JNIA, DAR: Rais Magufuli katika uzinduzi wa mradi wa rada na mapokezi ya ndege mpya ya ATCL

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
image.jpeg
Marubani wa ATCL wakiwa eneo la tukio Terminal One
image.jpeg
Tayari wageni mbalimbali wamehudhuria katika eneo la uzinduzi wa mradi wa usimikaji wa rada za kiraia katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) eneo la Terminal Two,na baadae Rais ataambatana na wageni mbalimbali kusogea eneo la Terminal One(VIP) kuipokea ndege yetu ya Bombardier iliyokuwa inashikiriwa huko Canada.

Wageni mbalimbali wamefika,wakiwemo viongozi mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama,Wakuu wa mikoa katika mikoa yote minne ambayo rada zitawekwa ambapo ni Dsm,Mwanza,Mbeya na K'njaro.Band ya Polisi inaendelea kutumbuiza.

Mkuu wa Mkoa wa Dsm ameshawasili akiambatana na msanii wa kizazi kipya Diamond Platinumz.Wanachama wa chama cha Mapinduzi wakiwa na sare za chama,wananchi toka maeneo ya jirani na uwanja wa ndege wa Dsm na mabalozi kadhaa wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania.



Itaendelea....

Makonda

Anamkaribisha Rais na kuwasalimia viongozi wote kwa kuzingatia itifaki.

Makonda anasema Pasaka hii hakuna Waraka toka jiji la Dar. Watu wameabudu kwa amani kabisa. Pia amezungumzia watu kutoka mikoa mingine na kuja kutoa kauli za uchochezi Dar na kusema wanajipanga kudhibiti hilo maana Dar ni Jiji la kibiashara linalohitaji utulivu.

Anamshukuru Rais kwa barabara zinazojengwa mkoani Dar ikiwemo ya Tegeta hadi Mbezi Mwisho.

Mwisho anamkaribisha Rais mkoani Dar

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza S. Johari

Anaelezea mradi wa rada 4 ambazo zitasimikwa katika Uwanja wa Dar, Mwanza, Kilimanjaro na Songwe. Rada hizi zitakuwa na mifumo Primary na Secondary na zitaweza kugundua kila chombo kitakachosafiri katika anga letu hata kikiwa kimezima vifaa vya ugunduzi ama ikiwa haina. Mradi utatumia Bilioni 67.3 ikijumuisha Rada pamoja na Miundombinu na utagharamiwa na Serikali yenyewe bila kukopa.

Mradi ulianza Novemba 2017 na utaisha Mei 2019 yaani utachukua miezi 18.

Hadi sasa malipo ya awali 20% yameshalipwa kutoka vyanzo vya ndani vya TCAA. Rada ya kwanza imeshaanza kuwekwa Dar na mwezi wa 4 factory acceptance test itafanyika.

Kwa sasa ndege haziwezi kupangwa bampa to bampa sababu za kiusalama. Zinapangwa dk 10 apart. Hivyo tutaingiza mara 8 ya kipato cha mwanzo. Zile ndege ambazo zilikuwa zinatukwepa zitapita kwetu.

Wataalamu 33 wa mamlaka wamepewa mafunzo ili kuweza kuoperate mitambo. Rada hizi zinaua kampeni za nchi jirani za kutaka kukasimiwa kuongoza anga letu kutokana na sisi kuwa na vifaa hafifu.

Changamoto iliyopo ni kutokamilika kwa jengo la kuongozea ndege Jijini Mwanza. Mwanza ilikuwa iwe ya pili katika kusimikwa kwa rada ila sasa inabidi iwe mwisho baada ya Dar, Kilimanjaro na Songwe. Tunategemea itakapofika wakati wake jengo hilo litakuwa kamili.

Waziri Makame Mbarawa

Anamshukuru Rais kwa kuwa mgeni rasmi licha ya majukumu yake ya kitaifa.

22 Agosti 2017 Serikali iliingia Mkataba na Kampuni ya Ufaransa wa kusimika rada 4 nchini ambapo mradi utagharimu takribani Shilingi Bilioni 67.3 na TCAA itagharamia 45% na Serikali kuu 55%.

Mradi huu umezingatia uendelevu hivyo umeweka dhamana ya miaka 3 ili kuhakikisha mkandarasi analeta vipuri endapo hitilafu yoyote itatokea. Pia mkandarasi atahakikisha vipuri vinapatikana kwa miaka 12 baada ya hapo.

