Africa kubakwa mara ya pili
Africa ni bara kubwa zaidi na lenye rasilimali za kutosha kuendesha maisha ya watu wake kama itapata viongozi makini wanaojielewa na kuielewa nini maana ya uongozi.Katika vitabu vingi vya mambo ya Public Administration wasomi wanalaumu zaidi uongozi wa Africa kuwa ni tatizo la muda mrefu zaidi na linalofanya Bara hili kuendelea kuwa hapa lilipo kimaendeleo.
Mara ya kwanza Africa ilibakwa na wageni walichukua Rasilimali watu kama nguvu kazi ana pia walichukua rasilimali nyingine na kujineemesha wao katika kitabu alichowahi kuandika msomi wa PHD mtanzania mwenye Walter Rodney How Eurpe Underdeveloped Africa anazungumzia kwamba Bank ya Baclays na kampuni ya lyoid insurence mitaji yake ilitokana na biashara hiyo haramu ya Utumwa.
Biashara hii ya Utumwa ilipigwa marufuku tarehe 25.03.1807 kupitia makubaliano yaliyowekwa kimataifa na kusainiwa kwa pamoja. Ingawaje pamoja na hilo la kuizuia biashara hiyo ya utumwa mwaka huo mwaka uliofuata bado biashara hiyo iliendelea Mwaka uliofuata kwa kificho ingawaje haikuchukua muda ilikoma kabisa kutokana na kukosa wanunuzi.
Huu mimi ninauita ubakaji mkubwa kuwahi kutokea barani Africa kwani nguvu ilitumika kuhakikisha biashara hii inafanyiaka.
Katika kipindi cha wiki mbili hizi kumekua na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao na vyombo vya habri vya kimataifa kama CNN kwamba kumekua na ushahidi kwamba Nchini libya biashara hii haramu imeanza kushamiri mpaka kufikia sehemu ambapo baadhi ya picha na video zimesambaa zikionyesha mmoja ya watumwa akiuzwa kwa dola 400 ambapo ni kama laki naneya kitanzania katika eneo ambapo lilidhihirika kwamba ni soko la watumwa huko libya.
Tayari Ufaransa imepaza sauti kuitishwa kwa kikao cha umoja wa mataifa kulizungumzia hili kwani ni kinyume cha haki za binadamu.
lakini wakati haya yakitokea ni sehemu ndogo tu ya Dunia inayozungumzia hili na sio Dunia nzima kwa maana wao wanafikiri kwamba wako salama kutokana na wao kuwa mbali na sehemu ambapo matukio hayo yametokea.
Viongozi wa Africa wanatakiwa kwa pamoja wapaze sauti kupinga huu ubakaji wa mara ya pili haraka kwa vitendo bila hivyo Africa inaweza kujikuta inarudi kwenye zama zile za utumwa na kutawaliwa.
ni muda tu ndio utakua shahidi kwenye hili na wala si vinginevyo.
hapo chini ni baadhi ya picha zikionyesha kinachoendelea hapo Libya kwenye hilo soko la kuuza watumwa.
View attachment 636975 View attachment 636996