Ulisimama for 3 days duh pole sana mkuuMiaka mingi imepita kama 25 hivi, nikiwa nmetokea arusha na uporipori wangu nikaingia jijini. Safari ilikuwa ya kuelekea mtwara shule kwa masomo ya A level, dar sikuwa na ndugu nnayemfahamu na isitishe mawasiliano wakati ule ilikuwa mbinde. Nikashuka zangu na basi la fresh ya shamba nikatua ubungo terminal. Kwa sababu sikuwa na mwenyeji dar nilala pale stand. Kwa Bahati mbaya nilipotoka arusha nilikuwa nmepewa taarifa zisizo sahihi hasa nauli ya nnakokwenda kutokea dar. Niliambiwa nauli in tsh 5000 ilhali ukweli nauli ilikuwa mara 3 yake. Nikaanza kuzungukia mabasi kutafuta nauli nafuu kuanzia akida hadi WiFi naye. Kumbe katika zunguka yangu wajanja wa Ubungo wakawa waneninasa na shida yangu, waninyemelea wakanipa tuketi kwa bei niliyokuwa nayo. Asubuhi naenda kituo walichoniambia wanapaki gari zao kumbe holaaaa...hakuna kitu. Niliangaika sana kituoni. Baadaye akatikea jamaa mmoja akaniuliza na mie nikamueleza yaliyonipata. Alinipa msaada mkubwa sana, akanikimbiza hadi Sudan ya temeke, akawaeleza makonda kilichonipata, hatimaye nikapewa tiketi yenye herufi 'KK' maanake kusimama! Gari ilikuwa inaitwa misungwi, nilifika masasi baada ya siku tatu nikiwa nmesimama tokea dar. Yule jamaa sikumuona tena, huwa natamani kukutana naye siku moja nimpe asante na nimuambie mm ndo niliyekuwa nalia na kuburuza begi miaka hiyo 29+ akanisaidia hadi nauli ya dalaldala kufika Sudan.
Abuu bin Umar ni vibaya Sana mtu kakosea kutuma hela au kitu chochote kikakufikia wewe ukachukua Hali ukijua kuwa amekosea.. Last week nilitumiwa hela ya kupeleka rambirambi msibani namba ikakosewa ikaenda kwa jamaa mwingine pamoja na kumweleza ni hela ya nini bado aliichukua. Sasa najiuliza huyu si kama anajeletea laana kwa kujua? Kwangu naona ni uungwana kurudisha na si kukimbilia kwa wakala kuitoaDaah! Kuna jamaa pale Tunduma ,alinirudishia pochi yangu baada ya kuidondosha , ndani yake mlikua na drivers licence yangu na pesa za nchi mbalimbali zote zikiwa na thamani ya kama 3 million kama ningezibalidilisha kwa shillings, sikuamini , yule jamaa nilitaka kumpa pesa kidogo kama shukrani lakini huwezi amini,' alikataa!
Kumbe na wewe ulikuwepo kwenye uvamizi ule saa 11 alfajiri munaturushia mawe kama mvua .
pole sana mkuu .
Kuna methali inasema asiyekujua hakuthamini. Hii sikubaliani nayo sana. Kuna wakati asiyekujua anaweza kukuthamini kuliko anayekujua. Yamenikuta mimi. Nilienda nchi za watu, watanzania walinikwepa ila watu kama waethiopia na wanaijeria ndo waliokua tayari kunisaidia. Nilishangaa mno
very touching mkuu, nahisi hapo ni milambo bila shaka
HeMie nakumbuka ilikuwa Mwaka 2015 nlienda Morogoro kikazi na ndo ilikuwa mara ya kwanza kufika Morogoro wakati nahangaika kutafuta hoteli nikaibiwa pochi,nkabaki napiga makelele ovyo, bahati nzuri kuna mkaka alikuwa anapita na aliona hilo tukio akaja akanipa pole akanambia dada unaenda wapi kwani nkamwambia mm ni mgeni nilikuwa natafuta hoteli akanichukua akanilipia hotel akanipeleka kula akanipa na pesa kidogo, alinisaidia sana , kesho nikampigia boss wangu nmepata matatizo akanitumia pesa nyingine, ni tukio ambalo kamwe sitalisahau maishani mwangu,amekuwa kama kakaang wa damu kabisaaaaa watoto wake likizo zingine wanakujaga kuniona, Mungu wa ajabu sana jamani
Amini kwa namna ya ajabu sana kuna siku utalipwa kwa mema uliyofanyaMi nilimuokota majeruhi wa ajali ya gari Mandela Rd enzi hizo ni barabara moja!
