Liangalie swala hili kwa jicho la tofauti!

bhikola

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,130
1,660
Habari za kwenyu kwa pamoja

Eti kila mtu anasema Dr JPM mr president anabana matumizi, mi nasema siyo kweli, hajabana matumizi. Nimegundua kuwa, watu wengi wameshindwa kutofautisha kati ya kubana matumizi, na kubadirisha matumizi.

Kwa mfano, kama ulikuwa ukitumia shs 10,000 kwa siku kwa chakula, kisha ukapunguza na kuanza kutumia shs 8,000 - hapo tunasema umebana matumizi. Lakini, kama unatumia kiasi hichohicho lakini umebadirisha menyu tu, basi haujabana matumizi kwasababu umetumia kiasi kile kile.
Turudi kwa le presida: fedha ya uhuru - imekenda kujenga barabara, hapo hajabana matumizi, amebadiri matumizi.

Fedha ya sherehe ya bunge - imekwenda kununua vitanda - matumizi yamebadirika, hajabana
Fedha ya safari za nje - ikalipie elimu bure,elimu ya juu mikopo imeongezeka

Tumuunge mkono JPM, na watu waache kulialia, kwamba mzunguko utapungua, sijui biashara zitadorora, hapana! mzunguko utakuwa ule ule kwasababu pesa inatumika vilevile.

Jumapili njema
 
Hajabana matumizi, ila anafanya vitu kutokana na vipaumbele, badala ya kwenda Ulaya vacation, unanunua dawa za wagonjwa au unasomesha watt wa maskini nk nk. Ni sawa na mzazi huwezi chukua hela kwenda kutanulia wakati nyumbani kuna dhiki kibao,
 
Nafikiri kubana matumizi maana yake ni kupunguza au kutoa mahitaji yasiyo ya lazima sana na fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi hayo kuongezwa kwenye matumizi ya lazima kwa kipindi hicho.

Rais anafanya vitu vitatu;
kubana matumizi mfn.kuondoa posho za vikao, kuondoa huduma kama vinywaji vya ghari nk.

Pili anabadili matumizi kama; fedha za maadhimisho ya uhuru kwenda kwenye barabara nk.

Tatu anaongeza makusanyo kwa kasi mfn. bandarini
 
Saafi! Rais songa mbele!
 
Habari za kwenyu kwa pamoja
Eti kila mtu anasema Dr JPM mr president anabana matumizi, mi nasema siyo kweli, hajabana matumizi. Nimegundua kuwa, watu wengi wameshindwa kutofautisha kati ya kubana matumizi, na kubadirisha matumizi.
Kwa mfano, kama ulikuwa ukitumia shs 10,000 kwa siku kwa chakula, kisha ukapunguza na kuanza kutumia shs 8,000 - hapo tunasema umebana matumizi. Lakini, kama unatumia kiasi hichohicho lakini umebadirisha menyu tu, basi haujabana matumizi kwasababu umetumia kiasi kile kile.
Turudi kwa le presida: fedha ya uhuru - imekenda kujenga barabara, hapo hajabana matumizi, amebadiri matumizi
fedha ya sherehe ya bunge - imekwenda kununua vitanda - matumizi yamebadirika, hajabana
fedha ya safari za nje - ikalipie elimu bure,elimu ya juu mikopo imeongezeka
Tumuunge mkono JPM, na watu waache kulialia, kwamba mzunguko utapungua, sijui biashara zitadorora, hapana! mzunguko utakuwa ule ule kwasababu pesa inatumika vilevile
Jumapili njema
Kwangu mimi naona kabaana matumizi tena sana maana kama pesa ile ingetumika kwa shughuli za sherehe za uhuru maanayake ilitakiwa itoke pesa nyingine tena kwaajili ya ujenzi wa barabata sasa hapo hajabana matumizi?? Au mie naelewa vibaya,,?
Labda kwa mfana wewe kama baba au mama una budget ya kunywa bia za 2,700,000/= kila mwaka na unamlipia mwanao ada ya sh.2,700,000/= kila mwaka maana yake kwa mwaka unatoa 5,400.000/=utakapo amua kuacha budget ya kunywa bia halafu zile pesa za bia ukalipa ada miaka miwili je!? Hapo huja bana matumizi, maana yake hiyo pesa ya ada ya mwaka mmoja mwingine itafanya tena kitu kingine sasa ni vipi ungekuwa umenywea bia? Nadhana hapo jibu litapatikana
 
Aisee umetoa mfano mzuri sana, si ajabu wewe ni mwl, na kama siyo basi unafaa kuwa mwl. tofauti iko hapa, JPM anachofanya siyo kusogeza matumizi, bali kuyatumia ndani ya muda uleule, kwa mfano tunaona vitanda vishanunuliwa, barabara inajengwa, na mengine yanafanyika. so kwa mfano ndani ya mwaka huohuo ungetumia hiyo 5.4m lakini badala ya kunywa bia, ukanunulia shamba, au ukanunulia nguo tv, baiskeli n.k
tuko pamoja
 
Nafikiri kubana matumizi maana yake ni kupunguza au kutoa mahitaji yasiyo ya lazima sana na fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi hayo kuongezwa kwenye matumizi ya lazima kwa kipindi hicho.

Rais anafanya vitu vitatu;
kubana matumizi mfn.kuondoa posho za vikao, kuondoa huduma kama vinywaji vya ghari nk.

Pili anabadili matumizi kama; fedha za maadhimisho ya uhuru kwenda kwenye barabara nk.

