Libya watu wanapigwa mnada kama ng’ombe

Libya watu wanapigwa mnada kama ng’ombe

Watajuta tena watajuta sana.

Hakuna hata siku moja Marekani atasikitika wala kuchukua hatua za kuwasaidia kuwa na amani, utulivu na maisha yanayoeleweka.

Wajifunze na wale vibaraka wengine wanaoweweseka mara tu wanapoona ngozi nyeupe.

Africa is for Africans.
 
Hao uliowaona siyo Walibya. wanatoka nchi mbalimbali za Afrika hasa Ethiopia, Somalia na Nchi za Afrika Maghribi na kati ikiwemo chad, Niger n.k

Libya ni mlango wa kupitishia hao watu kwenda Ulaya kutokana na Libya kukosa Udhibiti wa kuhakikisha wahamaji haramu hawaingii ama kupitia katika nchi yake. Libya imekosa utawala madhubuti wa kuhakikisha usalama wa mipaka yake lakjini siyo kwamba wanaouzwa ni Walibya. Si mwenyewe onaona walivyo weusi. WaLilbya wengi ni Waarabu.
 
Tamaa iliwaponza..... Eti mapinduzi yanaendeshwa na mtu ambae kwa miaka yupo nje anakula bata mzinga wa kukausha... tena anasubiri mushinde ndio aje... kazi wafanye wengine beef burger ale mwengine
 
Kuna video hiyo kiukweli inaumiza sana
mtu anauzwa kwa 400$
Du! haya laana ya Gadafi itawatafuna miaka 50+
Demokrasia ipi kwa Mamluki wa Wazungu hayo ndio malipo yao
Sasa $400 si laki 9 hiyo karibu 1M ?
 
Endeleeni kuanzusha vikundi vya kigaidi mkisingizia mnatetea dini.
Hivi hiyo habari inahusiana na dini? Au unataka kusema machafuko ya Libya yalitokana na masuala ya dini?!

Pole sana manake unatapika nyongo hata pasipo husika !
 
Naona majority wanachanganya madesa!

Hao Walibya mnaosema "wameyataka" sio waathirika wa hilo jambo! Kukosekana kwa serikali inayohodhi Libya yote kumeifanya nchi hiyo kuwa pepo ya genge la maharamia wanaojifanya kusafirisha watu kwenda Ulaya.

Sasa Africans kutoka West Africa na kwingineko; wale wenye ndoto za kwenda Ulaya; wakifika gate kuu la kuingilia Ulaya( Libya) ndipo wanakumbana na hayo madhira! Na wale wanaofanikiwa kuvuka Mediterranean Sea hadi Ulaya; hususani wasichana, nao wakifika huko wanajikuta hawana kwa kwenda wala kazi na hivyo kuishia kwenye mikono ya magenge yanayoendesha biashara ya ukahaba!

In short, hicho kinachotokea ni kile ambacho kimekuwa kikitokea kwa miaka kadhaa kwenye nchi za South East Asia.
 
Ngoja wapigwe mnada siwanakimbia nchi zao!,nchi za uarabuni ni matatizo mtupu na wanaubaguzi wa hali ya juu,hao waafrika weusi wanashindwa kutulia kwenye nchi zao wao kila kukicha wanakimbilia huko kutafuta maisha mazuri,maisha mazuri wanayotafuta ndo hayo sasa ngoja waipate fresh!


Swala la kupigwa mnada na ubaguzi linahusiana vipi? Umeielewa mada lakini?? Rudia tena kuipitia kwa umakini utajuwa kinachoendelea.
 
Hii haiwahusu walibya.. Nyie mnaosema laana ya Gadaffi mnaropoka..libya ni center ya hiyo biashara.. Watumwa wengi ni wa nchi za Africa magharibi na nchi zingine zilizokubuhu kwa umasikini..

Libya ni njia rahisi kwenda Italy kwa njia ya maji..Ndo mana biashara imeshamiri hapo..

Mambo ya Gadaffi na Walibya hayahusiki hapa
Hapana anahusika sana tena zaidi ya sana.
Yote yanashamiri kipindi hiki ambacho Libya haina serikali thabiti na wala si kipindi kile gaddafi akiwa madarakani.
Yakupasa ufahamu hao wanaowauza ngozi nyeusi ni miongoni mwa wale waitwao waasi ambao wametapakaa kila kona ya nchi.
USA na nato hawachomoki katika hili maana ndio waliovuruga ile nchi wakatengenezA mpaka movie 13 hours :secret soldiers of benghazi
 
Kuna video hiyo kiukweli inaumiza sana
mtu anauzwa kwa 400$
Du! haya laana ya Gadafi itawatafuna miaka 50+
Demokrasia ipi kwa Mamluki wa Wazungu haliyo ndio malipo yao
Mkuu, soma vzuri elewe wanauzwa sio walibya tu bali ni waamiaji toka mataifa mbalimbali pale libya ni kama soko/lango kuu la kwenda ulaya. mleta mada ni mnazi wa vyama na lengo lake ni kutisha watu ili waogope kufanya mabadiriko.
 
Wanaijeria mbona mnanisikitisha, mnatokaje huko kwenu mnakimbilia kwa waarabu wa libya matokeo mnaushia kuuzwa km nanasi sokoni, jamani Waafrika wenzangu mmniumiza sana, vijana tuache tamaa tukae kwenye mataifa yetu tupambane na maisha
 
Walitaka demokrasia.. kutoka kwa mabwana zao.
Kama wengine wanavyolilia hapa kwetu..au kule zimbabwe tusubiri tuone hatma yake.
 
Wapambane na hali yao ndiyo Maisha waliyochagu, Gadafi aliwaambia kuwa nchi za magharibi msifikiri wanawajali kuliko ninavyowajali. Tunaita mkataa pema..
 
Mm wala siwaonei huruma.. Maana ndicho walichokuwa wanakitaka,.

Hii ndio democracy waliokuwa wanaipigania maana waliikosa kipindi cha Gaddaf
Wa Libya ni madalali, wanaouzwa mnadani ni wajomba zetu wa West Africa, Ghana, Guinea, Nigeria, Cameroon etc
 
"Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba...!"
 
Wabongo wavivu kusoma wepesi kucoment na wafata mkumbo mnaambiwa african migrants mnasema laana ya gadafi wengne wanaenda mbali sijui chadema vile someni kwanza alafu comments mnashindana nin kucomments
 
Back
Top Bottom