1. Viti maalum vifutwe maana vinachochea wizi wa kura za Rais na wabunge.
2. Kuwepo na ukomo wa mihula ya wabunge. Pendekeza mihula mitatu na mbunge asiwe na umri wa miaka zaidi ya 70.
3. Wabunge wachaguliwe kwa kura za uwiano
4. Watendaji wa kikatiba (CAG, CJ, DPP, n.k) wapatikane kwa usaili wa kushindanishwa.
5. Watumishi wa vyombo vya usalama (JW, Magereza, Polisi, Usalama wa Taifa, Takukuru, n.k) wasiruhusiwe kujihusisha na siasa baada ya kustaafu, ili kukwepa mgongano wa maslahi wanapokuwa wangali kazini.
6. Ushindi wa Rais upingwe mahakamani.
7. Wabunge kutoka Zanzibar, kwa ajili ya bunge la muungano (Dodoma), wasichaguliwe kwa majimbo bali kwa uwiano wa idadi ya watu katika kila upande wa muungano. Mfano, Tanzania Bara watu mil 48: Zanzibar watu mil.2; kama idadi ya wabunge wa muungano ni 100, basi Tanzania Bara itoe wabunge 96 na Zanziba wabunge 4.
8. Wakuu wa Wilaya na Mikoa wachaguliwe na wananchi.