Lindeni makandarasi wa ndani - Mwakyembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lindeni makandarasi wa ndani - Mwakyembe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 22, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,604
  Trophy Points: 280
  Lindeni makandarasi wa ndani - Mwakyembe Friday, 21 January 2011 20:45

  Elizabeth Ernest
  WAKALA wa Ujenzi wa barabara nchini (TANROADS) , imetakiwa kuepuka masharti ya zabuni za ujenzi yenye mwelekeo bayana wa kuwaengua makandarasi wa ndani.

  Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Harrison Mwakyembe jana Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa Chama cha Makandarasi Tanzania (CATA), ambapo alijibu malalamiko makandarasi hao kwamba karibu 60% ya miradi yote ya ujenzi hufanywa na Makandarasi wa nje.

  Pia aliwataka Tanroads kuangalia upya viwango vya zabuni wanavyotoa wakati wa kutangaza tenda ili kuwapa fursa makandarasi wa ndani kushiriki nafasi hiyo.

  “Sina tatizo na miradi inayotekelezwa na nchini kwa ufadhili wa wabia wetu wa maendeleo, ila tatizon langu ni miradi inayogharamiwa na serikali ya Tanzania,”alisema na kuongeza:

  “Haingii akilini kwa miradi hii inayogharamiwa na serikali kutokana na kodi ya wananchi kuendelea kutekelezwa na makandarasi wa nje kwa asilimia 100 bila ushiriki wa makandarasi wa ndani kutokana na sababu kuu tatu”.

  Alizitaja sababu hizo ni kutokana na udhaifu wa sarafu ya Tanzania na kwamba mara zote malipo ya makandarasi wa nje hufanyiwa kwa dola badala ya shilingi ya Kitanzania na hivyo malipo yao huwa ni fedha nyingi zaidi na kufanya ujenzi wa barabara nchini kuwa ghali.

  Pia mikataba ya Tanzania haiwafungi makandarasi wa nje kuwekeza tunayowalipa nchini na kwamba sehemu kubwa ya malipo yanayofanywa huneemesha uchumi wa nchi nyingine pamoja na kutoa fursa kwa wageni badala ya wananchi wetu.

  “Kwakuwa mchakato wa zabuni ni zoezi la kitaalam, makandarasi wa ndani wajitahidi kuajiri watu wenye ujuzi katika masuala ya manunuzi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya ushindani,” alisema.

  Katika risala yake Mwenyekiti wa CATA, Mhandisi Lawrence Mwakyambiki alisema anasikitika kuwa bado kuna idara au Taasisi za serikali ambazo hupendelea kwa mazoea kutoa kazi za ujenzi zilizo chini ya bilioni 20 kwa kampuni za nje bila sababu za msingi wakati makandarasi wazalendo wana uwezo wa kuzifanya.

  Pia alisema miradi mingi ya serikali imekuwa haifanyiwi matayarisho ya kutosha na washauri pamoja na wataalamu wa serikali pamoja na kutoipa umuhimu unaostahili kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi wenyewe.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,604
  Trophy Points: 280
  Mbinu za kusaidia makandarasi wa ndani ni hizi hapa zifuatazo:-

  a) Iwepo Benki ya kukopesha makandarasi wa ndani bila ya riba............................na benki hiyo iwe na mtaji mkubwa wa kuweza kuwadhamini kwa kazi isiyozidi moja...............................

  b) TANROADS wawe na mtandao wa kuhakikisha makandarasi ambao hawajamaliza kazi hawapewi kazi nyingine....kwa lugha nyingine asiwepo mkandarasi mwenye zaidi ya kazi moja ya TANROADS kwa wakati mmoja.................................................

  c) Kazi zinazotolewa ziheshimu madaraja ya makandarasi..........................ukitaka kuzimaliza kampuni za kizalendo basi TANROADS waendelee kuruhusu makampuni ya madaraja ya juu kuyanyng'anya yale ya madaraja ya chini kazi...........................kampuni ndogo kamwe hazitakuwa ili kulisaidia soko la ujenzi kuleta ushindani ambao ndiyo muhimi katika kuteremsha bei za kazi za ujenzi....................

  d) Ziwepo sheria ambazo zinalazimisha kazi moja kugawanywa vipande vipande ili kuongeza ushindani kwa kazi ambazo zinatokana na mapato yetu ya humu humu ndani..............................................................

  Mheshimiwa Mwakyembe hizi ni baadhi tu ya hatua ambazo zitaisaidia serikali kuwajenga makandarasi wa ndani na hivyo kuinua uchumi wa taifa hili..................................
   
 3. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Nalazimika kumpa Big Up Naibu Waziri Dr H Mwakyembe kwa uzalendo wake wa kutetea maslahi ya Makandarasi wazalendo nchini.
  Sekta ya ujenzi imeharibiwa sana na mdudu rushwa, hasa pale TANROADS.
  Kwa kadri ya duru zangu, kazi hazitoki pale mpaka Mkandarasi atoe % ya mapato yake.
  Dr Magufuli na Dr Mwakyembe wanatia moyo kwa misimamo yao yenye lengo lililo wazi.
   
Loading...