Limbwata lina shida gani sasa?

Limbwata lina shida gani sasa?

Babumawe

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2014
Posts
2,585
Reaction score
2,670
Hivi jamani mi sijaona tatizo la limbwata, kwa sababu inavyosemekana unaekewa ili umpende mkeo sasa hapo shida nini sindio inavyopaswa umpende mkeo, mi sioni tatizo kama ambavyo inavyozungumziwa.

Kwanini asiende kumuwekea John au khamis au James au issa aje kukuwekea wewe si kwakuwa anakupenda basi inabidi nawe umpende

NAKARIBISHA WENYE MTAZAMO TOFAUTI
 
Unajua linakotoka limbwata na linachofanya utaelewa kwa nini jamii inaipiga vita kwa mikono yote miwili
 
Mkuuu penzi la limbwata sio penzi ni utumwa tu utalichoka
 
Hivi ni kweli kuna baadhi ya Limbwata unawekewa nywele za sehemu za siri za mwanamke kwenye chakula?

Nauliza tu
 
🤣🤣🤣🤣 Inabidi nicheke tu 😆😆
 
Kwa tetesi ninazosikiaga ni nyama inawekwa kwenye papuchi siku saba na mitishamba baadhi ndio unalishwa sasa ndio unakua huambiwi husikii yaana akipigiwa na hawara yake we ndio unampelekea simu anaongea mbele yako na hukoromi.

Akichelewa kurudi anakuta umedeki nyumba,umeosha vyombo na watoto umewaogesha na kuwalaza bila kusahau kumuachia chakula na akirudi huwezi kuhoji lolote zaidi we ndio utaomba msamaha kwa kupitiwa usingizi umechelewa kumfungulia.

Kali kuliko zote akikuwekea la kukumiliki usipatane na wanawake wengine ile dawa haichagui inakufanya usiwe karibu na wanaume pia ina maana wafanyakazi au wafanyabiashara wenzako inakuweka mbali ndio kuharibu kazi hata ndugu huwaelewi kasoro yeye tuu.
 
Limbwata hasaraa kuubwa mkuu ni kuleta umaskini ukishapewa limbwata kazi au biashara hutapenda kufanya utataka ukae nyumbani tu unazani kazi utakuwa nayo au biashara itaexist.
 
Mkuu limbwata anayekulisha hakupendi maana utayarishaji wake tu ni mambo mbaya.

Na kwann alazimishe upendo??? Mara nyingi akikupiga limbwata Kuna kitu anataka ama anataka kukusumbua tu

Kwann tusiwalaumu wanaopendana kwamba ni limbwata tunawalaumu wanaofanyiwa ujinga ujinga
 
Back
Top Bottom