Lifahamu jiji la Geneva nchini Switzerland kwa undani

Habari zenu wakuu, bado lock-down inaendelea huku.

Ukiachana na hilo kuna memba kanituhumu hapa kwamba niko bongo nilitaka kuleta uthibitrisho wa picha ama video lakini baada ya kuona kejeli nimegundua kumbe watu humu wanachukia sana kusoma maandiko ya namna hii nimeamua kuachana na kujibu ule ujinga wa upuuzi kule kwa vile hakuna mtu yeyote niliyemtapeli na kama unahisi siko huku haina haja ya kuumia wewe RELAX TU mkuu maisha yako yaendelee na kama unahisi nagoogle na wewe fanya hivo hupaswi kuumia kwa vitu visivyoumiza na siko hapa kutongoza mtu kwa hiyo mabaharia msipanick maana kuna watu wananitukana mpaka PM kisa pale chini naadika "Geneva -Switzerland" wengine wananiambia nibadilishe ID na matusi juu kisa eti najimwambafai:D :D NAWAELEZA tu nitaendelea kuandika kile ninachokijua mpaka pale lockdown itakapoisha na nianze kuendelea na ratiba zangu, na badala ya kujibu ule upuuzi leo nimeamua kuizungumzia hii Canton(Mkoa) wa Geneva yenyewe kwa mtu mgeni.

Kwa mara ya kwanza ukiwa unafika hapa na ukatua uwanja wa ndege wa GENEVA kama ni mgeni huwezi kupata shida kama unajua lugha vizuri ya kiingereza japo LUGHA ya kifaransa inatumika sana katika jiji hili, pia kuna lugha zingine kama 3 hivi ni official kutumika hapa jijini. Kifaransa kinatumika sana hapa kwa sababu hili jiji lipo karibu na nchi ya ufaransa kwa kiasi kikubwa mfano mji wa Annemasse wa nchini ufaransa kwa train ni kama dk10 tu unakuwa umefika ukitokea katikakati ya mji wa GENEVA na watu wengi wanaofanya kazi nchini GENEVA huishi hapa ili kukimbia ughali wa maisha jijini GENEVA

Ukiwa hapo Airport ambayo ina Terminal 2 ukishuka unaweza kutumia usafiri wa tax au gari la abiria ambao uko nje ya huu uwanja kuelekea katikati ya mji ama ukapande treni ya chini ya Ardhi iliyo karibu na Terminal 2 ya huu uwanja wa ndege, kutoka hapo kwenye kituo cha treni cha Geneva railway station kama ni mgeni nakushauri uende ubalozi wa Tanzania uliopo hapa Geneva mtaa wa Avenue Blanc kwa msaada zaidi ambapo haizidi dk 15 kwa treni inategemea na route au treni uliopanda ama mda usiozidi lisaa limoja kwa basi na kama ukiwa umechelewa umefika usiku shuka kituo kikubwa kabisa cha treni hapa jijini GENEVA cha Cornavin Railway Station hapa utakutana na hotel za bei rahisi tu ambazo hazizidi $300 kwa siku, umbali wa dk kama 8 kwa kutembea kutoka hapo kituoni kuna msululu wa hotel kama four season, Hotel Geneva na House swisss Hotel

Na kwa vile chakula cha hotel ni gharama hupaswi kabisa kula hotelini wewe lipia chumba tu halafu ingia mtaani angalia migahawa ya Milan, Holy Cow, La Favola na La matze upige msosi kwa bei poa kabisa kabla ya kurudi hotel kusinzia

ukichukua Tax kwa CHF 10 tu ukashuka mitaa ya Cornavin karibu na Migros Supermarket ( Hapa tuelewane sizungumzii Migros Supermarket ya Uwanja wa ndege au ile iliyopo kwenye kituo cha treni utakachopanda cha chini ya ardhi) kuna hotel za bei rahisi pia kama Cornavin Hotel Geneva, Swiss Luxury apartment na hotel Century hizi ni baadhi tu zilizo karibu na za bei nafuu ambazo hazitakupa usumbufu kuzipata, na ukifika usiku zaidi ya saa 6 utalazimika kulala hapo uwanjani mpaka kesho yake ndio utaruhusiwa kuendelea na safari


Prabora
Geneva - Switzerland

Chukua hatua stahiki, Corona ipo na ni hatari
Mhh
 
Back
Top Bottom