Linaniumiza kichwa

Linaniumiza kichwa

Binti.com natamani nione ushauri wako maana siku hizi umekua kimya sana.

Back to topic
Mkuu kabiriga inakupasa ukutane na mpenzi wako na kuyazungumza yote hayo bila kumficha hata chembe, haina haja yakumfumbia macho wakati unaona kabisa anakokupeleka sipo kabisa.
 
Alijisahau akachanganya madawa hakujua anatengeneza sumu.
 
Ongea na mpenzi wako na ikiwezekana yawe ni maongezi ya ana kwa ana.
Jaribu kumuuliza kama ana "kidumu", ila mwanzoni jifanye kama haujui chochote.
Ukiona anapinga basi toa shahidi zako na umuhakikishie kuwa unajua mchezo wake.
Halafu baada ya hapo mueleze kuwa umeamua kuachana naye na humuhitaji tena...then uangalie reaction yake.
atamwambia nenda babu weee ukisusa wenzio wala kila la kheri
 
Nina mchumba wangu (wakike) ni mwanafunzi wa chuo kikuu kimojawapo hapa nchini.Siku moja nilipata ujumbe kwenye simu yangu kutoka kwenye namba ngeni ukisomeka hivi ("Hapa huna mchumba jamaa wana mega kama nini") sikuelewa nini maana yake.Baada ya week kama mbili hivi siku moja nilimpigia simu mchumba wangu saa 3 na nusu usiku,tukaongea yetu na kisha tukatakiana usiku mwema .lakini sikukata simu yangu na sikuitoa sikioni nae pia hakukata nadhani kwa vile nilipiga mimi alidhani nitakata mimi.kisha baadae kidogo nikaanza kusikia mazungumuzo kati yake na mtu mwingine sauti ya kiume,kati ya mengine mengi niliyo yasikia ni mazungumuzo ya mahaba kati ya watu hao,siku hiyo ilikuwa jmosi ,kesho yake saa nane mchana nilipokea ujumbe kutoka kwa mchumba wangu analalamika kwanini nimechelewa kufika sehemu furani,sikuelewa nikitu gani kinaendelea kwani mimi nipo mbali nae na hatukuwa na miadi yeyote ya kukutana nae sehemu ile,kisha baadae kama dk 10 akatuma ujumbe mwingine akisema yeye amefika akiniuliza nipo wapi?nikazidi kushangaa sikujibu .nikapiga moyo konde nikangoja .kisha dk 30 baadae akatuma ujumbe wa kuniomba radhi kwani ujumbe uliokuja kwangu alikuwa anamtumia rafiki yake na kwakuwa namba yangu ya simu ndo ameizoea sana ameshtukia ameisha nitumia mimi.sikumjibu kwa wakati huo kisha nikaanza kuunganisha matukio.kichwa kinaumia nichukue uamuzi gani kwani nimeaanza kupoteza imani nae.Ushahuri wenu jamani

pole sana ila mwache huyo dada mara moja,uwe na uamuzi wa kiume.
 
atamwambia nenda babu weee ukisusa wenzio wala kila la kheri

Kwangu mimi hilo ni jambo jema kuliko kuwa na mtu halafu wengine wanamtafuna kwa raha zao...ya nini kushika pembe wakati chuchu wazinyonya wengine!!!
 
kwanini usimpigie simu huyo aliyekutumia sms kukuambia huna demu hapo?maana waswas wako umeanzia hapo ulipopata hiyo msg, inawezekana ni wrong number.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom