LHRC kuipinga 15% ya Bodi ya mikopo Mahakamani

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Kuna tetesi japo ni za uhakika kwamba kuna watetea wanyonge wamejitolea kulipeleka swala la 15% mahakamani kwa lengo la kupinga ongezeko hili .

Kama ni kweli binafsi nipo tayari kuchangia gharama kama zitahitaji kwa ajili watoto na ndugu zetu ambao wananyanyasika bila sababu.

Tamko kutoka LHRC

"LHRC tunajiandaa kuandaa kesi kupinga malipo ya bodi ya mikopo ya 15% kwa waliopata elimu ya juu tutakuwa na kikao na mawakili jumanne next week saa 10 ofisi za LHRC karibuni mawakili pia mje kwa wingi."

Imetolewa na
Advocate Patience Mlowe
 
Sio mbaya kujaribu, ila inaonyesha ukilaza wa watu. Habari haikuanza leo...tangu sheria inapitishwa walikuwa kimya tu.
Wasomi bana....teh teh......
 
Sio mbaya kujaribu, ila inaonyesha ukilaza wa watu. Habari haikuanza leo...tangu sheria inapitishwa walikuwa kimya tu.
Wasomi bana....teh teh......
poa , sa hivi kwa sababu wameanza kukata , ni rahisi zaidi, imagine MTU wakati unakopa ilikua 8% lakini unabadilishiwa na kukatwa 15% why???
 
15% in halali kuilipa kwa wale tu watakaosaini aslimia hiyo. Wale waliosaini 8% haikutakiwa kuwagusa. Serikali imevunja mkataba. Kisheria imekosea na itashindwa vibaya.
mkuu umesema vyema kabisa, na mahakama itatakiwa kuiamuru serikali iwalipe fidia.
 
Hii ni nchi ya kodi kubwa kubwa. Mnatakiwa kujua hivyo. VAT ni 18%, PAYE yenyewe hata sisemi, HESLB 15%, ukiagiza kigari chako chakavu unalipa zaidi ya asilimia 85% ya CIF nk. Lakini bado nchi yetu ni miongoni kwa nchi maskini zaidi duniani. Kuna clip amepost Mange Kimambi kule Instagram, wazungu wanajadili umaskini wa watanzania na kodi kubwa tulizonazo. Watakaoweza waiangalie tena, inachekesha, lakini inafikirisha sana. Tuna taifa ambalo viongozi wake wanafikiri kodi kubwa kubwa tu kila siku..... hawajawahi kufikiria nje ya box ili kutambua ni kwa nini kuna nchi zina maendeleo makubwa ya kiuchumi kuliko sisi huku zikiwa na na viwango vidogo vya kodi. Ni mwendelezo wa akili zile zile za miaka nenda rudi: zikitokea ajari mbili tatu, dawa yake ni kuweka matuta katika barabara zote! Think outside the box....
 
Kwa hili mawakili wetu wako sahihi kabisa. Tunafundishwa kuwa sifa mojawapo ya sheria ni kuanzia pale inapotungwa na si kurudi nyuma. Lakini nashangaa sheria zinazotungwa sasa hivi zinarudi mpaka nyuma. Labda wana sheria watusaidie kwenye hili ili na mimi nielewe.
 
Kwa hili mawakili wetu wako sahihi kabisa. Tunafundishwa kuwa sifa mojawapo ya sheria ni kuanzia pale inapotungwa na si kurudi nyuma. Lakini nashangaa sheria zinazotungwa sasa hivi zinarudi mpaka nyuma. Labda wana sheria watusaidie kwenye hili ili na mimi nielewe.
muhimili wa bunge sio rahisi kuupinga, ni rahisi mahakama kupinga bunge kuliko bunge kujipinga lenyewe.

Bunge limetawaliwa na wana ccm, si unakumbuka zile mil 10, huwezi honga mahakama na ukabaki salama.
 
Kwenye hili hata mimi ntachangia gharama mana linanitesa sana. Ukijumlisha bank nina mkopo wa marejesho ya 400,000 +Paye(30%)+NSSF +15%(HESLB) bado kodi ya nyumba bado mafuta ya gari +matumizi ya kuishi afu salary chini ya million, achen tu
 
Naomba niwaulize wadau kwa sisi tuliopewa mkopo na Heslb kabla ya hii 15% je kulikuwa na kipengele kwenye mkataba kilichoonyesha kuwa tutakatwa 8%?
Naomba mnisaidie
 
Watoe account tuchangie gharama za uendeshaji wa hiyo kesi hii nchi sasa imekua sio rafiki kwa mfanyakazi, sheria zinavunjwa bila aibu wala haya usoni, unaanzaje kumkata mtu 15% wakati mlikubaliana 8%!!!!!!!!!!!! kuna vitu tunavichekea leo siku tukifa watoto wetu watachapa viboko makabuli yetu.
 
Naomba niwaulize wadau kwa sisi tuliopewa mkopo na Heslb kabla ya hii 15% je kulikuwa na kipengele kwenye mkataba kilichoonyesha kuwa tutakatwa 8%?
Naomba mnisaidie
Hahaha yani ww kipindi hicho ulikuwa unawaza boom tu, ndio ipo kwenye mkataba 08%
 
we lipa wwe kutesa kwazamu mmetuoshea sana chuo na vi boom vyenu ssa mnalalmika nni ukiangalia uliishia kula bata tu hafu saivi unaona uchungu we tuliaaa unyolewe
 
Back
Top Bottom