozi kulalamikia wananchi ndo tatizo lenyewe.Tunategemea solutions kutoka kwa viongozi na si malalamishi.Kiongozi akilalamika wananchi nao wafanyaje?Kiongozi asipokuwa na solution ya nini cha kuwafanyia wananchi,wananchi wanatakiwa wafanyeje?

  We lack leadership,thats the fact,ngoja tusubiri kama kiongozi wetu atatoa na ushauri wa nini kifanyike,yeye si mmojawapo wa watunga sheria?Mbona China wananyonga mafisadi na ni ushahidi tosha kabisa kwamba hilo limesaidia taifa hilo kusonga mbele?

  Kwanini asiseme yeye kama kiongozi,tufanye so and so kuutokomeza ufisadi kama ni kweli anaamini kuwa ni kikwazo cha maendeleo yetu?

   
 20. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #20
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Zitto kumbe upo? Habari ya siku nyingi broda

  By the way, nimefurahi kukuona kwamba you are still alive and kicking. ngoja sasa nirudi kwenye hoja yako kisha nitarejea kwa comment
   
Loading...