Leo tume ya katiba iko eneo langu, nini ungependa niwasilishe ktk maoni?

Wakuu wote wa mikoa wachaguliwe na wananchi husika ili kuepusha malalamiko ya mara kwa mara Vile vile iundwe serikali ya majimbo ili kwa maana ya kuongozwa na mkuu wa mkoa ambaye kwa marekan humwita senator
 
Sera ya wizara ya mambo ya ndani itamke wazi polisi wote pamoja na jeshi lake ni kosa la jinai kutumia silaha dhidi ya waandamanaji wanaodai haki zao.
 
Wakuu wote wa mikoa wachaguliwe na wananchi husika ili kuepusha malalamiko ya mara kwa mara Vile vile iundwe serikali ya majimbo ili kwa maana ya kuongozwa na mkuu wa mkoa ambaye kwa marekan humwita senator[/QUOTE
sawa sawa mkuu
 
  1. Wabunge/Wawakilishi kutoka Zanzibar wasiwe mawaziri na makatibu wakuu kwenye wizara ambazo siyo za Muungano.
  2. Elimu ya chini kwa mgombea nafasi ya Urais wa JMT iwe first degree, na kwa nafasi za udiwani wa ubunge iwe kidato cha nne
  3. Mameya wa majiji/manispaa na wenyeviti wa Halmashauri wapigiwe kura na wananchi badala ya kupigiwa kura na madiwani tu
  4. Mbunge/diwani aruhusiwe kuhama chama bila kupoteza kiti chake. Pia mgombea binafsi kwa nafasi za URAIS, UBUNGE na UDIWANI aruhusiwe
  5. Watangayika waruhusiwe kumiliki ardhi Zanzibar kama Wazanzibaris wanavyomiliki ardhi Tanganyika kwasababu ZNZ ni sehemu ya JMT. Kama hilo haliwezekani basi na Wazanzibari nao wasiruhusiwe kumiliki ardhi Tanganyika.
 
1. Viti maalum vifutwe maana vinachochea wizi wa kura za Rais na wabunge.
2. Kuwepo na ukomo wa mihula ya wabunge. Pendekeza mihula mitatu na mbunge asiwe na umri wa miaka zaidi ya 70.
3. Wabunge wachaguliwe kwa kura za uwiano
4. Watendaji wa kikatiba (CAG, CJ, DPP, n.k) wapatikane kwa usaili wa kushindanishwa.
5. Watumishi wa vyombo vya usalama (JW, Magereza, Polisi, Usalama wa Taifa, Takukuru, n.k) wasiruhusiwe kujihusisha na siasa baada ya kustaafu, ili kukwepa mgongano wa maslahi wanapokuwa wangali kazini.
6. Ushindi wa Rais upingwe mahakamani.
7. Wabunge kutoka Zanzibar, kwa ajili ya bunge la muungano (Dodoma), wasichaguliwe kwa majimbo bali kwa uwiano wa idadi ya watu katika kila upande wa muungano. Mfano, Tanzania Bara watu mil 48: Zanzibar watu mil.2; kama idadi ya wabunge wa muungano ni 100, basi Tanzania Bara itoe wabunge 96 na Zanziba wabunge 4.
8. Wakuu wa Wilaya na Mikoa wachaguliwe na wananchi.
 
mawaziri wasiwe wabunge,wabunge wasiwe wakuu wa mikoa..huku ni kugonganisha mihimili
 
Katiba iweke wazi kuwa Rais atawajibika kwa makosa yote aliyotenda akiwa Madarakani hata kama yakibainika wakati ameshatoka Madarakani.
 
8. Wakuu wa Wilaya na Mikoa wachaguliwe na wananchi.
mkuu hao kwenye red wasiwepo kabisa..kazi yao inaweza fanywa kwa ufasaha na mkurugenzi wa halmashauri/mwenyekiti au meya
 
1. Kupiga marufuku neno Dollar kutumika kufanya biashara hapa nchini, pesa za madafu zinatosha
2. Kuvunja muungano yaani kuwe na nchi mbili tofauti Tanzania kivyake na Zanzibar kivyake
3. Mwanasiasa yeyote atoaye ahadi ya aina yeyote apewe muda fulani kutekeleza vinginevyo ajiuzulu.
4. Kiongozi yeyote aonae kazi imemshinda ajitolee kujiuzulu kuliko kung'ang'ania halafu hana idea mpya.
5. Viti maalum ni ufuska
6. Rav 4 iwe official Vehicle
 
Katiba mpya itamke kuwa WAJUMBE WA BODI IWE TAASISI/MASHIRIKA YA UMMA wapatikane kwa usaili wa kushindanishwa
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom