LHRC yaitisha Maandamano nchi nzima kupinga malipo ya DOWANS

LHRC, natofautiana nanyi! Suluhu siyo kuandamana ila ni kuwafungulia mashtaka WOTE waliohusika na sarakasi hii ya DOWANZI? RICHMOND! Wanajulikana, kama hamuwajui wasilaneni na kampuni ya HaliHalisi. Wana ushahidi wote, wameundika kwenye magazeti yao na ukweli huo haujakanushwa! Tutumie SHERIA kuwashinda KISHERIA kwani wao walitumia SHERIA (ya mikataba ya ki Mangungo), na wakashinda kesi ICC KISHERIA na Mahakama zetu KISHEIA, zimeshindwa kutengua malipo hayo kwani yapo KISHERIA!
 
Walikwenda mahakamani lakini wakashindwa au umesahau LHRC waliweka pingamizi la malipo haya ya Dowans? Halafu maandamano siyo vurugu endapo yatafuata taratibu zote zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na kupata kibali.
 
Kila raia mwenye kuitakia nchi yetu mambo mema bila shaka atayaunga mkono maandamano.Napendekeza marekebisho kidogo.Maandamano yalenge kupinga malipo ya Dowans,Yalenge kushinikiza uwajibikaji wa walioshiriki uingiaji wa mkataba,Yalenge kuishinikiza serekali kukamata mali za wamiliki wa Dowans na mwisho maandamano yasiwe na ukomo hadi madai yote yametekelezwa bila kuruka kipengele hata kimoja.




 

Haya malipo ya Dowans yanawahishwa ili kupata fedha za kusherehekea kifo cha mpambanaji Mwakyembe nini? Tusipoangalia na kukataa kwa pamoja watazikwa wote mmoja mmoja!!!!
 
Kwanini visifanyike vyote viwili ...kuandamana na kuwafungulia mashitaka..!?
 
Mlima gani kuna milima mingi Kitonga, Sekenke, Nyashana, fafanua baada ya kutoka Mlimani wapi?

Huwezi kujua ni Mlima gani kwa sababu wewe ni Shule less (Standard Seven leaver)!
 
Yatakuwa dsm tuu au nchi nzimaaaaaaaaaa!
Nina hamu na mabomu ya machozi!
 
ndugu zangu kwa wale wenye mali, tujaribu kuacha kabisa barua za urithi kwenye familia zetu.

Uwezi kujua kama tutarudi salama baada ya maandamo kama mnavyojua askari wetu na ffu.

Tujitokezeni kwa wingi vifo vya wengi ni harusi
haya ni maandamano ya woote ikiwemo na hao polisi kwani wenyewe ndo wakuua ndugu zao na kuishia kukaa kwenye magofu huku b 111 zikipotea bure hapo kuna nyumba ngapi za hao polisi!
 
pamoja na yote hakustahili adhabu ya kikatili namna ile!
 
 
Sidhani kama hayo maandamano yatafanikiwa coz watu hawaifahamu hiyo LHRC ndiyo kitu gani: Nashauri waya binafsishe kwa cdm zen waone peoples power ilivyo na nguvu, ten days mfululizo? ****** aweza kimbia pale magogoni walahi
 
Tuko pamoja aisee ni mevimiss virungu ngoja nitayarishe bango na helment
 
 
Huyo ritz mwacheni anaweweseka make very soon kitumbua kitaingia mchanga!muda wa kulea uozo umekwisha, maandamano hadi watwambie pesa tunamlipa nani na kwa lipi!nani mkuregenzi dowans tanzania?walijiona wajanja kutuingiza kule lakini najua ipo siku watakimbia nchi kwa nguvu ya umma!
 
Hayo mashirika yaliyoungana yahakikishe wanaweka vipindi vingi vyakutosha kwenye tv redio na magazeti, waTZ wengi zaidi wasikie ufedhuli uliofanywa na viongozi na makusudi yakuandaman na madhara ya kukaa kimya. Knowlege is power. Lets educate uma wa Tz. Its time to stand for our rights.
 
111 bilioni ni sawa na madawati 2,200,000 kwa bei tsh 50,000 dawati moja . Hapo utakuwa umewaokoa wanafunzi zaidi ya milioni sita adhabu ya kukaa sakafuni . Wizi uzembe wa kiwango hiki haukubaliki kamwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…