Let's talk about savings: Ikitokea umeachishwa/umeacha kazi leo, una akiba ya kukutosha kwa siku ngapi?

Nokia83

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
24,664
2,000
Mimi nina miezi 4 sasa sijaweka akiba,mwaka huu tika umeanza nlikuwa na majukumu fulani yamenifanya nishindwe kuweka akiba
 

Galore

JF-Expert Member
Feb 14, 2015
253
250
Ila honestly speaking,kusave ni mtihani jamani,sikumbuki mara ya mwisho mishahara yangu kukutana,hata 5000 :(:(:(
 

wiser1

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
2,135
2,000
Binafsi kila nikipata hela yangu ya mshahara naweka savings kabla sijautumia

250,000 ndo akiba nayoiweka kwa mwez! Kwahyo ninayobaki nayo ni ndiyo napanga nayo budget!

Mwaka ujao nina plan za kuongeza kiwango cha kusave maana nauhakika naweza anza mradi wakunipatia kipato cha ziada kuliko kutegemea kale ka mwisho wa mwez
 

Kijana kijana

JF-Expert Member
Mar 11, 2018
2,549
2,000
mimi nilianza kazi miaka miwili nyuma nikawa natumbua sana ,ila kama minne nyuma nikagunduka kwamba haya sio maisha ,

ni miezi mitano kama hivi nikaanza kusave wakuu huwezi amini mwiki mbili nyuma nikawa na kiasi cha milioni moja na saivi nimenunua kiwanja tayari na nafanya mpango ndani ya mwaka huu niwe na viwanja kama viwili hivi kisha mwakani niwe na viwanja viwili tena jumla vinne kwa uwezo wa mungu..

kisha hapo naanza kufikiria biashara ya kufanya ,
 

Mr.genius

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
1,246
2,000
mimi nilianza kazi miaka miwili nyuma nikawa natumbua sana ,ila kama minne nyuma nikagunduka kwamba haya sio maisha ,

ni miezi mitano kama hivi nikaanza kusave wakuu huwezi amini mwiki mbili nyuma nikawa na kiasi cha milioni moja na saivi nimenunua kiwanja tayari na nafanya mpango ndani ya mwaka huu niwe na viwanja kama viwili hivi kisha mwakani niwe na viwanja viwili tena jumla vinne kwa uwezo wa mungu..

kisha hapo naanza kufikiria biashara ya kufanya ,
Safi sana mkuu, unatupa moyo na sie wengine kuona kua mambo yanawezekana kama hutojali kwa upande wa changamoto katika suala la saving ipi ilikupata na ulipigana vipi kuishinda mana kwangu changamoto ni kua na save lakini shida inapopiga hodi hua ni majanga inakomba hela yote naanza na moja sasa sijajua kua tatizo ni amount ninayo save ni ndogo (kulingana na kipato changu) mpaka saving yangu inashindwa kuhimili changamoto za kiuchumi mara zitokeapo au nini? (i don't know) Na je, mwenzangu ulikua unatumia njia gani ku save kwa kuweka bank (saving acc) au ulifungua fixed acc special for saving only? Au kuweka m-pawa kama njia ninayoitumia mimi?
 

marrykate

JF-Expert Member
Mar 4, 2012
717
500
The best way ya kufanya savings,ikifika mda wa mavuno nunua chakula cha kutosha, nunua friji yako,ukiwa na mchele hada debe 5 kwa wenye familia,na gunia la mahindi na lita kumi ya mafuta ya alizeti huo mwaka unakupita poa kabisa,kila mwisho wa mwezi nenda na sh arobaini kanunue kauzu na maharage nyanya nk nk huwezi amini route za kwa mangi kila siku mara nipe una robo nk,

Lakini ukinunua mazaga yako mfano carot unayouziwa wewe gengeni sh 200 ukienda karume unapata sadolini kwa 5000 ukiweka kwenye friji si zinakupiga kick, sado ya nyanya 4000 nk,unaweza kuta kila siku pay inayotoka mfukoni haizidi hata 3000 kwa mboga.utashangaa bajeti yako kwa mwezi kwa chakula tuu hazidi 70000 out of lakini naa,sasa hapo huja save bado?

Hapo home machalii unawapiga na uji poa wa lishe,maisha haya bila kuwa na bajeti usawa wa uncle magu hutoboi,mi kuna mzee nilimshuhudia analipwa 150000 na alikuwa anaishi hivyo huwezi amini anasomesha watoto shule kali tuu, yeye anakwambia mi dukani huwa sikanyagi kununua chakula labda niamue mwenyewe

lita kumi mwaka mzima, unatania wewe labda kama upo peke yako
 

Dharra

JF-Expert Member
Jun 23, 2017
1,667
2,000
Jiulize kwanini wakina Mark Zuckerbeg mmiliki wa facebook anarudia nguo? ya jana anavaa leo pia na ni milionia? Matumizi yasio ya lazima ndio yanatukosti wengi, jaribu fanya hivi. Weka malengo unataka kufanya nini, akili yako iweke kwenye malengo yako na usitetereke, Weka akiba na kitakachobaki ndio utumie na sio unatumia na kinachobaki ndio unaweka akiba, Tumia muda mwingi kwenye kazi, wachina wanafanikiwa kwa sababu wanalala masaa machache sana muda wote ni kazi tu. Mama mmoja wa kichina anamiliki duka kariakoo mchana kutwa yupo dukani usiku anafanya kazi kama massage therapist hoteli flani kubwa hadi saba usiku, kwa siku anapumzika masaa 6 tu. Nakumbuka kipindi nafanya kazi posta kuna msichana mmoja kazi yake ni office attendance. Akitoka hapo office saa kumi na moja mbio anakimbilia kariakoo ananunua mzigo wa viatu vya bei rahisi kwa jumla anamwaga chini kwenye kiroba anauza. Anafanya kazi mpaka saa tatu usiku ndio anarudi nyumbani, alianza na mtaji wa elfu 50. Sasa amekodi majiko kwenye Bar mbili tofauti, yupo mbali sana
 

Kete Ngumu

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
6,067
2,000
Hichi ulichokisema hapa niliwahi kukifikiria na kubadili kabisa kuwaza watoto wangu wawe nani, yani daktari, mwanasheria n.k, nitawapitisha njia itakayowafanya wajiajiri waachane na kuajiriwa kabisa wala wasiwaze.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom