Nimepata taarifa kutoka kwa mmoja wa rafiki zangu aliyepo Dar es Salaam, ameniambia kwamba Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Leticia Nyerere, amehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Tangu awali mbunge huyo alisakamwa na maneno mengi kutoka kwa viongozi wa Chadema akiwemo kwamba aachane na ubunge ndani ya Chadema ili ajiunge na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuliko kuendelea kukipigia debe chama hicho akiwa upinzani.
Hata hivyo, mbunge huyo anadaiwa kufanya matendo ya kujipendekeza kwa CCM kabla ya kujiengua na chama chake cha awali.