Let us think a little big

GedsellianTz

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
1,348
1,803
Inakuaje bibi kule kijijini asiyejua kusoma wala kuandika anaweza kufuga ng’ombe na kuku kuliko ‘msomi’ mwenye digrii ya mifugo anayelia njaa na hajui nini cha kufanya?

Inakuwaje mmachinga darasa la saba kariakoo anafanya biashara vizuri kuliko msomi mwenye digrii ya uchumi anayelia njaa na kutia huruma?

Inakuwaje mama kijijini anaweza kuchimba kisima cha maji na kutosheleza familia lakini mhandisi wa maji hawezi hata kuvuna maji ya mvua na analalama shida ya maji?

Inakuwaje msumkuma na mmasai aweze kufuga na kuzalisha maelfu ya mifugo wakati profesa wa ufugaji hawezi kufuga kuku hata mmoja na anashinda anailalamikia serikali?
 
Kuna kitu wanacho kwa kiswahili wanaita Uzoefu, kwa kingereza Experience
 
Muda wanaopata hao watu kufanya shughul naona km watu wa kijijini wanapata muda zaid
 
Muda wanaopata hao watu kufanya shughul naona km watu wa kijijini wanapata muda zaid
Lakini kumbuka hawa watu waliosoma wanaujuzi zaidi na wanaweza kuzalisha mara mia zaidi ya watu wa vijijini....tatizo kubwa ukikuta kijana mwenye degree ya kilimo anang'ang'ania kuishi dar wakati akiwa shamba ataweza kuitumia elimu yake vyema in a pratically way
 
Sawa nakubaliana na wew VP kuhusu inshu ya capital kwa kijana aliyemaliza Chuo mwenye degree ya kilimo je ataanzaaje kulima km hana mtaji na vi2 vingine km vile eneo nk
 
Back
Top Bottom