Ilikuwa usiku, watu wakawa wanamgwaya, nikajitolea kupigania uhai wa dada yule.
Nikiwa na masela wa Kijiweni, tuliweka mabench ya saloon ili kufunga barabara kwani gari iliomgonga ilikimbia na gari nyingi zikawa hazitaki kusimama kutoa msaada.
Baada ya kufunga barabara kwa mabench, ilikuja Toyota nadhani STH ama SU, nikiwa nimetoka tu A level, nikapata ujasiri wa kuongea na dereva yule mtu Mzima kwa kifupi na huruma, akanipa mashart kuwa tumpeleke mgonjwa hospital pasi na kupita Police na vile vile yatakayojiri hospital hayamuhusu! Nikakubali.
Tulifika MUHIMBILI na mgonjwa wangu akahudumiwa baada ya KUKUBALI KUKUNJUA MKONO, of course (nilikuwa Mwl wa tuition so nilikuwa na vijihela kidogo) nilijiongeza baada ya kuambiwa eti mtu wa X-Ray kalala!
Dada yule alikuwa amevunjika mguu, pia alikuwa na maumivu ya mbavu! Police wa pale Super star walikuja na wakanihoji, kisha tukapata PF3.
Ndugu wa dada yule walikuja usiku kama Saa 7, wakanikuta bado napigwa nenda rudi ktk vicorrido vya muhimbili.
Kufika kama Saa 8 police walinchukua niwapeleke eneo la tukio ili wapate vipimo vya ajali!
Asubuhi nilienda muhimbili kumjulia hali manusra wangu na kiukweli alifurahi sana, ndugu zake walinisifu na kunishukuru sana!
Walitaka kunirudishia gjarama za matibabu, nikakataa.
Alihudumu mgonjwa wangu pale wodini kama siku 10 kisha akaruhusiwa, nikawa naenda kumjulia hali kwake Ubungo!
Nashukuru dada yule alipona, mara ya mwisho alijoin UDSM na mawasiliano yalishakufaga!
Dunia Mapito tu, ubinadamu ndio kila kitu!
na bado unaendelea....?NILISHASAIDIWA SANA .Mungu ni mwema sana sana
siwezi hata kueleza
mtafute huyo bintiMimi mwaka 2010 nikiwa dodoma pale stand ilikuwa usiku ninatafuta gari ta kuja dar kesho yake magari yote yamejaa maana UDOM walikuwa wamefunga na st.john.
Sasa wakati nimekata tamaa akanifuata jamaa flani akaniambia kuna Yutong mpya nilikuwa na rafiki yangu tukakata tiketi zetu.
Then tukasema tukatafute sehemu ya kulala.
Wakati ninaondoka **** binti mdogo pale alikuwa kati ya miaka 15-17 hivi sema ana mwili mwili flani akanifuata.
Akaniambia kaka mimi nina shida, nikamuuliza shida gani.
Akasema kuwa alikuwa anatoka dar kwenye kesi ya mirathi ana mjomba wake pale dodoma alikuahidi akifika dodoma atampokea alale kwake ampe nauli ya kuelekea tabora maana alikuwa anaenda Tabora. Sasa toka amefika anampigia simu hapokei na hana mtu mwingine wa kunsaidia alikuwa na dada yake flani amempigia anememjibu kuwa hana ela.
Mida hiyo ilikuwa saa tatu usiku nikaona anazingua tu atakuwa anataka kuntapeli nikamwambia sina ela nikaondoka na jamaa yangu.
Jamaa yangu akaniuliza huyo dada alikuwa anakwambia nini nikamwambia, akasema ungemchukua ukalale naye mimi nikamwambia haa siko katika mood hiyo kama anamtaka akamfuate.
