Lifahamu Gugu chawi

Naomba tuwekee kapicha kake mkuu
 
Kuna UA niliambiwa ukiliotesha nyumbani wachawi hawawezi kufanya yao ila sijui ni UA gani hilo
Ninalo nyumbani mkuu!! Achilia mbali wachawi na wapiga zongo pia ni dawa nzuri pia kwa matatizo mbalimbali kama ya tumbo na kichwa! Wahindi wanajua na kuliheshimu sana jani hilo! Mfano mtoto akizaliwa kwenye familia ya mhindi basi jani hilo hutundikwa mlangoni kwa wiki tatu au zaidi wakiamini kuwa linamwepusha mtoto na mabalaa mengi.
 
Ukiacha Tabia yake ya kushambulia mimea, je matatizo gani mengine ya kiafya yanàyoweza kumpata mkulima kwa kuwepo kwa guguchawii shambani kwake?
Hakuna kama hatakula punje zake
 
Uzungu umetuharibu na kutupofusha na kugandisha ufahamu wetu.... Leo unapozungumzia hizi habari kama hazina majina ya kizungu ama link yake basi inaonekana ni habari ya kiswahili na ya kupuuzwa
 
Ni lile lenye miiba ambalo hutumiwa kwenye Practical sekondari au?
 
mshana Jr, asante kwa kutufahamisha gugu chawi au Striga Hermonthica kwa jina la kitaalamu.

Pamoja na hasara zake za kuangamiza mazao ya chakula na biashara kwa binadamu pia una faida kama mmea dawa. Hutumiwa kutengeneza dawa ya kutibu kisukari, magonjwa ya ngozi, ukoma, vidonda ndugu, homa ya mapafu na manjano, nk, mbali ya kutumiwa na wachawi.

Lakini, faida hizo haziwezi kulinganishwa na hasara yake ya kuangamiza mazao.

Ni gugu ambalo ni gumu sana kuangamizwa kwa kuwa mbegu zake husambazwa kirahisi kwa njia nyingi kama vile upepo, mtiririko wa maji ya mvua, na wanyama.

Njia sahihi ya kuliangamiza gugu hili ni kuling'oa mapema kabla maua hayajaanza kutoa mbegu zilizokomaa.
 
Mkuu mshana jr,
Mbona picha ya kwanza ni tofauti na hii?? Tushike lipi kwani ninavyojua ile picha ya kwanza ndo yenyewe. Angalia rangi ya maua
Ni kweli kabisa Picha ya kwanza ni kipindi cha mvua hapo kila mmea hustawi inapokuja kipindi cha kiangazi gugu chawi hunyonya mimea mingine
angalia hata majani ya rangi ya maua vinatofautiana Lakini ni Specie ile ile
 
Asante sana mwengeso nimeongeza ufahamu hapa ....pamoja na mapungufu yake Lakini linaweza kuwa na faida nyingi kumbe [emoji120] [emoji120] [emoji120] thanks again
 
Asante sana mwengeso nimeongeza ufahamu hapa ....pamoja na mapungufu yake Lakini linaweza kuwa na faida nyingi kumbe [emoji120] [emoji120] [emoji120] thanks again
Tafuta makala ya kitafiti iliyoandikwa na Koua, F.H.M. (2011): Striga hermonthica (Del.) Benth: Phytochemistry and pharmacological properties outline, Journal of Applied Pharmaceutical Science O1(07), pp 01-05
 
Tafuta makala ya kitafiti iliyoandikwa na Koua, F.H.M. (2011): Striga hermonthica (Del.) Benth: Phytochemistry and pharmacological properties outline, Journal of Applied Pharmaceutical Science O1(07), pp 01-05
Leo tafanya hivyo kwakweli, it takes few mbs to gain a very crucial education ili ije iwe msaada kwa wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…