Licha ya Karume kutambuliwa: Kamchezo Uboreshaji Daftari Pemba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Licha ya Karume kutambuliwa: Kamchezo Uboreshaji Daftari Pemba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Nov 11, 2009.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,611
  Trophy Points: 280
  Licha ya Maalim Seif Kumtambua Karume kama rais halali wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar, mambo niliyoyashuhudia hapa Pemba kwenye muendelezo wa zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea kisiwani hapa, kuna kamchezo makini kanaendelea, na kakikamilika kama kalivyo pangwa, CUF itaangukia pua kwa kupoteza baadhi ya majimbo kisiwani Pemba na kuufuta ule msemo kuwa Pemba ni ngome kuu ya CUF.

  Kamchezo kenyewe ni haka...

  1. Sheria ya Uchaguzi Zanzibar, inataka lazima uwe na kitambulisho cha ukaazi ili kuandikishwa kupiga kura.
  2. Ili kupata kitambulusho cha ukaazi, lazima uwe umeishi mahali husika kwa kipindi kisichopungua miezi 36, kwa lugha nyingine, miaka 3 na Sheha ndiye anayetakiwa kulithibitisha hilo.
  3.Sheria hiyo hiyo imetoa mwanya kwa Wafanyakazi, depandants na wajeshi, polisi na vikosi vya SMZ kupewa vitambulisho hivyo muda wowote watakapo kuwepo eneo husika bila kuzingatia kipengele cha miezi 36.
  4. Wakuu wa polisi, majeshi, wafanyakazi na depandants wanahaki ya kupata vitambulisho vya ukaazi bila kuthibitishwa na masheha wala kuzingatia kipengele cha muda gani.
  5. Katika zoezi la uboreshaji daftari unaoendelea sasa, makundi ya watu wengi wao vijana, wanasombwa kwa malori na kupelekwa vituo vya mbali ili kuandikishwa ambako masheha na mawakala wa maeneo husika hawafahamu, ila wamekuja na barua kuwa wao ni watu wa vikosi vya KMKM na wamekuja piga kambi eneo husika.
  6.Sheria ya Uchaguzi Zanzibar unamlazimisha msisimazi kuwaandikisha watu wate atakaotajiwa ni ni polisi au askari wa KMKM hata kama ndio wameingia leo na haimpi mamlaka msimamizi kuuliza idadi halisi ya wajeshi hao, yeye ni kuwapokea tuu na kuwaandikisha, huku sheha ikishuhudia sura mpya asizozijua, mawakala hawawatambui ali muradi hawajavunja sheria yoyote.
  7. Kufuatia hali hii, yale majimbo ya CUF kisiwani Pemba ambako marjin ya ushindi ni ndogo, wameletewa wajeshi wa KMKM wamepiga kambi kihali kuimarisha usalama wa maeneo husika, hivyo wanalazimika kuandikishwa hapo walipo na 2010 watapiga kura kusawazisha ile slim difference ya kura za CUF na CCM hivyo CCM kujishindia kiulani.
  8. Pia kuna uthibitisho usio mashaka, viongozi wa CUF waliwahamasisha wafuasi wao kususia kujiandikisha na kuleta fujo ili kudororesha zoezi zima la uandikishaji kisiwani Pemba na serikali ikiwachukulia hatua, wapeleke kilio chao kwa jumuiya ya kimataifa kuwa uchaguzi sio huru na haki.
  9. Wakati CUF wao wakisusa, wenzao CCM wao wala vichwa, kwa kuwahamasisha wafuasi wake kujiandikisha kwa wingi, hivyo uchaguzi ukiitishwa leo, CUF wataangukia pua.
  10. Baada ya Maalim kumtambua Karume, wana CUF sasa wanajutia kisuso chao kutaka zoezi lirudiwe. Hata hivyo kwa Seif kumtambua tuu Karume, haitoshi, analazimika kuwa muwazi kwa wana CUF mazungumzo yao ya siri yalihusu nini ili hii michezo michafu inayoendelea kwenye uboreshwaji imalizike rasmi na zoezi liendelezwe kwa uwazi, amani na utulivu.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Nov 11, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Afadhali Pasco umetupatia habari kutoka kwenye chungu chenyewe! Tutajua tofauti kati ya kupambana na adui usiyemtambua na kupambana na adui unayemtambua! Which is which? Time will tell, 2010 is just nearby!
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kwa kweli mambo ni mazito
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hili la kupeleka Valontia, KMKM na JKU lilianza tokea mwaka 2000... Vijana wengi walipelekwa Pemba hata hivyo hapokuwepo na mafanikio yoyote. Miezi kadhaa baada ya uchaguzi kwisha vijana hao walionekana tena katika mitaa ya Unguja wakilalamikia hali ngumu katika makambi hayo ya muda...
   
Loading...