Likizo ya uzazi inafuta likizo ya kawaida ya mwaka?

Kibuja

JF-Expert Member
Aug 12, 2009
510
90
Wana JF mliobobea katika sheria za kazi. Hivi nikichukua likizo ya uzazi ya siku 84 sitakuwa na haki ya kuchukua likizo yangu ya mwaka ya siku 28? nisaidieni
 
ukitaka chukua likizo yako ya siku 28 kabla ya likizo ya uzazi. hapo bosi atachemsha.

macinkus
 
unaamua mwenyewe uchukue lini kabla au baada ni chaguo lako ilimradi tu isihesabiwe kwenye likizo ya uzazi
 
Nashukuru wanazuoni wa Sheria maana ofisi nyingine tunanyimwa haki ya likizo kwa kisingizio kuwa ati ukichukua likizo ya uzazi basi inafuta likizo yako ya kawaida. Sijui ni umbumbumbu wa sheria au ni ukandamizaji? jamani ni kweli tutafika?
 
Waliokujibu hawako sahihi. KWANZA LIKIZO YA UZAZI INA PISHANA KWA VIPINDI SI CHINI YA MIAKA MIWILI. ukizaa ndani ya miaka miwili mara mbili utapata likizo ya uzazi moja tu ile iliyotangulia.
ukipata likizo ya uzazi mwaka 2011, mwaka unaofuata kama ulichukua likizo ya kawaida mwaka 2011 hutopata likizo ya kawaida(annual leave) kwa mwaka 2012.
 
Wana JF mliobobea katika sheria za kazi. Hivi nikichukua likizo ya uzazi ya siku 84 sitakuwa na haki ya kuchukua likizo yangu ya mwaka ya siku 28? nisaidieni

Kumbe Kibuja unakaribia kujifungua.,hongera sana
 
Waliokujibu hawako sahihi. KWANZA LIKIZO YA UZAZI INA PISHANA KWA VIPINDI SI CHINI YA MIAKA MIWILI. ukizaa ndani ya miaka miwili mara mbili utapata likizo ya uzazi moja tu ile iliyotangulia.
ukipata likizo ya uzazi mwaka 2011, mwaka unaofuata kama ulichukua likizo ya kawaida mwaka 2011 hutopata likizo ya kawaida(annual leave) kwa mwaka 2012.

Samahani weka majibu yako katika maelezo mepesi, sijapata kitu kabisa hapo.
Ulikusudia kueleza nini?
Ninavyoelewa mimi likizo ya uzazi ni siku 56 plus siku 28 za likizo ya mwaka husika na inatolewa mara moja katika mzunguko wa miaka mitatu.
 
kwa maelezo uliyotoa yaani siku 56 plus 28 inaleta jumla siku 84. Maana yake ni kuwa na likizo ya mwaka huo inahesabiwa. Endapo ulikuwa umeshachukua siku 28 kabla ndani ya mwaka huo inamaanisha utakuwa umechukua likizo ya mwaka mara mbili. Hivyo, mwaka utakaofuata hutopata likizo kwa kuwa ulishachukua siku 28 zilizoleta jumla ya siku 84.
 
Likizo ina mzunguko wake, huo mchanganuo niliokupa unachukuliwa katika ujumla wake ndani ya mzunguko wa mwaka husika. Hakuna room ya kuchukua kwanza siku 28 then uchukue 84 katika mzunguko wa mwaka huo huo.
 
Mie binafisi nilichukua siku 86 za likizo ,baada ya hapo nilirudi kazini na kufanya 2 month baada ya hapo nilichukua likizo yangu ya siku 28 bila tatizo ..
 
Hapana.Mimi napenda kuweka mambo sawa,sheria mpya inaruhusu mfanyakazi kuchukua likizo yake ya uzazi ndani ya mzunguko wa miezi 36 sawa na miaka mitatu,baada ya miaka mitatu kuisha ndio mfanyakazi anaweza kuchukua likizo ya uzazi nyingine,lakini sheria hii mpya pia ina ruhusu mfanyakazi kupewa likizo yake ya mwaka,lakini likizo hiyo haita enda samba samba na likizo ya uzazi.Sheria ya zamani ya kazi ndio ilikuwa inafuta likizo ya mwaka kama mfanyakazi atachukua likizo ya uzazi.Kwa maelezo zaidi kuhusu hizi likizo rejeshea sheria mpya ya ajira na mahusiano kazini na.6/2004
 
Asanteni kwa kutuelimisha kumbe ni wengi tulikuwa hatujui sheria hasa sheria mpya ya 2004. Inavyoonekana hata waajiri wengi awajui ama wanafanya makusudi kutoitambua hii sheria. Mimi nilijifungua mwaka jana na nilikuwa sijachukua likizo yangu ya mwaka. Nilipoomba likizo ya uzazi nikapewa siku 84 na kuambiwa kuwa kwa kuchukua likizo ya uzazi ya siku 84 sitakuwa na haki ya kuchukua llikizo yangu ya mwaka
 
Back
Top Bottom