Let's share: Uliwahi kusaidiwa na mtu usiyemfahamu kabla (msamaria mwema)? Kipi kilitokea?

Mwaka 2013 nikiwa nimepitka hali ngumu baada y kumaliza chuo niko nyumbani tu , niliamua kwenda tanga kufanya kaz ndogo ndogo ili nipate mtaji ,niliwaza kwenda kulimia watu mashamba na kufyeka ,nilipanga kutumia usafir wa roli kutok mwanza Dom, then dodom tanga , nilipo fika Dom nilikuwa n kias kidogo sana niliunga unga hadi kufikia gairo,hap gairo nilipata lift ya bure hadi moro, morogoro nilisaidiw n fuso hadi chalinz fuso hii ilibeba miwa, nilifka chalinz usik mida ya SAA 5 nikiwa na elfu mbili tu nikala mandaz na mawiza fresh ,usiku SAA kumi nilianza safari niitafut muheza ,aisee nilitembea sana bila kupata msaada wowote, mida ya SAA 1 kuelelea saa2 nikiwa nimechoka sana ilikuja basi zuri sana likapaki mbele yangu kisha akashuka konda akiwa na kitu kama chuma akawa anagongagonga tairi kupima upepo nikajihis nieleze ukwl kuwa nimekwama naenda tanga, konda alishangaa sana akamweleza dreva akaniruhusu kuingia, hapa nilikuwa na panda basi moja zuri sana modern coach dar to? Nilikuta kwenye basi kuna siti moja tu imebaki inanisubiri kwa hal niliy kuwa nayo niliona nimependelewa sana , gari lilitembea mwendo mrefu sana n tukafika segera walinishusha na nilipewa elfu 30 na konda ikanisaidie, hiki kitu nakikumbuka na kimenifanya niwe na roho ya kusaidia sana ukwel nikiwa long safar kwa SSA huwa siwapiti watu ninao hisi wanaelekea muelekeo wangu , nimekuwa nikijitahid sana kumwona Huyo konda na dreva wake ili sijafanikiwa kuwarudishia fadhila watu hao ila nawaombea kwa mungu mafanikio

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli umenifanya nikumbuke mwaka 2002 wakati huo nikiwa form six pale Malangali, nilitoka Dar likizo na kurudi shule kwa bahati mbaya niliposhukia kituo cha Mbalamaziwa ili nipande gari ya Malangali muda ulikuwa umeisha maana mwisho wa usafiri wa kutoka Mbalamaziwa kwenda Malangali ilikuwa saa 12 jioni kwa wakati huo, nami nilifika maeneo haya Mbalamaziwa saa 3 usiku, na umbali wa kutoka hapo kituoni mpaka Malangali ni kilometa 18 kupitia msitu wenye wanyama kipindi hicho. Pale Mbalamaziwa nikaingia mgahani kula chakula cha usiku kisha nikajieleza kwa mama lishe kuwa mimi ni mwanafunzi na nimekosa usafiri wa kwenda shuleni, yule mama akamuita mwanae wakiume ili nikalale naye nyumbani kwake. Ukweli alinisaidia sana kwa siku. Nakumbuka sana hilo tukio kila niitumiqpo hiyo barabara safari za nikoani.
 
Ni kweli umenifanya nikumbuke mwaka 2002 wakati huo nikiwa form six pale Malangali, nilitoka Dar likizo na kurudi shule kwa bahati mbaya niliposhukia kituo cha Mbalamaziwa ili nipande gari ya Malangali muda ulikuwa umeisha maana mwisho wa usafiri wa kutoka Mbalamaziwa kwenda Malangali ilikuwa saa 12 jioni kwa wakati huo, nami nilifika maeneo haya Mbalamaziwa saa 3 usiku, na umbali wa kutoka hapo kituoni mpaka Malangali ni kilometa 18 kupitia msitu wenye wanyama kipindi hicho. Pale Mbalamaziwa nikaingia mgahani kula chakula cha usiku kisha nikajieleza kwa mama lishe kuwa mimi ni mwanafunzi na nimekosa usafiri wa kwenda shuleni, yule mama akamuita mwanae wakiume ili nikalale naye nyumbani kwake. Ukweli alinisaidia sana kwa siku. Nakumbuka sana hilo tukio kila niitumiqpo hiyo barabara safari za nikoani.
Kumbe umesoma kwetu mkuu!!? Ulikuwa comb. gani? Mimi pia nimesoma malangali O'level mwaka 2001 to 2004
 
