Mimi niko nyuma ya Slaa, sababu ndiye chaguo la wengi. Na atakalosema talifuata. NEC ni extension ya CCM, haina jipya. Hata matokeo yanayotangazwa hayana mvuto si kwa wana-CHADEMA tu, hata kwa Wana-CCM wenyewe na watanzania wote kwa ujumla. Wameyaona matokeo yalivyokuwa katika majimbo yao, wanamshangaa Makame anavyoropoka ovyo. Hata kama umepewa sheria ya kutangaza, tangaza kadiri ya matashi ya wananchi sio kwa shinikizo. Makame unachafua profession yako kama mwanasheria na zaidi kama Jaji. Mbona aibu hata mtaani ukipita? Pole Makame kwa kukosa utashi binafsi.