Anaipongeza TCAA kwa matokeo mazuri ya ukaguzi wa kimataifa wa ICAO(Intenational Civil Aviation Organization) wa viwango vya udhibiti wa kiusalama wa Anga. Matokeo yameonesha Tanzania imepanda katika viwango vya udhibiti wa Kiusalama wa Anga kutoka 37.8% za 2013 hadi 64.35% za 2017.

Rais Magufuli

Nimefurahi kwa sababu mradi utakapokamilika tutaweza kuona nagaletu lote na pia Burundi na Rwanda ambalo tumekasimiwa.

Hivi sasa tunapoteza tozo la Bilioni 1 kutokana na sehemu ya anga letu kukasimiwa kwa Kenya. Nina imani mradi ukiisha wataturudishia.

Nawapongeza TCAA kwani nimesikia mmevuka lengo la usalama la ICAO la 60%. Mlikuwa na 37.8% mlikuwa vilaza kweli kweli.

Zaidi ya 70% ya watalii wanatumia usafiri wa Anga. Tumepanga kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini kutoka milioni 1.3 hadi milioni 5.

Tumenunua ndege mpya 6 ikiwemo 1 ambayo itafika leo saa 11.

Kabla sijaweka jiwe la msingi la Rada naomba nisema mambo matatu:-

1. Mumsimamie mkandarasi ili mradi uishe hata kabla ya wakati. Tunahitaji mradi uishe haraka. Nchi ya Ufaransa ni rafiki zetu hivyo najua mtashirikiana vema.

2. Naomba muandae wataalamu wa kutosha kuendesha mfumo. Nimefurahi kusikia wataalamu 33 wako Ufaransa wakijifunza.

3. Nakuagiza Waziri kuwa Kandarasi wa Jengo la kuongozea ndege Mwanza amesuasua sana asimamiwe akamilishe. Suala la pesa nimeshakwambia Serikali ya Awamu ya 5 haina tatizo la pesa. Tena isibadilishwe schedule, Rada zisimikwe kwa utaratibu uliowekwa awali. Naomba uwe mkali kwa hili Waziri japo unatokea ZNZ, nione ukali wako katika hili. Kama tatizo ni pesa asema anadai kiasi gani lakini asilete kisingizio cha pesa.

Hiki ni kiporo kilichopo tangu Uhuru. Lazima tuwe na control ya Anga letu.

Ninakuomba contractor umalize kazi. Nchi ya Ufaransa ni tajiri mfanye kazi usiku na mchana.

Nchi hii uwezo wake sasa ni mkubwa mno, ni wa maajabu. Ndio maana watu wengine wenye wivu wivu hivi wanaumia sana. Na wenye wivu wapo tu, hata Mungu aliumba malaika pakatokea wenye wivu Mashetani yakagoma yakatupwa huku duniani. Nayo lazima yawe na wafuasifuasi wa aina fulani wenye wivu wivu.

Kwa sababu ni maajabu kwa nchi kama hii Tanzania ambayo katika miaka mingi heshima ya Tanzania ilipotea. Ulikuwa huwezi ukayaona mawingu ya kitu kinapaa huko angani kilichoandikwa Tanzania. Nchi kubwa, watu milioni 55 hata ndege tulikuwa tumekosa. Na ndege ndio heshima ya nchi!! Tumeingia madarakani tukaamua lazima tuwe na ndege. Wakasema pesa atapata wapi. Nikasema pesa ziko kwa Mafisadi na watazitema hata ikibidi kwa kutapika.

Tukanunua ndege 6 bila kukopa. Zilipokuja hao hao waliokuwa wanaponda ndio wa kwanza kupanda hizo ndege. Tunawasamehe sana.

Kwenye nchi zilizostaarabika, huwa wanaungana hata wakiwa na itikadi tofauti. Tunajenga hivi vitu kwa ajili ya Watanzania wote na si familia zetu tu.

Sekta ya madini imechangia 11.5% hadi 17% baada ya sisi kubana wanyonyaji.

Wapo watu duniani hata ukiwabeba mgongoni ukawavusha mto wakifika ng'ambo watasema limgongo lake lilikuwa linanuka jasho. Tuwaombee tu, tusiyumbishwe tuko pazuri mnoo.

Wako watu waliokuwa wamezoea fedha za bure za kuwaibia masikini hao ndio wanapiga kelele sana. Ninafahamu hata makanisani zaka zimepungua sababu zilikuwa zinatolewa na mafisadi.