Mm kuna dada mmoja anaitwa dominica meena sitamsahau wakt nipo sec. Boarding yeye yuko chuo alinisaidia bila kunifahamu. Nilikuwa na anwan yake ya posta lakn ckuwah kumpata baada ya hapo. Kwao ni moshi. That was late 90's. I wish ningejua yuko wap now
 
mimi kuna siku nilipost kitu ambacho nadhani wengi hawakukipenda kuna mwana jf mmoja alinitetea sana aisee kila comment negavitive aliijibu tena kwa mkwara....Mungu ambariki
The same applies to me mkuu

Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
 
Ndio sababu huwa sikatai kuwa kuna waislam kamili sio wabwabwajaji.

Mwaka 2010 mwezi wa 8-10 katika jiji flan nilisaidiwa sana na jamaa mmoja aliyeitwa Sadick (Mzaliwa wa Tanga) na wakati huo ndugu yangu alinipotezea bila sababu.

Hakuwahi kuniona kama mtu baki ila alinitreat kama mdogo wake kabisa na kuna wakati alijinyima kwaajili yangu.

Alipohitaji pia msaada wake na wadogo zake kwa Arusha nilimsaidia vilivyo.

Kwasasa tumekuwa kama ndugu kabisa.

Nilichojifunza katika maisha ya Mwanadamu ni kuwa:

"Usimdharau binadamu yeyote yule eti kwakuwa hana pesa ama elimu"

Unaweza kupata shida kubwa ukasaidiwa na usiyemjua.
 
Sitamsahau kaka Fulani nilikutana nae Arusha pale mianzini wakati nasoma chuo,,nlikua naeleke hospitali ile ya ENT ipo tanki la maji,nikasimama katika bar ile barabarani nile nlikua na njaa..
Nkakaa meza moja na mkaka hvi simjui,chakula kilivokuja nkamwambia waiter aisee chps zenu ndogo bora ningekula ndizi,yule kaka baada ya mda baada ya kuniskia nalalamika akamwita waiter akamwambia aniletew "rosti" aniongezee na chps...akaniuliza nlipokua naelekea,akampgia simu rafiki yake daktari nikaongea nae akanielekeza hospitali aliopo..bill ilivokuja akanilipa chakula na vinywaji jumla 18,000/=..(bill hii kwa kipindi nasoma chuo ni kubwa mno)
Baadae akaniaga akaondoka,,,hakuniomba namba ya simu wala kuniuliza jina...nlimshangaa ila alinisaidia maana nlikua na njaa na budget ilikua ef 5000 tu..

Namuombea kwa Mungu amfungulie milango ya rizki yule kaka..!!
Kuna watu wana mioyo ya ajabu sana,nataman nimuone tena ila ndo siwezi mkumbuka kabisa,ila natumai dua zangu zinamfikia.
Heee kumbe upo dada za siku nimimi nilikusaidia naomba namba sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitasahau nilisaidiwa nikiwa zangu shuleni A-leve na madam nilipo hibiwa pesa za nauli za kutoka mkoani songwe hadi Lindi ukizingatia wazazi wameniambia nisubiri mwisho wa mwezi na shule tumefunga mwezi mmoja -madam akanichukua nikawa naishi kwake likizo yote niliishi kwake na mahitaji yote muhimu alinipatia hapo ndipo nilipoaza kupenda walimu zaidi nikajua msaada sio darasani hata ñje.walimu mpoo juuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeufatilia huu uzi toka mwazo hadi hapa, nimejifunza mengi sana, dear God nipe uwezo nisaidie wengine.Amen
 
Back
Top Bottom