Limbwata la gundi na kamba

Limbwata la gundi na kamba

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,153
Reaction score
829,100
Niko kijijini kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka lakini pia nikiendelea kutafiti maarifa mapya na utaalam wa nguvu za giza, ushirikina na ulozi kwa matumizi chanya ya kilinge... Nia ikiwa ni kuwasaidia wahitaji.

Hizi habari za malimbwata kwa ajili ya kumshika mpenzi, mke au mume... Na wengine huenda mbali zaidi... Kwa ajili ya kumshika mwajiri au boss si ngeni kabisa masikioni mwetu... Na malimbwata maarufu yakiwa ni kwa kutumia vyakula na vinywaji.

Kuna hili limbwata baya zaidi.. Limbwata la kutiwa gundi mdomoni au kufungwa kamba.. La kutiwa gundi mdomoni hilo sahau kutongoza nje ama kuwa na kibezi mbele ya mwenza wako... Hapa mhitaji akifika kwa mganga hupewa kinyago chenye umbo la kiume na gundi ya maji au plasta.. Mhusika huelekezwa kukitia gundi mdomoni ama kukiziba na plasta huku akinuia kwa kutaja jina la mtu wake

Ukiachana na hilo la gundi kuna hili la kamba.. Kuna kamba kama za aina tatu hivi
Kamba laini
Kamba ngumu
Kamba ngumu na nzito

Aina ya kamba hutegemea na uimara kiroho wa mhusika anayetaka kufanyiwa... Mhitaji akifika kwa mganga atapewa kinyago chenye umbo la kiume na kamba husika.. Kamba hiyo atatakiwa aifunge shingoni, au miguuni au mikononi... Lakini pia inaweza kufungwa kote kwa pamoja huku akinuia

Baada ya hapo aliyefungwa hatakuwa na sauti tena kwenye lolote.. Atakuwa ni mtu wa kuamrishwa na kufuata maelekezo tuu... Utaburuta na kuburuza utakavyo.

Hili la kamba hutumika pia kufunga sehemu za siri za jinsia zote... Mwanamke akifungwa ndoa inaweza hata kusambaratika kwakuwa anakuwa hana hamu tena. Akifungwa mwanaume hupata ukhanithi.
Vikambakamba vipini pini na vigundigundi kwenye mapochi sio vitu vizuri sana

.
VyIdPMj.jpeg
the-crone-found-in-a-new-york-cave-is-cursed.jpeg

Jr
 
Jamaniiii hili ata kuwa kafanyiwa mtu wangu wa karibu sana! Hasemi kitu kwa mkewe ana achwa nyumbani mke aba rudi usiku wa manane kalewa chakari na ana fungua gate! Ana achiwa mtoto wife ngomani hukooo! Ndugu tume baki kuduwaa! Ukijaribu kuongea ana kukasirikia
 
Ni mpaka agutuke na kufunguliwa ndio ataona ukweli

Ndugu wote wame kaa kando mke kavurugana nao! Je bila kufunguliwa ata kuja kurudi kawaida au ndiyo basi tena? Yaani amekuwa kama ana ogopa ndugu haji hata misibani na cm hapokei! Ni mimi tuu ndiyo naelewana kiasi na huyo bibie! Ila siyo mke wa kwanza alimtoa mwenzie! Kamfanya baba mpka ana mkataa mwanae ambaye ame mkuta huyo mama! Juzi graduu ya mtoto ana maliza chuo mzee hakwenda na cm kazima kabisa! Yaani mambo ni mengi haya ni baadhi!
 
Kila lenye mwanzo halikosi mwisho.. Hata hilo litafika mwisho japo linaweza kuchelewa na huyo mama atakuwa na mwisho mbaya kama kweli anayafanya hayo

Back
Top Bottom