Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,232
- 3,334
Unakuta kijana msomi ana kazi yake safi inayompa kipato, ameoa binti msomi mwenzake ambae hana kazi. Cha ajabu utakuta binti amekaa miaka mitatu bila kazi akisubiri ajira. Lakini wakati huo huo mume wake hakosi milioni 4 ambazo anaweza akampa mkewe wakafanya biashara na kujiingizia kipato. Yaani msomi anaona bora asubiri ajira ya take home laki 4 kuliko kufanya biashara ya faida ya laki 6 kwa mwezi. Utadhani pesa itokanayo na biashara haina thamani.