Lie detector test

Lie detector test

Aadilu

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2013
Posts
645
Reaction score
464
Katika Sony Tv inayopatikana katika visimbuzi vya dstv kuna Tv show inaitwa Trisha. Miongoni mwa yanayojadiliwa katika kipindi hicho ni hasa mambo yahusuyo familia kama vile watu kusingiziwa watoto kuwa wa kwao ilhali sio. Usaliti katika ndoa na mambo yanayofanana na hayo.
Kilichonifanya niandike thread hii ni namna wanavyomgundua msaliti wa ndoa au mtu yeyote anayetoa taarifa za uongo. kinachofanyika mtuhumiwa wa kutoa taarifa za uongo anavishwa nyaya kadhaa kifuani mikononi na kichwani na nyaya hizo huingizwa katika kompyuta yenye software maalum yenye uwezo wa kugundua kama kinachosemwa ni uongo au ni kweli "Lie detector software" Hivi utaalam kama huu ukija huku kwetu bongo watu wengi si wataumbuka?Wake za watu, waume za watu, viongozi wanaoomba kura kupitia kampeni zao za kimagumashi si wataaibika au mnalionaje hili Great thinkers?
 
lie detector hukamata watu wa kawaida mtu aliekubuhu huwa haiwezi kumdaka
 
Kinachonishangaza inakuwaje kompyuta ikagundua kwamba sentensi hii ni ya uongo au hii ni ya kweli?
 
Kinachonishangaza inakuwaje kompyuta ikagundua kwamba sentensi hii ni ya uongo au hii ni ya kweli?

wanaangalia mabadiliko ya mwili unapotajiwa kitu. mfano ukitajiwa kitu kibaya ulichofanya moyo huongezeka mapigo hivyo wanajua. ila kama mtu mzoefu kawaida tu
 
Back
Top Bottom