Life Begins at 40, How Old Are You Friend?

Life Begins at 40, How Old Are You Friend?

Huo ni msemo wanao utumia waingereza wakimaanisha maisha yako, ijapokuwa yanaanza toka milele iliyopita na toka umeumbwa na toka umeanza kukua n.k bado maisha halisi yataanza rasmi siku ukitimiza miaka 40.

Hapo kama nauli ya daladala, ada, chakula, kodi ya nyumba, n.k basi ndo utaanza kuelewa maana ya muda uliokuwa unautumia WHATSAPP, FACEBOOK kulike picha za ajabu na story zisizokupeleka popote.

Ulipokuwa mdogo lisema, nikiwa mkubwa nitakuwa na gari na nyumba nzuri,wazazi wangu wataishi hivi na vile. Je sasa unavyo hivo vitu. May be yes, but my be no. Km haijatokea je bado hujawa mkubwa.

Basi kama ni mkubwa ujue kuna kitu hujafanya. Utasema tena nikifika miaka 40 nataka niwe na hiki na kile watoto wangu wasome inter schoools. Usishangae kufika 40 bado hujaajiriwa au kuajiriwa kila kukicha ni JamiiForums kwenye uzi wa KAZI NA TENDA. Kazi nyingi no bright future. Just existing and not living.

Hapo ndo unawaza kufuga kuku wa nyama Kibamba na Mabwepande kwenye kiwanja chako cha MIGUU 12 kwa 15 ambacho hakijapimwa. Wenzako wa umri wako hapo wameanzisha biashara in Turkey.

Wanamiliki Apartment UK, France na wanaenda kula The Ritz. Wanasomesha watoto wao finest schools wewe wakwako wakati huo amekosa nafasi Jitegemee na Makongo wameenda Mama Salma school Tandale huku wakipanda daladala nne kwenda na kurudi huku wakitukanwa na makondakta eti wakusoma usikalie siti.

Wenzako at 40s wanasidia wasio na uwezo katika jamii wewe ndo kwanza ukipokea simu kutoka kijijni mzazi anashida kiduchu unazima simu. Wenzako in their 40s wakisikia kuna tetemeko la aridhi na baa la njaa wanachangia 10M kimyakimya, wewe ukitoa elfu hamsini unamtafuta ripota mmoja wa habari ukurushe hewani.

Wakati wenzako wanapambana kimaisha wewe ulikuwa unashinda Facebook na whatsapp kuongelea UKUTA, KESI YA MILIONI SABA KWA DAKIKA 1, sijui kufunja viti uwanja wa taifa. Unajua Diamond kaimba vizuri na Raymond akimshirikisha Hamisa. Mimba ya Sepetu ni hewa. Zari agombana na mama mkwe.

Wenzako katika umri wa 40 wana exposure ya kutosha. Wewe 40 bado umeajiriwa na mchana unakula kwa mama lishe, wakati wenzako walishaacha kazi wanatembelea nchi mbalimbali duniani. Zitaje uwezavyo.

Wewe hata Bujumbura au Zanzibar hujawahi kufika. Kila kukicha MBEZI POSTA, TEGETA KARIAKOO ndo ruti yako mfululizo kwa miaka 20 eti unawatafutia watoto maisha. Eti mimi nina mshahara mzuri nalipwa laki nane ngazi ya shahada bado posho. Huo ni mshahara mzuri kweli.

Then unasubiri kiinua mgongo cha LAPF, NSSF kwa makato ya elfu 55 kwa mwezi ndani ya miaka 30. Utaenda kuinvest wapi na kwa nguvu ipi at 60yrs, tena unafungua duka la chakula ali maarufu kwa Mangi shop. Kwanini hukufungua ukiwa na 30yrs ili uone linalipa au la.

Kisa ulikuwa unafuatilia ratiba zote za mechi za mpira wa kimaitaifa nahuku ukicheza kamali mbaya alimaarufu KUBETI. Ukifuatilia ratiba za matamasha ya fiesta na mikutano yote ya kisiasi. Hao unaofuatilia wamo ndani ya kazi yao tena kwenye idara ya propaganda za chama.

Ulikuwa unatumia muda mwingi kufuatilia vichekesho, sijui nani kafulia, nani mjamzito. Kama hujui ndugu hivyo vitu vinagharimu muda wako. Umri wako siyo hesabu ya mwaka, ni sekunde inayozaa dakika na lisaa. Amka kijana. Wasukuma wanasema time is money. Mungu siyo mjinga kukupa umri huu wa ujana. Faidika na ujana kabla ya uzee haujakukuta. Na uzee siyo mzigo wala tusi, ila jiulize utafikaje huko.

LIFE BEGINS AT 40, HOW OLD ARE YOU NOW. Scopioni na Lipumba hawatakusaidia lolote.
Umejitaidi kuchambua sehemu zote vijana wazipendazo lakini hazina tija kwao,40 si mchezo[emoji3] [emoji3]
 
Wachache saana wapo katika nafasi hizo za kimaisha, wengi wao waliandaliwa kuwa hivyo walivyo
 
Roughly 80% of the people above 40 yrs havent achieved anything ,actually they are approaching 60 with nothing achieved !!!! Its a challenge ,
 
Nimepigwa za uso, haki ya Mungu! Nimekuwa mpole ghafla. Nakubali, penye ukweli uongo hujitenga. Aisee sasa labda niapply "It's never too late to mend".
Kwa kujipa moyo nasema "Never say never in life". ONE DAY YES!
Mi nasubiria mtu atangaze niwe Punda wake tu,Get rich or die trying
 
All in all this is not my home.. Am here for some moments then i will leave this selfish world.. Whatever come to me i will thank God for that and no need stretch beyond my ability.. Live without fear of your age coz this is not your permanent home.. Be happy and pray be thankful Lord knows better how and how much will provide to you.... Do your thing legally....
 
Mi nasubiria mtu atangaze niwe Punda wake tu,Get rich or die trying
To die is the promise from your Lord.. Do not cut short... Ridhika muda ni ule ule uwe tajiri utaacha mali na mke au wake wanatumia wengine be gentleman
Tafuta kwa halali na kwa kiasi.. Usitamani pesa, jibrandi pesa ikutamani wewe....
 
Back
Top Bottom