Watendaji wangu wanafanya kazi sana. Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wanafanya kazi ndio maana tuko salama leo. Ilifikia kipindi hata kwenda Kibiti ilikuwa shida, hatukuona mtu yeyote analaani. Kufa kwa Kibiti ni salama, hakuna hata waraka uliotoka. Ingawaje sipendi sana kulizungumzia hili kwa sababu ninalijua wala halina msingi wala halitafanikiwa wala hakuna lolote. Kwa sababu Serikali ipo nimekabidhiwa na wananchi kuilinda kwa nguvu zote. Na ninasema kweli kweli; Wengine nawaangalia tu nawacheki nasema " Hiiiiiiiiii"

Baba wa Taifa alishasaidia nchi nyingine kupata uhuru. Jukumu langu mimi sasa ni kujenga uchumi wetu!

Katika juhudi hizi watatokea wa kunung'unika, wa kupiga kelele hata sitawasikiliza.

Kazi ya uongozi ni ngumu sana, unageuka huku unakuta watu wanalalamika. Hata Wakina Musa walipata shida, unawavusha watu unakuta wengine wameshajenga na sanamu la dhahabu.

Hivi vitu vya maendeleo kama Stiegler's Gorge, Ndege 6, SGR mbona havikuwepo miaka iliyopita? usione vyaelea vyaundwa.

Serikali ipo haijalala na haitalala. Usimuone Simba amelala ukamchezea Mkia.

Mapokezi ya ndege Bombardier Dash-8 Q400...

Ndege ya tatu ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Dash-8 Q400 imewasili nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na rais Magufuli.

Ndege aina ya Bombardier Q400 ambayo ilikuwa ikishikiliwa nchini Canada imewasili nchini na kupokelewa na Rais Magufuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa (JNIA)

Baada ya Viongozi wa dini kufanya sala, rais Magufuli amesema na kusema tukiendelea na mambo ya kufuata ratiba tutatoka hapa usiku,

Viongozi wa dini wameongea maneno yenye utukufu yenye ujazo, niwaombe ndugu zangu watanzania tutangulize Uzalendo, penye mali ya watanzania tushikamane kwa pamoja.

Hakuna maneno ya kuongea makubwa zaidi ya haya maombi Viongozi wetu wa dini waliyoyatoa.

Kwa maneno ya Viongozi wa dini, sasa nipo tayari kwenda kuzindua ndege.

Amezindua ndege na kusema ikibidi ianze kazi ndani ya siku tatu. Baada ya kuzindua amepanda kwenye ndege yeye na Viongozi wa dini.

Akiwa amekaa ndani ya ndege ameomba waandishi wa habari wote waitwe, alivyoona wanachelewa akasema "acha nikawaite mwenyewe". Akashuka kutoka kwenye ndege na kuagiza Viongozi wote wa Ulinzi na Usalama na Wabunge wote wapande wakapige picha baada ya hapo akataka kila mtu aliyefika uanjani apande akapige picha.

Rais ametoa ruhusa kwa Watanzania waliofika kuipokea Ndege hiyo kupanda ili kupiga picha
-
Amesema waingie 76 (level seat) wakitoka waingie 76 wengine hadi watu wote waishe
-
Ujio wa ndege huu umekuwa ukisubiriwa kwa hamu na wananchi sambamba na kutaka kufahamu sababu za kwanini ilishikiliwa Canada tangu 2017 na kesi imeishaje?
 
Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa. Mubashara TBC 1 linarushwa tukio muhimu sana la mapokezi ya Ndege aina ya bombadia iliyokuwa imezuiliwa nchini Kanada. Tufuatilie Uzi huu kwa update. Rais magufuli anaongoza maookezi hayo makubwa na muhimu KBS kwa nchi yetu.
 
Tayari wageni mbalimbali wamehudhuria katika eneo la uzinduzi wa mradi wa usimikaji wa rada za kiraia katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) eneo la Terminal Two,na baadae Rais ataambatana na wageni mbalimbali kusogea eneo la Terminal One(VIP) kuipokea ndege yetu ya Bombardier iliyokuwa inashikiriwa huko Canada.

Wageni mbalimbali wamefika,wakiwemo viongozi mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama,Wakuu wa mikoa katika mikoa yote minne ambayo rada zitawekwa ambapo ni Dsm,Mwanza,Mbeya na K'njaro.Band ya Polisi inaendelea kutumbuiza.

Mkuu wa Mkoa wa Dsm ameshawasili akiambatana na msanii wa kizazi kipya Diamond Platinumz.Wanachama wa chama cha Mapinduzi wakiwa na sare za chama,wananchi toka maeneo ya jirani na uwanja wa ndege wa Dsm na mabalozi kadhaa wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania.



Itaendelea....

Kwahiyo huyo Diamond Platmumz amekaa high table na RC?
 
Back
Top Bottom