kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,991
- 17,890
Avigdor Lieberman akiri kwamba Israel imeshindwa na harakati ya HAMAS Ukanda wa Ghaza
Jan 10, 2019 15:52 UTC
Waziri wa zamani wa vita wa utawala haramu wa Israel, Avigdor Lieberman sambamba na kukiri kwamba siasa za Tel Aviv mbele ya HAMAS zimefeli, amesema kuwa harakati hiyo ya Kiislamu imepata mafanikio makubwa kama ambavyo imeendelea kubakia imara.
Lieberman ameyasema hayo katika mahojiano na kanali ya 7 ya televisheni ya utawala huo na kuongeza kwamba Israel ilisalimu amri mbele ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS katika vita vya hivi karibuni.
Aidha amezungumzia muqawama wa Palestina dhidi ya Israel na kusema kuwa, wanamapambano hao hawaogopi kitu chochote na kwamba Tel Aviv haina siasa za maana za mustakbali wake katika kukabiliana vilivyo na harakati ya HAMAS.
Amekiri kwamba siasa za utawala huo katika eneo la Ukanda wa Ghaza zinaelekea kufeli. Katika mahojiano hayo, waziri huyo wa zamani wa vita wa utawala wa Kizayuni amesema, katika vita vya siku mbili kati ya Israel na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, Tel Aviv ililazimika kutangaza usitishaji vita siku mbili tu baada ya harakati hiyo kuvurumisha zaidi ya makombora na maroketi 500 upande wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni. "Uvurumishaji wa makombora na maroketi zaidi ya 500 kutoka Ghaza dhidi ya vitongoji vya Israel, ni kufeli kukubwa kwa baraza la mawaziri la Netanyahu." Amesema Avigdor Lieberman.
My take:Hamas wame-advance oneni makombora yao tofauti na mwanzo
Sent using Jamii Forums mobile app