Hiki Kisa kilitokea Singida miaka 99 au 2000 kwa Mshkaji wangu, Huyu jamaa wakati akienda kwenye shughuli zake alimuona mtoto wa miaka kama 8 akitembea barabarani, akasimama na kumuuliza we dogo unaenda wapi? Maana aliona kama amepotea, dogo akasema anaenda singida kijijini, jamaa kusikia hivyo akajua huyo dogo ni mgeni Singida. Akamuuliza unatoka wapi akasema ametoka Dar. Mshkaji akamwambia Panda gari, Kwenye mazungumzo jamaa akagundua kuwa huyo dogo ameachwa stendi ya Bus na mzazi wake, na sababu kuu ni kuwa mama wa kambo alikua hamtaki huyo mtoto,Jamaa akamwambia dogo kama wao hawakutaki basi utaishi na mimi kama mtoto wangu. Huyu mshakaji alimchukua huyo dogo na kumpeleka kwake(jamaa alikua na Uwezo) Dogo alishi hapo , mahitaji yote alipewa kama watoto wengine wa hiyo nyumba, mwisho alipelekwa mwanza kusoma na kuishi na wazazi wa huyo mshkaji. Kwa ujumla huyo dogo aliishi na hiyo familia kwa takriban miaka kumi, hii familia ni waarabu na dogo alikua ni mkristo lakini walimchukulia kama mtoto wao na wala hawakutaka kumsilimisha. Dogo alivyo kua akaona maisha ya nidhamu, shule hayawezi akaamua kutimua zake. Hii familia mpaka leo ina masikitiko maana wameona kama mtoto wao amepotea, Huyo mshkaji sitakuja kumsahau maishani mwangu.