Linaniuma sana nisaidieni jamani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Linaniuma sana nisaidieni jamani.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Fasta fasta, Apr 1, 2011.

 1. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Ndugu zangu wanajf. Ninapenda kuwasilimia wote mabibi na mabwana. Nimefurahishwa sana na ushauri na mawazo manayotoa kwa kweli ni ya kujenga sio kubomoa. Shukrani.

  Mimi ni kijana ambae nilibahatuka kumpenda binti mmoja na nilibahatika kuzaa nae mtoto mmoja tukiwa tunaishi nae pamoja kama miaka mitatu. Lakini baada ya kupata mtoto nikamwona bibie anabadilika kwa sababu dada zake wanauwezo. Mimi nilivumilia mambo mengi sana kiasi kwamba ilifikia kipindi ikawa tunasemana chumbani na kuombana msamaha yanaisha. Mimi mwenzio ninaumia kumbe yeye anapata raha tu na nikimuuliza hivi anajisikiaje labda anavyuniona kama ananipenda anajibu kama chizi ninakupenda kumbe ananing’ong’a huku nyuma. Haya mambo ya simu ni historia ndefu sana kwangu na yeye kuhusu kijana mmoja tulie kuwa tumepanga nae nyumba moja. Na hili la simu nimelifuma mwenyewe live bila kuambiwa na mtu yeyote. Kama ni chakula cha mtoto alikuwa anapata kila siku isipokuwa siku ambazo anakua. Lakini tamaa inaendelea kumzidi. Ninasikia anachukuliwa na rafiki yangu mzee ambaye alifiwa na mke wakati sija toka huko Tz. Na mimi ninamwita ni baba kwa sababu mtu akisha kuzidi miaka 30 ni lazima umuheshimu. Na nilimweshimu kwa sababu alikuwa ni jirani yangu. Sina ukoo nae wala sio kabila langu.
  Ubinafsi:
  1. Amefuga mifugo kwa mtu bila kuniambia, na nimemuuliza akasema ni kweli alikuwa nazo hata kabla sijatoka huko na hela alipata kwa dada yake.
  2. Amejenga nyumba bila kuniambia walipomuuliza wenzake ya kuwa baba watoto anajua alisema hataki nijue ni nyumba yake atapangisha kwa sababu anajua nitajenga nyumba na tutakaa. Baada ya kujua nimeshajua ndio akaaza kuniomba hela za kuchimba choo na kuanza kunieleza ameamua kujenga nyumba sijuii sababu haziishi. Nilipo muuliza amepata wapi hela anajitetea ametumia hela nilizokuwa ninampa za matumizi. Kweli nilishikwa na hasira nikampeleka mwanagu boding japo ni mdogo wa miaka 7.
  3. Ana majibu kama kuku ambaye anaharisha.
  4. Hapendi kusikia ninawasaidi ndugu zangu kabisa ilifikia kipindi kabla sijaja huku kawakejeli wazazi wangu, nikimwomba embu wasaidie kitu fulani anasema si uwasaidie wewe si wazazi wako, anasema sijamuowa kwa ajili wa wazazi au ndugu. Lakini ninashukuru mungu hakuna mtu yeyote anajua adha ninayoipata, sija wahikuwaambia hata wazazi. Ninasema hivyo kwa sababu anzia nimetoka huko mama yangu alikuwa anaumwa lakini alifika nyumbani kwao akawa anajificha mpaka akaondoka hakuwasalimia wazazi wangu kabisa.
  Ninaomba ushauri ndugu zangu nifanye nini? Na mimi ndio nimemaliza masomo ninataka kurudi nyumbani, nianzie wapi maisha? Dada zangu wote wameshaolewa nimebaki na mdogo wangu wa kiume ambaye yupo sekondari.
   
 2. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Pole sand ndugu yetu. Mimi nitakushauri kama ifuatavyo; kwanza kabisa mwenza wako siyo mwaminifu; hili ni tatizo kubwa sana ambalo nafikiri liko juu ya uwezo wako. Huyu mtu bila maombi hawezi badilika kamwe ni kitu kiko damuni. 2. Kajenga nyumba bila kukwambia, hiyo inaashiria kwamba anahitaji nafasi ya kuishi maisha yake mwenyewe bila wewe. 3. Ana jeuri kwa umalaya wake, inawezekana wewe unachompa ni kidogo kwa kutumia mwili wake anaongezea pale ulipoishia wewe. 4. hana mapenzi na ndugu zako, ubinafsi mbaya sana ambao ki ukweli wale wote wenye roho hizo na wako kwenye ndoa huwa hawabadiliki. Mazingira waliyokulia ni ya kimaskini sana kiasi kwamba kila kitu kwake ni lulu, though kuna wengine ni tajiri wa mali na maskini wa roho.