Tatu anaongeza makusanyo kwa kasi mfn. bandarini

Hicho ndicho linachoitwa kubadiri matumizi sasa, na siyo kubana matumizi. Ukibana matumizi tunategemea uwe na surplus
. kwa maana nyingine inabidi salio liongezeke kwa kipato kilekile kwasababu umebana, haukutumia
kwa maana hiyo basi, kubana matumizi ni kutotumia au kupunguza matumizi na usitumie kabisa
 
Hajabana matumizi, ila anafanya vitu kutokana na vipaumbele, badala ya kwenda Ulaya vacation, unanunua dawa za wagonjwa au unasomesha watt wa maskini nk nk. Ni sawa na mzazi huwezi chukua hela kwenda kutanulia wakati nyumbani kuna dhiki kibao,

very well said
pamoja sana
 
Habari za kwenyu kwa pamoja

Eti kila mtu anasema Dr JPM mr president anabana matumizi, mi nasema siyo kweli, hajabana matumizi. Nimegundua kuwa, watu wengi wameshindwa kutofautisha kati ya kubana matumizi, na kubadirisha matumizi.

Kwa mfano, kama ulikuwa ukitumia shs 10,000 kwa siku kwa chakula, kisha ukapunguza na kuanza kutumia shs 8,000 - hapo tunasema umebana matumizi. Lakini, kama unatumia kiasi hichohicho lakini umebadirisha menyu tu, basi haujabana matumizi kwasababu umetumia kiasi kile kile.
Turudi kwa le presida: fedha ya uhuru - imekenda kujenga barabara, hapo hajabana matumizi, amebadiri matumizi.

Kabana matumizi kabisa.Kama unabisha kawaulize wale waliokuwa wakipata posho za safari na vikao kama matumizi yao yako vilele.Hajawabadilishia matumizi bali kawabania matumizi.Hawaendi kukesha na kulala baa kama zamani.Sasa hivi wakinywa kiroba kimoja cha konyagi kilichochanganywa na kiroba cha gongo wanatimka mbio kulala.

Hawafungi baa kama zamani.Kawabania matumizi.
 
Hicho ndicho linachoitwa kubadiri matumizi sasa, na siyo kubana matumizi. Ukibana matumizi tunategemea uwe na surplus
. kwa maana nyingine inabidi salio liongezeke kwa kipato kilekile kwasababu umebana, haukutumia
kwa maana hiyo basi, kubana matumizi ni kutotumia au kupunguza matumizi na usitumie kabisa

Sasa surplus haitatumika?
 
Kabana matumizi kabisa.Kama unabisha kawaulize wale waliokuwa wakipata posho za safari na vikao kama matumizi yao yako vilele.Hajawabadilishia matumizi bali kawabania matumizi.Hawaendi kukesha na kulala baa kama zamani.Sasa hivi wakinywa kiroba kimoja cha konyagi kilichochanganywa na kiroba cha gongo wanatimka mbio kulala.

Hawafungi baa kama zamani.Kawabania matumizi.

Ha ha ha haaaaa
Thanks Mkuu, nimekusoma vyema,
ni kweli kabisa, kwa mtu mmoja mmoja "kawalazimisha" kubana matumizi, na hata kwa baadhi ya taasisi, kazilazimisha kubana matumizi. Lakini ukitazama nchi kama taasisi moja, basi kabadili matumizi
tuko pamoja mkuu, na pole kama umekuwa muathirika wa "kubana matumizi"
 
surplus unafanyia serving, na hata ukija kutumia siyo kwa wakati huo, itakuwa baadaye

Sawa mkuu, kwa bahati mbaya hatujafikia hatua hiyo ya kusave kwasababu mahitaji ni mengi na ya msingi ndio maana matumizi yanabanwa kisha kinachobaki kinabadilishiwa matumizi.
Hapo sawa?
 
tuko pamoja mkuu, nimekusoma point yako!
Thanks
 
Kabana matumizi kabisa.Kama unabisha kawaulize wale waliokuwa wakipata posho za safari na vikao kama matumizi yao yako vilele.Hajawabadilishia matumizi bali kawabania matumizi.Hawaendi kukesha na kulala baa kama zamani.Sasa hivi wakinywa kiroba kimoja cha konyagi kilichochanganywa na kiroba cha gongo wanatimka mbio kulala.

Hawafungi baa kama zamani.Kawabania matumizi.

Nimecheka balaa hakiyanan!
 
In Fact Kabadili Matumizi Zaidi Kwa Kutanguliza Matumizi Kwenye Vipaumbele Kwanza. Cause Kila Mradi Wa Serikali Unatakiwa Upangiwe Bajeti Ya Mwaka Pale Bungeni. Ipo Bajeti Hadi Ya Kutatua Majanga. Sasa Kama Unanunua Vitanda Muhimbili, Wakati Amana Wanawake Wa3 Wanashea Kitanda, What Is The Point?. Na Ikija Bajeti Ya Afya Ambayo Ilipaswa Kutatua Kero Zote Za Madawa Vitanda Nk. Itapunguzwa?. Mfano Ni Gwaride Kua Siku Ya Usafi. Kisha Akasema Hela Aliyosave Itafanyia Shughuli Nyingine. Je Itatumiwa Nje Ya Bajeti Ya Serikali? I Dont Think So! Kimsingi KApeleka Matumizi Kwenye Vipaumbele Vyake, Ili Kuweza Kupata Hela Nyingi Ya Kutekeleza Na Kukamilisha Mipango Ya Serikali Pengine Bila Kutembeza Bakuli Kwa Wahisani.
 
Back
Top Bottom