Let's talk about savings: Ikitokea umeachishwa/umeacha kazi leo, una akiba ya kukutosha kwa siku ngapi?

Nafkir nikuelekeze kitu mdau.
Lima heka 3 za mpunga kwa kuanzia.
Ukihudumia vizur ni Magunia 60 then yaweke stoku kwa miezi sita gunia moja ni sh 100,000.
Hivyo ukiuza unapata 6,000,000 unaweza ukaanza ujenzi.

Altenative way.
MweI wa saba wakivuna Mpunga nunua magunia 10 ya mbegu kubwa kama una mtaji mdogo kwa sh 760,000.
Baada ya miezi sita kila gunia ni sh 100,000 hivyo kwa nagunia 10 itakuwa ni milion moja.
Iweke fixed akaunti ili msimu ujao ufanye hivyo na uongezee na mtaji mwingine hiyo itakutoa kimaisha kama utakuwa mvumilivu.

Binafsi mjmi ni Muajiriwa wa gvt nimelima hekar 10 za Mpunga msimu huu tena mbegu ndefu.
Gharama zake mpaka kuvuna ni sh 3,000,000 natarajia kuvuna kima cha chini gunia 200.
Nikiweka stoku nakuja kuuza baadae miez 8 natarajia kupata 22,000,000.
Sasa una hiari mkuu kutafakar suala hili.
 
Focus yako weka kwa basic needs tu. Hakikisha unatumia allowance zaidi kama zipo na mshahara usiguse. Hela ikikua invest kwa fixed assets na liquid assets kwa kucheza na financial markets japo nazo ni fragile sana hasa kipindi hiki. Biashara ni nzuri sana kama una committed staff kama umeajiriwa. Ila zinalipa sana.
 
Salaam wakuu

Ushauri wangu kwako unayetaka kusave japo watu wengi wamekiri ni vigumu mimi pia hapo kabla ilikuwa ngumu ila nimefanikiwa baada ya kuapply njia hii

Mimi ni Mkristo so baada ya kufundishwa sana juu ya fungu la kumi / ZAKA. kwa kweli hii ni ya muhimu sana hasa kama unatamani kufanikiwa kiuchumi bila kujali kipato chako. Zaka ni 10% ya pato lako ila ni insurance ya 90% ya kilicho baki. Wajumbe wengi wamesema wa nasave ila kunatokea majanga mbalimbali yanakomba saving yote sababu ni kutokuwa na ulinzi katika fedha yako
kwa reference tusome hapa

Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.
Malaki 3:10‭-‬11 SUV

Nawatakia mafanikio mema
 
Humu Jf wengi watasema wa mamilioni benki...Akiba ni jambo la muhimu na ni ukweli wengi wanalipuuzia au kulichukulia kwa urahisi.
Kuna kanuni ya kuweka akiba kabla hujaanza kutumia fedha,ni nzuri inasaidia sana.
ingekuwa ni vyema kusema hiyo kanuni hapa ili itusaidie wote
 
Kulingana na usawa huu ulivyo, na jinsi kipato kilivyo kigumu upatikanaje wake na hata kinapopatinakana hakikidhi mahitaji na hapo hapo unahitajika uweke akiba i wonder how is it possible kwa uchumi huu nilionao!.

My personal story.
Ni kijana nimeajiriwa mahali mshahara wangu ni Tsh 250,000 per month najitegema lakini bado sijaoa! Kwa muda sasa nimekua nikipambana kufanya savings kwa sababu najua umuhimu wake hasa kwa wakati wa shida na pia hata kama si wakati wa shida unaweza jiwekea akiba ili uweze kufikia malengo fulani ya kiuchumi like kupata mtaji wa kuanzisha biashara e.t.c!

Lakini mambo yamekua si rahisi hivyo mshahara haunitoshi kulingana na mahitaji niliyonayo na pamoja na kujitahidi kujibana na kwa maana hiyo haufiki hata mwisho wa mwezi hua nakaaga natafakari hivi kwa mtindo huu mshahara kutotosha ikitokea nimeachishwa kazi sasa hivi ka akiba kangu kadogo ninakojiwekea kanauwezo wa kunitosha hata kwa wiki mbili zaidi kweli??

Nimeuleta uzi huu wa changamoto zangu binafsi kufahamu wenzangu linapofika suala la saving mnakabialiana nalo vipi na je, una kiwango cha kutosha cha saving ikitokea chanzo chako cha mapato mirija imekatwa? Mwenzangu unatumia njia zipi unazoziamini katika kufanya saving? Let me hear from you, let's talk about savings!
Your personal story ni kama ya kwangu
 
Nafkir nikuelekeze kitu mdau.
Lima heka 3 za mpunga kwa kuanzia.
Ukihudumia vizur ni Magunia 60 then yaweke stoku kwa miezi sita gunia moja ni sh 100,000.
Hivyo ukiuza unapata 6,000,000 unaweza ukaanza ujenzi.

Altenative way.
MweI wa saba wakivuna Mpunga nunua magunia 10 ya mbegu kubwa kama una mtaji mdogo kwa sh 760,000.
Baada ya miezi sita kila gunia ni sh 100,000 hivyo kwa nagunia 10 itakuwa ni milion moja.
Iweke fixed akaunti ili msimu ujao ufanye hivyo na uongezee na mtaji mwingine hiyo itakutoa kimaisha kama utakuwa mvumilivu.