  Mimi nakushauri mwache tu aende zake, omba mtoto wako akue katiika mazingira mazuri, Mungu atakupa mke mwema. Kuanza maisha peke yako sidhani kama ni kitu kigumu unless wewe ukifanye kuwa kigumu. Make sure una muda na mtoto wako, usiingie kwenye mambo yanaitwa mapenzi kabla ya hujajua hata huyo utakayekuwa nae kama atampenda mwanao. Siku hizi mambo ni magumu, mtu anakubali kumpenda mwanao kwa sababu anataka aingie kweye ndoa akishaingia vimbwanga vinaanza. Simama katika imani huku ukiomba mungu kukupa hekima na busara za kulea mwanao.
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  mwache aendlee na maisha yke cz hakupendi. Toka lini kwnye mapnz kukawa na cr? Hzo psa za ma2miz kias gn mpk ajenge nymb? Na kw nn ackshrikishe?
   
 4. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mkuu pole sana na adha inayokupata. Lakini ningeomba ujaribu kuwa na msimamo wako maana mi nafikiri huenda hata jina lako linakugharimu kwa kufanya mambo ya maisha "fasta fasta". Kitu muhimu sana katika maamuzi ni kile wazungu walisema "Peace of Mind". Na kosa kubwa linaloweza kumsumbua na hata kumgharimu mtu maishani mwake katika swala la mapenzi ni "Kupenda bila Kupendwa".Cha msingi kaa chini na ujaribu kuonesha kama unaweza kuamua.... Vinginevyo, kubaliana na hali hiyo na uwashirikishe nduguzo ili nao wajue umezidiwa....

  I will come back soon...
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  i see !
   
 6. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,468
  Likes Received: 3,739
  Trophy Points: 280
  Umeishi nae kwa muda wa miaka 3 hujaweka msimamo wa kufunga nae ndoa, ndio maana ameamua kufanya mambo yake bila kukushirikisha
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Achana nae hakufai huyo...
   
 8. v

  vegule Senior Member

  #8
  Apr 1, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo mzee unasubiri hadi akuharishie? duh kweli wanaume mna uvumilivu!!
   
 9. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  pole!! hili ndilo langu neno
   
 10. m

  mbweta JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 600
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Bado mapema unaweza anza upya na kuachana nae kuliko umvumilie mtakuja achana kipind ambacho ni too late na itakuchukua mda kugain control.
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Divorce divorce..................
   
 12. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  FF huyu mwanamke hakufai kabisa na uking'ang'ania kuwa karibu naye utaishia kwenye foleni kwa babu Loliondo.Mkimbie fasta fasta!
   
 13. e

  ejogo JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2011
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Duh! pole sana! Nakushauri lala mbele!
   
 14. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Ilikuwa tufunge ndoa kanisani 2006 lakini aliyetibua mambo yote ni huyo kijana tulipanga nae nyumba moja. Ikabidi niwaombe wazazi wasubiri mpaka nitakapo rudi masomoni na kuangalia watamalizia wapi mechi yao. Kwa sababu ilinibidi nimweleze yule kijana lakini alikataa nikamwonyesha ushahidi wote niliokuwa nao. Baada ya kuona hivyo alihama pale akahamia kwa ndugu zake na sasa hivi ninasikia ameoa.
   
 15. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2011
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Aisee...mambo mengine jamani

  huyo ni wa kuachana naye tu manake heshima na uaminifu hakuna...sioni sababu ya kuwa na ndoa hapo...
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  daa mkuu fasta shukuru Mungu bado unaishi naye kama mchumba wako(Kidini) kama umegundua hayo mapema mkuuu usifunge naye ndoa kabisaa, kuvunja uchumba si zambi!
   
 17. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #17
  Apr 2, 2011
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  pole sana, umefunga ndoa? kama umefunga ndoa vumilia, lakini kama hujafunga ndoa, hapo huna mke, tafuta mwingine.....atakuja akuchinje ukizipata huyo ili arithi..ametoka wapi kwanza, machame au mkuu?
   
 18. Mayasa

  Mayasa JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 587
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hafai kuwa mke. Kwanza sio mwaminifu, pili ni m-binafsi. Anapoamua kufanya maendeleo bila kukushirikisha ni wazi kabisa hana future na wewe. Achana nae mapema kabla hujajuta mbele ya safari..
   
 19. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #19
  Apr 2, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
   
 20. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  pole mshkaji wangu
  pole kaka
  uyo si mie
  1. si mwaminifu
  2.mchoyo
  3.hana huruma
  4.akili zake /upeo mfup sana
  6.ana uchu na mali
  8.han ukike

  maoni;
  kimbia
  tafuta anayekufaa km mke ,kuzaa na mtu si lazim awe mke wako
  take ya time thk,swallow pain n u wl move on sweetie pole sana chalii angu!
   
Loading...