Lindi: Rais aagiza RC Zambi kumnyang’anya passport mkandarasi wa mradi wa maji wa Ngapa

Benz Petrol

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
504
195
Rais John Pombe Magufuli amemuagiza RC Lindi Godfrey Zambi kumnyang’anya pasi ya kusafiria mkandarasi wa mradi wa maji wa Ngapa hadi atakapomaliza ujenzi huo.

Pia Rais Magufuli ampa Waziri wa Maji Gerson Lwenge miezi 4 kuhakikisha maji yanapatikana katika mradi wa maji wa Ng’apa mkoani Lindi.

Update: Video clip

tanzania ni shamba la bibi mtu anayejiita mkandarasi amekula hela na mradi haushi
 
Hatua nzuri. Hakuna mtu kusafiri mpaka amalize kazi

mhh umeshafika kila jambo wew unaonaga sawa Tu

umeshajaribu kujiuliza huyu mkandarasi Ni wa nchi gani

Na wewe ulie anzisha uzi mbona hujatoa taarifa kamili sababu ya mkulu kutoa maagizo ayo

ata kama ni kachelewa kumaliza mradi zipo sheria za adhab ya kuchelewa kukamilisha mradi kwa mkandarasi
 
tanzania ni shamba la bibi mtu anayejiita mkandarasi amekula hela na mradi haushi
Kuna miradi imeanza toka 2012 mpaka leo 2017 haijakamilika. Kinachoshangaza zikitolewa tender nyingine, wakandarasi hao hao wasiomaliza kazi ndio wanapewa nyingine. Halafu tunashangaa kwanini hatuendelei?
Tubadilike...Magufuli anajitahidi sana kuamsha uwajibikaji ambao kwa kweli haupo. Nchi ilikuwa nchi ya kitu kidogo kwa kwenda mbele
 
Hulipi wakandarasi kwa muda alafu wamalizeje hizo kazi. Contractual obligations ni two sided.
 
Mkuu keshajua janja yao; kuna makampuni ya ujenzi sana sana ya hawa jamaa wenye macho madogo hubadili mameneja mradi kila mara, kesho unamkuta huyu kesho kutwa ukija ni mwingine, halafu watata sana kwenye kulipa sub-contractors wao.
 
Kuna miradi imeanza toka 2012 mpaka leo 2017 haijakamilika. Kinachoshangaza zikitolewa tender nyingine, wakandarasi hao hao wasiomaliza kazi ndio wanapewa nyingine. Halafu tunashangaa kwanini hatuendelei?
Tubadilike...Magufuli anajitahidi sana kuamsha uwajibikaji ambao kwa kweli haupo. Nchi ilikuwa nchi ya kitu kidogo kwa kwenda mbele
Kama hawalipwi kwa wakati kazi itaishaje?
Hili bila kujua pande zote za shilingi ngumu kuchangia.
Uwanja wa ndege dar hauishu kwa sababu serikali hadi ikabe watu fine za barabrani ndio ipeleke mafungu.,wanapeleka leo hela kiduchu, kesho wanafanya ziara na mikwara kibao hela zipo ujenzi uende kwa kasi.
Tumerogwa.
 
Mkuu keshajua janja yao; kuna makampuni ya ujenzi sana sana ya hawa jamaa wenye macho madogo hubadili mameneja mradi kila mara, kesho unamkuta huyu kesho kutwa ukija ni mwingine, halafu watata sana kwenye kulipa sub-contractors wao.
Sasa atakaenyang'anywa passport ni nani kwa mtazamo wa ukubwa wa kampuni?
 
Mkuu keshajua janja yao; kuna makampuni ya ujenzi sana sana ya hawa jamaa wenye macho madogo hubadili mameneja mradi kila mara, kesho unamkuta huyu kesho kutwa ukija ni mwingine, halafu watata sana kwenye kulipa sub-contractors wao.
Ni kweli uwajibikaji ni muhimu,haiwezekani watu wawe wanachukua hela za wavuja jasho kujenga miradi ambayo haikamiliki miaka nenda rudi.Nidhamu ya kazi iko wapi?
 
Back
Top Bottom