Baada ya kutafuta sehemu ya kulala tulikos maana wanafunzi walikuwa wamejaza nyumba zote za wageni ilabidi turudi pale stand tukaensa bar flan tukaanza piga urabu mpaka bar ilipogungwa.
Tukaenda lala kwenye lile basi nikamkuta yule binti amekaa na watu wengine ambao walikuwa nao wasafiri wanaolala stendi.
Nikamwita nikamwambia asubuhi nitamkatia tiketi ya kwenda Tabora.
Then nikamwambia kama anataka anaweza kulala kwenye basi maana tumeambiwa na wenye basi kuwa tunaweza lala mle.
Basi kutokana na urabu nikasinzia sa sijui mwenzangu na yule binti nini kiliendelea.
Asubuhi jamaa yangu ananiambia amemtongoza wamekuwa wapenzi nikimcheki binti namuona innocent nikamuuliza uko kidato cha ngapi akaniambia cha tatu.
To cut the story short nilimkatia tiketi bus lao liliondoka kabla yetu na nilimpa ela ya kula njianu hata namba yake sikuomba.
Baada ya week kama mbili nikapokea simu toka namba mpya mkumbe yule binti akaniambia kampigia yule rafiki yangu akamuomba namba yangu.
Toka siku hiyo akawa ananipgia mimi badala ya jamaa sema sikuwa namtafta na namba nikabadirisha.
Kitambo sana mkuu, mara ya mwisho kuwasiliana naye nadhan ni 2012 alikuwa kaja dar akanipigia kuwa yuko dar anaomba tuonane... mimi nilikuwa nimesafiri niko mkoabhuko kanda ya ziwa na nilibadiri namba...mtafute huyo binti
Na ubarikiwe sana ndugu. Nadhani kwa msaada huo uliotoa ulizidi kubarikiwa zaidi na matunda yapoMi nilimuokota majeruhi wa ajali ya gari Mandela Rd enzi hizo ni barabara moja!
Ilikuwa usiku, watu wakawa wanamgwaya, nikajitolea kupigania uhai wa dada yule.
Nikiwa na masela wa Kijiweni, tuliweka mabench ya saloon ili kufunga barabara kwani gari iliomgonga ilikimbia na gari nyingi zikawa hazitaki kusimama kutoa msaada.
Baada ya kufunga barabara kwa mabench, ilikuja Toyota nadhani STH ama SU, nikiwa nimetoka tu A level, nikapata ujasiri wa kuongea na dereva yule mtu Mzima kwa kifupi na huruma, akanipa mashart kuwa tumpeleke mgonjwa hospital pasi na kupita Police na vile vile yatakayojiri hospital hayamuhusu! Nikakubali.
Tulifika MUHIMBILI na mgonjwa wangu akahudumiwa baada ya KUKUBALI KUKUNJUA MKONO, of course (nilikuwa Mwl wa tuition so nilikuwa na vijihela kidogo) nilijiongeza baada ya kuambiwa eti mtu wa X-Ray kalala!
Dada yule alikuwa amevunjika mguu, pia alikuwa na maumivu ya mbavu! Police wa pale Super star walikuja na wakanihoji, kisha tukapata PF3.
Ndugu wa dada yule walikuja usiku kama Saa 7, wakanikuta bado napigwa nenda rudi ktk vicorrido vya muhimbili.
Kufika kama Saa 8 police walinchukua niwapeleke eneo la tukio ili wapate vipimo vya ajali!
Asubuhi nilienda muhimbili kumjulia hali manusra wangu na kiukweli alifurahi sana, ndugu zake walinisifu na kunishukuru sana!
Walitaka kunirudishia gjarama za matibabu, nikakataa.
Alihudumu mgonjwa wangu pale wodini kama siku 10 kisha akaruhusiwa, nikawa naenda kumjulia hali kwake Ubungo!
Nashukuru dada yule alipona, mara ya mwisho alijoin UDSM na mawasiliano yalishakufaga!
Dunia Mapito tu, ubinadamu ndio kila kitu!
Amin ndugu yangu.Amini kwa namna ya ajabu sana kuna siku utalipwa kwa mema uliyofanya