Leo tupeane uzoefu wako, unajua nini kuhusu huyu kiumbe vunja jungu? (Mantis) je ni kweli ana super natural kama wazungu wanavyoamini?

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,608
93,380
Ndugu wana nzengo amani iwe kwenu.

Leo kuna jambo naomba tushirikishane uzoefu limeniumiza kichwa muda mrefu sana.

Katika maisha yangu nimebahatika kuishi na wazungu kwa ukaribu sana kiasi kwamba nilipaswa kujuwa ukweli wa ninachokiuliza lakini wazungu ni wagumu kufunguwa codes, ukiwauliza wanakwambia just for fun.

Nimeishi kwa mabeberu, nimefanyakazi nao Africa kwenye tourist industry lakini kuna vitu nakosa majibu.

Nimefanyakazi kwenye hunting company, mpaka leo bado sijaelewa vizuri ukiacha trophy za meno ya tembo hawa wanyama wengine wana thamani ya trophy kwa zile pesa wanazospend kuja Africa?

Maswali ni mengi kuliko majibu, sasa tuache yote leo nataka kujuwa kuhusu wazungu wanaofuga Mantis (Vunja jungu) je ni kweli hawa Vunja jungu wana super natural? je ni za namna gani? Zinamsaidia vipi huyu anayewatunza Vunja jungu? Kuhusu Swala la kujifurahisha tu hilo nimelikataa ndani ya ubongo wangu.

Yani huwezi kuamini mzungu yupo ulaya au America maisha yake yote na uchumi wake wote unatokana na hawa Vunja jungu, je kuna siri gani? Kuna elimu gani ambayo wazungu wanaojuwa na hawatoi codes?

Yani Africa mtu unajitutumuwa kufuga Kuku, Ng'ombe, mbuzi na hutoboi, inakuwaje hawa jamaa wanatobowa kwa Vunja jungu? tena wanawachukuwa kwetu na kuwasafirisha kwa magendo?

Cc: Mshana Jr Rakims Pascal Mayalla

European_praying_mantis_(Mantis_religiosa)_green_female_Dobruja.jpg
 
Wazungu wanaakili hawabahatishi
Nataka tujikite na tuzame kwa undani, kuna kitu wazungu wanakijuwa lakini nadhani wamekula kiapo kabisa asijue mtu yeyote nje ya jamii yao.

Sasa si vibaya tukifanya vireseach vyetu wenyewe.

Ona kama Bongo zozo anazunguka dunia ukimuuliza source of income yake atakwambia ni forex trading, uwongo mtupu.
 
Waba akili sana wale watu,kuna vitu vingi wanavijua na sisi hatuvijui na hatutakuja kuvijua
 
Kwamba wanatumia movie kufikishiana codes wao KWA wao? Na wewe ulivyoangalia hizo movie ulielewa codes zozote?
Angalia movie ya Bruce inter the Dragon, wakati wapo kwenye mashua kutoka Hong Kong kwenda kwenye kisiwa cha Dragon kwenye ile mashuwa walikuwemo Bruce Lee, Jim Kelly, Jim Brown na wengine siwakumbuki, kuna Mantis walitumika pale walipiganishwa.

Hii movie Bruce inter the Dragon kama sikosei ilichezwa mwaka 1976, Vunja jungu alikuwemo kama hiden code.
 
Kwa vile wewe ulishaiangalia,tu(ni)saidie kuelezea kulikuwa na code gani mpaka ikaonekana ni ajabu
 
Wazungu sometimes hupenda kuyafanya mambo ambayo sisi tunayaona madogo, wao huyafanya makubwa. Mambo ambayo sisi tunayaona hayana maana wao huyafanya ya maana.

Unakuta mtu anatengeneza mechi ya mapigano kati ya vunja chungu na mende, nyoka au wadudu wengine hatari afu anaweka kiingilio cha pambano ambapo watu wanaingia kuangalia, au wengine wanafuatilia pambano hilo kupitia YouTube nk. Na kupitia pambano hilo unakuta mtu anavuna madolar ya kutosha. Afu mara nyingi vunja jungu ndo hushinda mapambano hayo 😂😂😂
Kuna pambano nimeshahudia vunja jungu akiuwa nyoka. Aisee vunja jungu yupo vizuri kwa kung fuu, na akikupiga roba moja tu kwisha habari yako. Maana ni mfano wa roba yenye mbao ya misumari.
 
Attachments

  • Screenshot_20230803-140813.png
    Screenshot_20230803-140813.png
    185.8 KB · Views: 12
Back
Top Bottom