Linahitajika Guta au Suzuki Carry kunusuru biashara yangu

Jul 13, 2019
51
93
Rejea hiyo Subject hapo juu. Sina nguvu yakununua vipya, hivyo nataka used chenye afya. Natambua na kuheshimu Madalali ila kwenye hili ninahitaji wamiliki.

Juzi dalali kaniambia Carry mil3.7. Nikachukua namba za usajili nikaomba Query zakikodi au Customs (If any), huko nikapata namba ya mmiliki, kumuuliza bei akasema mil3.0 na maongezi yapo (Hapa madalali wataanza kuficha plates # ili tusiwapate wamiliki directly). Sikuweza kuclose hii deal kwa sababu nyingine

Kwanini nataka Guta au Carry
Niliwahi kuleta uzi wa Nataka kuiona nguvu ya milioni 2 kwenye biashara mpya.
Ziliwekwa shauri nyingi za faida ingawa mawazo HASI hayakukosekana(Siunajua tena watanzania)

Sasa iko hivi: Mrejesho
Nilifungua Car Wash maeneo flani, nikapata Changamoto kadhaa, nikafunga. Tar 8 Dec, 2020 nikafungua nyingine, mahali pengine kabisa.

Sitaki kuweka specifics nyingi lakini nilihamia mahali amboko maji ni ya chumvi kali sana, so nalazimika kununua dumu sh 400 kwa maji ninayotumia. Mtu anaeleta maji (kwa guta), namlipa kwa bili.

Baada yakufanya kazi siku 6 za mwanzo nilikua nimeaccumulate 121,000/=, bili ya maji ilikua 102,000/= (Faida 19,000/=)
Mwendo ndo umekua huo wakumtajirisha mleta maji.
Hata jana niliamua kuhesabu hela niliyonayo tangu nilipolipa bili yamwisho, nimekuta nimetumia maji ya sh 56,400/=, faida ikiwa sh 11,600/=

wanaotuuzia maji wananunua sh 50/= mpaka 30/= kwa dumu.
Nafahamu Rizki ni kugawana ila ninahitaji kupunguza gharama za maji.
Hivyo: Ninahitaji usafiri wakuweza kufata maji kwa urahisi
Simu: 0789361508
 
Hivi mfano ukiwa na madumu. Kukodi carry na kuyabeba mwenyewe inaweza kuwa inakost shingapi kukodi carry kwa safari moja na unaweza pakia madumu mangapi umejaribu kupiga hesabu? Wakati ukisubiri kupata hiyo toyo au carry.
 
Niliwahi kukodi Guta, nikapakia Tank moja nikafata maji. Nilisave 4,500/=, Sio haba ila bado sio Significant kama nikiwa na guta langu. Kwa wastani guta dogo linabeba dumu 30-35.

Pia hapo niliendesha guta mwenyewe, nikapakia maji mwenyewe. Akienda mwingine zoezi linacost zaidi.
 
Kuna jamaa anauza guta mkuu ubaoni kaanzia 2.5m lakini naamini atashuka ukiweza ikague pia anazo mbili anaitoa moja nicheki 0763542515 nikuunganishe nae yupo mbezi
 
Maybe it's time to move again.

Anza kutafuta location upya.
1. Pamoja na gharama zote hizi siwezi kuhama kwasababu location ilipo car wash ni location bora kuliko zote kwa eneo hili. Nikipunguza gharama za maji, biashara itanilipa sana.

2. Siwezi kuhama kwasababu mahali nilipo ninatumika ofisi fulani. Labda mpaka mwaka huu uishe.
 
Vipi unaweza leta hesabu? Mfano mtu akikununulia jipya kabisa.

Hesabu ni 20,000
Mkuu ofa yako ni ngumu kidogo.
Guta hili nataka lifanye kazi yakubeba maji tuu.. hivyo hesabu yako itakua inatoka kwenye hesabu yakuosha magari. Hii itaniumiza.

Ila kama utanipa kwa "Mkataba" usioumiza nitakubali ofa yako. Baada ya mkataba litanifaa sana.

Nakubali kufanya mazungumzo.
 
Ninalo Guta Nilimpa Dereva kama miezi Sita hakuleta Pesa aliliharibu kiasi nikamtumia pesa akatengeneza but siku ya kulirejesha akasema cable imekatika nimtumie pesa nikaona Jau... So Kama Una Milion nakuuzia kama lilivyo Kodi ya Mapato utalipia Deni ilikuwa inaishia mwezi wa 9 Sijalilipia Njoo na pesa nikukandamize nalo... uokoe Biashara yako Guta lipo Bomba Zile TOYO za Mwanzo kabisa Engine yake ni Kapoor.
 
MPE kijana wako akishindwa hapo makubaliano
 
Ninalo Guta Nilimpa Dereva kama miezi Sita hakuleta Pesa aliliharibu kiasi nikamtumia pesa akatengeneza but siku ya kulirejesha akasema cable imekatika nimtumie pesa nikaona Jau... So Kama Una Milion nakuuzia kama lilivyo Kodi ya Mapato utalipia Deni ilikuwa inaishia mwezi wa 9 Sijalilipia Njoo na pesa nikukandamize nalo... uokoe Biashara yako Guta lipo Bomba Zile TOYO za Mwanzo kabisa Engine yake ni Kapoor.
Mkuu nimependa umekua muwazi kuhusu chombo, mpaka mambo ya kodi. Mwingine hapo anakuacha ukafe nalo, siku unaenda kufanya transfer ya umiliki ndo unakutana na fine imesimama kwelikweli.

Mkuu nimeweka namba yangu hapo juu, au kama hautojali unitumie namba yako kwa namna yoyote ile, mimi nitakutafuta.
 
Utanitafuta au Unataka kununua? eleweka Meeen...!
 
Back
Top Bottom