Binafsi mjmi ni Muajiriwa wa gvt nimelima hekar 10 za Mpunga msimu huu tena mbegu ndefu.
Gharama zake mpaka kuvuna ni sh 3,000,000 natarajia kuvuna kima cha chini gunia 200.
Nikiweka stoku nakuja kuuza baadae miez 8 natarajia kupata 22,000,000.
Sasa una hiari mkuu kutafakar suala hili.
Safi sana ndg nmeipenda hii
 
Nimeiweka mbona..Ni hii kanuni ya kuweka akiba kwanza kabla hujaanza kutumia fedha.Yaani ukipata fedha zako unatoa kwanza akiba kama tumizi lako la kwanza then unaendelea na mengine.Infact anza na sadaka kama ni mtu wa imani yeyote kisha weka akiba then anza kutumia kwa matumizi mengine.


ingekuwa ni vyema kusema hiyo kanuni hapa ili itusaidie wote
 
nawafundisha watu kuweka akiba lakini siamini katika kuweka akiba kweye pesa.
hivyo mimi sifanyi ninachokihubiri.
uelewa wao unapokuwa mkubwa sasa naanza kuwaeleza ukweli kuwa kuweka fedha ni hasara ni bora wafikirie jinsi ya kuziwekeza kwakuwa kila anayeweka fedha benki fedha hupungua thamani na hasa katika nchi zetu tulioamua kupima uchumi kwa fedha za wazungu! USD money
 
kula like!
Nimeiweka mbona..Ni hii kanuni ya kuweka akiba kwanza kabla hujaanza kutumia fedha.Yaani ukipata fedha zako unatoa kwanza akiba kama tumizi lako la kwanza then unaendelea na mengine.Infact anza na sadaka kama ni mtu wa imani yeyote kisha weka akiba then anza kutumia kwa matumizi mengine.
 
Safi sana mkuu, unatupa moyo na sie wengine kuona kua mambo yanawezekana kama hutojali kwa upande wa changamoto katika suala la saving ipi ilikupata na ulipigana vipi kuishinda mana kwangu changamoto ni kua na save lakini shida inapopiga hodi hua ni majanga inakomba hela yote naanza na moja sasa sijajua kua tatizo ni amount ninayo save ni ndogo (kulingana na kipato changu) mpaka saving yangu inashindwa kuhimili changamoto za kiuchumi mara zitokeapo au nini? (i don't know) Na je, mwenzangu ulikua unatumia njia gani ku save kwa kuweka bank (saving acc) au ulifungua fixed acc special for saving only? Au kuweka m-pawa kama njia ninayoitumia mimi?
mkuu Mr genius mimi siijui benki yoyote ya akiba ,zaidi naijua benki ya mshahara wangu tu.
baada ya kuona nadumbua sana nikaona sio kesi,nikaanza kucheza mpeano na rafk angu,mwezi mmoja nampa kiasi fulani cha pesa na mwezi ungine ananipa yeye,

mfano mwezi huu nampa laki mbili na yeye mwezi ujao ananirudishia laki mbili(mimi natenga laki mbili yangu na ile alonipa inakuwa laki nne) natunza.
.mwezi baada ya mwdzi mmoja akinipaa tena natunza nakuwa na laki nane na tunza natunza mpaka inakuwa nyingi....
.

lakini nilikuwa nampa mtu ambae ninamuamini nimetoka nae tumbo moja,nikioa nadhani ntatoboa zaidi kwa sababu kinachonikost kula sasa nikioa namuambia wife chaakula kwa mwezi kiasi kadha na hii akiba

ndugu siri ya kutunza pesa ukiwa na kiasi fulani tu unatamani uweke zaidi,juzi juzi nimepata tatizo nikawa naona hasara kuzitoa kwa sababu zimekuwa nyingi,

kusave pesa ni kutamua muhimu usiweke kwenye akaunti yako ya kila siku eidher mpe mtu unaemuamini kama wife au mama au dada,

mimi nilikuwa nampa sister wangu yuko mbali na mimi kabisa
 
The best way ya kufanya savings,ikifika mda wa mavuno nunua chakula cha kutosha, nunua friji yako,ukiwa na mchele hada debe 5 kwa wenye familia,na gunia la mahindi na lita kumi ya mafuta ya alizeti huo mwaka unakupita poa kabisa,kila mwisho wa mwezi nenda na sh arobaini kanunue kauzu na maharage nyanya nk nk huwezi amini route za kwa mangi kila siku mara nipe una robo nk,

Lakini ukinunua mazaga yako mfano carot unayouziwa wewe gengeni sh 200 ukienda karume unapata sadolini kwa 5000 ukiweka kwenye friji si zinakupiga kick, sado ya nyanya 4000 nk,unaweza kuta kila siku pay inayotoka mfukoni haizidi hata 3000 kwa mboga.utashangaa bajeti yako kwa mwezi kwa chakula tuu hazidi 70000 out of lakini naa,sasa hapo huja save bado?

Hapo home machalii unawapiga na uji poa wa lishe,maisha haya bila kuwa na bajeti usawa wa uncle magu hutoboi,mi kuna mzee nilimshuhudia analipwa 150000 na alikuwa anaishi hivyo huwezi amini anasomesha watoto shule kali tuu, yeye anakwambia mi dukani huwa sikanyagi kununua chakula labda niamue mwenyewe
Nashangaa una-like 12 tu na hii ya kwangu ya 13...ulichozungumza ndio ukweli wenyewe na wengi huwa wanatoboa alafu baadae wanakula kuku kwa mrija
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom