Let's be real: Zaidi ya Bilioni mbili kwa Semina Elekezi!?

Let's be real: Zaidi ya Bilioni mbili kwa Semina Elekezi!?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Wakati akijinadi kwa wapiga kura, Rais Magufuli alikuwa kila mara anasema nchi yetu ni tajiri na anafahamu sehemu ambazo pesa zinavuja zikiwa njiani kuwafikia wananchi wa kawaida.

Kadri siku zinavyopita, Rais Magufuli ameanza kutuonyesha njia za panya na panya waliokuwa wanatafuna pesa za wananchi wa kawaida.

Hii hoja inaweza ikawa imefunikwa na tukio la majina ya mawaziri wapya lakini Serikali kupanga kutumia zaidi ya shilingi bilioni mbili kwenye semina za Mawaziri ni ufisadi wa aina yake. Haya ni matumizi mabaya sana ya pesa za wananchi. Hata wale waliokuwa wanatengeneza bajeti hii wanafaa kuwa gerezani na kuchapwa viboko 12 wakiingia gerezani na 12 wakitoka ili wakawaonyeshe wake/waume zao.

Ni dhambi kubwa kutenga zaidi ya bilioni mbili kwa ajili ya semina elekezi wakati kuna wagonjwa hawana hata sehemu ya kulala hospitalini achilia mbali kupata madawa. Ni dhambi kubwa kutenga zaidi ya bilioni mbili kwa ajiri ya semina elekezi wakati vijana wetu wa taifa la kesho hawana hata madarasa, madawati, vitabu na walimu wa kutosha wanaolipwa at least living salary.

Hii ndiyo hasara ya kuwa na viongozi ambao maisha yao yote ni kwenye ofisi zenye imported car, furniture, fixtures and equipment. Wanafahamu zaidi kinachoendelea kwenye nchi za Magharibi kuliko kinachoendelea mikoani. Kuna wengine ninaamini hata ukiwauliza hawawezi kukutajia majina ya mikoa yote nchini achilia mbali kama wamewahi kufika kwenye mikoa hiyo. Kuwauliza majina ya Wilaya ni kuwaonea!

Hii inaonyesha ni jinsi gani taifa kwa sasa linavyokabiliwa na athari ya tofauti kifikra na kimtazamo kati ya wenye nacho (kielimu na kimapato) na wale wasio nacho. Kwa sasa tuna viongozi ambao miili yao iko Tanzania lakini fikra zao ziko kwenye nchi za Magharibi. Hata priority wanazozipanga zinakuwa ni kama za nchi za kimagharibi wakati ni viongozi wa taifa ambalo wananchi wake bado wanakufa kwa ugonjwa wa kipindu pindu.

Kwa mentality hizi za maofisa waandamizi wa serikali, sina shaka ninaposema kazi aliyonayo Rais Magufuli ni kubwa sana!
 
Makatibu wakuu wazee wa bajeti na safari za nje mikutano semina warsha makongamano unategemea nini
 
Well spoken bro! Mkwere anastahili kuondolewa kinga ashitakiwe na kuadhibiwa kama Mfalme Haile Sellasie wa Ethiopia enzi hizo; afungiwe kwenye chumba cha giza na unyevunyevu akipewa unga mkavu na mende kama chakula na kitoweo!
Kameumiza sana wananchi! Heko JPM kwa kutufungua macho; lakini kaza kamba; tunakuombea afya njema na salama. Wezi na wabadhirifu watashindwa kwa jina la Yesu.
Wakati akijinadi kwa wapiga kura, Rais Magufuli alikuwa kila mara anasema nchi yetu ni tajiri na anafahamu sehemu ambazo pesa zinavuja zikiwa njiani kuwafikia wananchi wa kawaida.

Kadri siku zinavyopita, Rais Magufuli ameanza kutuonyesha njia za panya na panya waliokuwa wanatafuna pesa za wananchi wa kawaida.

Hii hoja inaweza ikawa imefunikwa na tukio la majina ya mawaziri wapya lakini Serikali kupanga kutumia zaidi ya shilingi bilioni mbili kwenye semina za Mawaziri ni ufisadi wa aina yake. Haya ni matumizi mabaya sana ya pesa za wananchi. Hata wale waliokuwa wanatengeneza bajeti hii wanafaa kuwa gerezani na kuchapwa viboko 12 wakiingia gerezani na 12 wakitoka ili wakawaonyeshe wake/waume zao.

Ni dhambi kubwa kutenga zaidi ya bilioni mbili kwa ajili ya semina elekezi wakati kuna wagonjwa hawana hata sehemu ya kulala hospitalini achilia mbali kupata madawa. Ni dhambi kubwa kutenga zaidi ya bilioni mbili kwa ajiri ya semina elekezi wakati vijana wetu wa taifa la kesho hawana hata madarasa, madawati, vitabu na walimu wa kutosha wanaolipwa at least living salary.

Hii ndiyo hasara ya kuwa na viongozi ambao maisha yao yote ni kwenye ofisi zenye imported car, furniture, fixtures and equipment. Wanafahamu zaidi kinachoendelea kwenye nchi za Magharibi kuliko kinachoendelea mikoani. Kuna wengine ninaamini hata ukiwauliza hawawezi kukutajia majina ya mikoa yote nchini achilia mbali kama wamewahi kufika kwenye mikoa hiyo. Kuwauliza majina ya Wilaya ni kuwaonea!

Hii inaonyesha ni jinsi gani taifa kwa sasa linavyokabiliwa na athari ya tofauti kifikra na kimtazamo kati ya wenye nacho (kielimu na kimapato) na wale wasio nacho. Kwa sasa tuna viongozi ambao miili yao iko Tanzania lakini fikra zao ziko kwenye nchi za Magharibi. Hata priority wanazozipanga zinakuwa ni kama za nchi za kimagharibi wakati ni viongozi wa taifa ambalo wananchi wake bado wanakufa kwa ugonjwa wa kipindu pindu.

Kwa mentality hizi za maofisa waandamizi wa serikali, sina shaka ninaposema kazi aliyonayo Rais Magufuli ni kubwa sana!
 
Viongozi wetu wamekosa uzalendo....wanajali matumbo yao.....ndio maana hawaoni aibu kupanga vitu vya kipuuzi kama hivi....
 
Uozo wa yote haya ni katiba mbovu....inayowalinda watenda maovu........viongozi waliofisadi taifa hili kwa miaka mingi hawahitaji kufungwa maana bado watakuwa wanatumia kodi za wananchi masikini kuwahudumia gerezani....wanatakiwa kunyongwa maana uwepo wao hapa kwenye uso wa ardhi ya tanzania ni kama dhihaka kwa wanyonge na walalahoi wa taifa hili........ENOUGH...
 
Magufuli mwenyewe hakupewa semina elekezi sasa hawa wengine wapewe semina elekezi kwa bajeti kubwa kiasi kwa sababu gani? Hyo hela ikapunguze madeni ya watumishi wa uma!
 
yaliyopita si ndwele tunaganga yajayo kwa sababu tukianza kuchokonoa mambo ya nyuma jamani, mgombea wetu mwenye skandali ya Richmond ataswekwa ndani tuanze kulialia hapa. nawaambia sisi tumemsafisha kisiasa na tukauaminisha umma kuwa sasa anafaa kuwa rais wa nchi hii. ngoja aje Magufuli ndio utagundua aliyoyowahi kuyafanya akiwa serikalini.
hii pia inamhusu kampeni meneja wake Sumaye! chini ya mtetezi wao Kingunge.
unadhani kwa nini wamekaa kimya kama maji ya mtungini? ?? kwa sababu wanajua maovu yao, wakisema fyo Magufuli atawalipua wanajua kabisa Magufuli hana breki. he cant spare anybody
 
Hii ni DHAMBI KUBWA SANA wale wote Waliyoifanya na kupanga BAJETI ZA ULAJI WAFAHAMU DHAMBI HII ITAWAANDAMA DAIMA NA MWISHO WAO SIO MWEMA KULA NA KUTUMIA HAKI NA MAPATO YA WAVUJA JASHO WA NCHI HII.MH.RAISI TUNAKUOMBEA UIPONYE NCHI HII NA VIRUS VILIVYOWAKUMBA WATENDAJI WA SERIKALI YAKO NA HAO WALIYOKO NJE YA SERIKALI YAKO BIMANA WACHORAJI WA MA-DEAL KUIBIA NCHI
 
Matumizi ya shilingi bilioni 2 kwa ajili tu ya semina elekezi ya baraza la mawaziri pale Ngurdoto?!
Wakati wizara ya utumishi inapanga bajeti hiyo inajua wazi kuwa kwenye mahospitali yetu wagonjwa wanalala chini.
Kwenye shule zetu wanafunzi wetu wanakaa chini sakafuni.
Wanafunzi wa vyuo vya juu kwa maelfu wanakosa mikopo.
Aisee...... kilichokuwa kinafanywa na viongozi wetu wa juu kwenye hii serikali ya CCM ni kufuru ya hali ya juu kwa Mwenyezi Mungu!
Kwa matukio ya aina hii, naanza kushawishika kumbe nchi kama China kupitisha sheria ya kuwatwanga risasi hadharani viongozi wa design hiyo walikuwa perfect right.
 
Hizo Semina elekezi itolewe tu handout kama Ya Lecture, then mwisho wa kusoma hizo handout kila mtu anafanya mtihani, chini Ya marks 60 unavuliwa uwaziri
 
Kwa kweli kwa namna Magu anavyoendelea kuweka hadharani kila kukicha, maovu mengi yanayofanywa na viongozi wenzake waandamizi ndani ya serikali yake ya CCM, inabidi kila mwananchi aendelee kuongeza maombi kwa Mungu ili aendelee kumlinda Rais wetu.
Kwa kuwa ni dhahiri kuwa hatua anazochukua Magu hivi sasa zinawaathiri sana watu ambao wako so powerful economically and politically.
Kundi ambalo ni so dangerous.
 
Magufuli tumpongeze kwa kutujulisha haya mauzauza yaliyofanywa. Na anafanya hivi kwa dhamira tujue udhaifu wa awamu iliyopita na matumizi ya anasa aliyokuwa akiyafanya mkwere.
 
Magufuli mwenyewe hakupewa semina elekezi sasa hawa wengine wapewe semina elekezi kwa bajeti kubwa kiasi kwa sababu gani? Hyo hela ikapunguze madeni ya watumishi wa uma!

Semina elekezi ilikuwa kale kadokumenti kenye kurasa 53 alikoachiwa na JK, hizo 53 ni pamoja na utangulizi, dibaji, table of content, executive summary, appendix na michoro...

Kweli raisi tulikuwa naye, no wonder alipata GPA 2.1
 
Naamni kuwa hata Ukawa wanaposema kuwa Magu anatekeleza sera yao ya kubomoa mfumo wa ulaji ndani ya CCM wako right.
Kwa kuwa tatizo la nchi hii halikuwa ubovu wa sera za CCM bali viongozi waandamizi ndani ya serikali ya CCM kuiona nchi hii ya TZ kuwa their own property!
 
Back
Top Bottom