Ligi ya mpira ikiisha Watanzania huwa wapo serious na siasa. Ligi ikianza kelele za Simba na Yanga zitatumika kuwaleta DP World rasmi

R-K-O

JF-Expert Member
Jun 27, 2023
482
2,138
Kwa sasa Ligi imeisha kumetulia sana, habari za Dpworld zinakita kila kona ndio main talk ya nchi mithiri ya panya anaezurura kila kona pale paka akienda nje kupumzika kidogo.

Hili suala limewekewa pause, linakuja kuplay ligi ikianza hasa kama Yanga na Simba zitakutana hapo ngao ya jamii.

Ndio muda muafaka unaosubiriwa kuwachomekea waarabu waje waanze shughuli zao huku watu wakiwa wamelala na viatu kwa timu kufungwa ama kuwa na furaha kwa timu kushinda.
 
Kwa sasa Ligi imeisha kumetulia sana, habari za Dpworld zinakita kila kona ndio main talk ya nchi mithiri ya panya anaezurura kila kona pale paka akienda nje kupumzika kidogo...
Mkuu R.K.O. Wewe ndiyo umewachambua Watanzania sawa sawa. Na ulichokisema ndicho watawala wanachokijua na kukikitumia kuwatoa Watanzania katika kufikiria na kuchambua mambo ya maana na ya msingi yanayohusu maisha yao. Formula ni moja tu .

Wape Simba na Yanga. Mwaga mamilioni kwa mojawapo ya hizo timu. Hutawasikia wa Tz wakilalamika kuhuzu ugumu wa maisha,tozo bei ya sukari nk,nk.
 
Back
Top Bottom